Umeandika mambo mengi kwa point ndogo sana. Russia ni kubwa mara 28 zaidi ya Ukraine, Russia ilionekana ni ya pili kijeshi duniani wakati Ukraine hata top 20 haipo, Russia inaizidi Ukraine kiuchumi, inaizidi idadi ya silaha na wanajeshi na mambo mengi.
Sasa Russia tangu tarehe 24 February hadi leo inapigana na dogo Ukraine. Hapo ndio kuna superpower?
Hao hackers hata North Korea wapo, sio kitu cha ajabu hata Iran na Israel wanapokezana mashambulizi ya hacking. Russia mwanzoni tu walishindwa kuhack satellites za Elon Musk. Hakuna cyber war, ni enthusiasts wanaamua. Mbona walihack sites za Rosatom shirika la nyuklia la Urusi. Mbona walihack TASS shirika la habari la Urusi.
Misaada inayotolewa kila washirika wakijisikia, inayochelewa kufika, ambayo haitoshi. Hiyo siyo sababu ya msingi kwa jeshi linalodai lina silaha za kisasa na jeshi imara. Misaada iliyotolewa ni kama $10 billion, haifiki hata robo ya bajeti ya Russian military kwa mwaka. Russia wahangaishwa na hela ndogo hivyo miaka yote walikuwa wanajenga jeshi gani.
Russia ni nchi kubwa ila haina uwezo wa kusimama kwenye international arena kama inavyojiaminisha. Huwezi pigana na Ukraine ambayo ni jirani, unavuka tu mapori unamvamia ila unatumia miezi sita unahangaika kisha unajiona superpower. Huyu Russia akipata mission ya kuvuka bahari masafa marefu kupigana hata na Brazil hawezi