Dah Asante kiongozi kwa kunipa sifa.nami nazipokea,kwa sababu wewe ni moja ya vichwa makini sana humu jamvini.kupewa heshima hiyo na kichwa kama wewe ni heshima kubwa sana kwangu.
Nyongeza kwa Nini sisi wengine tunaiunga mkono Urusi kwa "baadhi" ya mambo yake.
Wakati wa ukoloni USA ilikua ndio rafiki mkubwa wa wakoloni,watesi wetu.
Viongozi wa Afrika wa wakati huo akina Nyerere,kwame Nkuruma,Patrice Lumumba,Keneth Kaunda,Robert Mugabe,Govan Mbeki,Nelson Mandela,Sam nujoma,Augustine Neto,Samora Machel,Jose Eduardo Dos Santos na wengi wengineo walianzisha harakati za kujikomboa kutoka makucha ya wakoloni.
USA Alikua alizisapoti nchi wakoloni kwa Hali na Mali,mbali na wakoloni aliwasapoti watawala wa Afrika ya kusini na Namibia ambao walikua ni makaburu.hawa walikua na mkono wa chuma zaidi hata kuishinda wakoloni wenyewe.
Walikua makatili,kwa kuua watu weusi,kubaka,kupiga,kufunga,kuwabagua na Kila aina ya mateso ikiwa ni pamoja na kuchoma nyumba zao.
Weusi wakaanzisha vikundi vya kujilinda na kudai uhuru na haki zao.
Nguvu za Urusi kijeshi,silaha na mafunzo.
Hakika nakuambia kama sio Urusi Hadi Leo Makaburu na wakoloni wangeendelea kutawala kwa mukono ya chuma.
Weusi waligundua kuwa Makaburu na wakoloni hawaelewi kabisa lugha za diplomasia na majadiliano ya kudai haki na uhuru wa mtu mweusi.
Lugha pekee ambayo wakoloni na Makaburu wangeielewa na kweli waliielewa sana,ni mtutu wa bunduki,vita,mapigano na ubabe.
Makaburu waliwahi kuua wanafunzi weusi wa shule kwa risasi.
Kilichofuata ni ukiua mtu mweusi na mweusi anaua mweupe.
Makaburu wakwa wanatumia uwezo wao wote wa kijeshi silaha na ujasusi na msaada kutoka UK,Israel,USA na France na German,.weusi wakawa wanazidiwa.
Hapa ndipo Urusi ikaingilia kati kwa kutoa misaada ya mafunzo,silaha,fedha,elimu,hifadhi na Kila kitu kwa wapiganaji wa kiafrika kutoka nchi yoyote ya Afrika iliyohitaji msaada wa namna hiyo.
Sio TU Urusi Bali Cuba,china na nchi nyingi za kisoshalist na kikomunisti ziliwasaidia watu.weusi kutoka na madhira ya Makaburu na wakoloni na hatimae Makaburu na wakoloni walishindwa kwa msaada wa Warusi.
Urusi pia ilisimama kidete huko umoja wa mataifa kuweka maazimio,mashinikizo na mapingamizi ili kuhakikisha wakoloni na Makaburu wanashindwa na walishindwa kweli.
Urusi ilijenga vyuo vya ufundi Tanzania mfano huko mbeya Kuna chuo matata sana Cha ufundi, na nchi nyingine za Afrika,
Ilisaidia kuyajenga majeshi ya Tanzania kisilaha na miundombinu ya kijeshi,mafunzo na mengi mengineyo.
Rubani mmoja matata sana na WA kipekee wa Kitanzania aliejifunza Urusi na kupata mafanikio makubwa sana ,alielisambaratisha jeshi la nduli Amini na baadae kuwezesha kujengwa kwa chuo imara kabisa Cha jeshi la anga Bora kabisa la Tanzania ni CDF (RTD)Robert Philemon Mbona,huyu mwamba pamoja na kusomea nchi nyingine Alipata kusomea Urusi.
(Kama Kuna makosa hapa Naridhia kusahihiswa)
Urusi hua Haina misaada yenye masharti kama wengine.
Urusi ni rafiki wa kweli kwa Waafrika.
Ule ugeni wa Rais wa USA wa wakati ule, George Bush ulipo kwenda kutembelea nchi moja ya Afrika kwa mbwembwe,walifanikiwa kuzima rada zote, wakati ndege ya Bush ilipoingia katika anga la nchi ile,lakini rada moja walishindwa kuizima, ambayo kwa kweli ni rada iliyotengenezwa Urusi.(made in Russia)
Naomba niishie hapa kwa Leo.
Wewe ni mtu mzima nadhani utakua umeielewa nchi hiyo.