Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Duh. , Masikini Putin [emoji848].., jamaa kapoteza dira ya vita, hajui atamaliza vita kivipi, anachofanya ni kuendelea kupigana kiume Ili kuficha aibu anayopata lakini kihualisia jamaa ana uchungu sana moyoni kwa kuingizwa mkenge na washauri vilaza [emoji848]
 
Tazama video lile group linalotumia drone tu na hilux yao hawana mambo mengi ila wana vipa shida vifaru ya mrusi

 
Siku hizi habari za Ukraine front line kwenye vyombo vya habari vya magharibi unatafuta kwa tochi.

Wakati hapo nyuma tulikuwa tunaletewa na kulazimishwa kuzisoma zikiwa zimepambwa kwa kila aina ya mapambo.

Inashangaza sana.
Wako busy na uchaguzi nchini Kenya..,

Hili nalo linaitaji ufafanuzi kweli?[emoji848]

Alafu tukiwaambia pro-Russia wengi mna mtindio wa ubongo mnatuona wachokozi
 
Mkuu vunjo na kp kipanya44 moto mnaowatembezea pro russia sio wa kawaida. Habari almost zote unazoleta nazipata kwenye source za ukraine.
Warusi naona wanashupaza shingo tu humu na vihabari vya kuokoteza visivyo na hata source.

Hii battle tutaona mwisho wake mfupa umeshakuwa mgumu kwa fisi.
Hakika, wengine wameshaanza kusalimu amri tayari,Kuna mmoja alikuwa anajiita " Jesus mulokozi"' huyu kila siku alikuwa akileta gazeti leefu kweli kweli akielezea mafanikio ya hii wanayoita ""special epereshen "" baada ya kuona super pawer wa mchongo anazidi kudhalilishwa naona kaukimbia Uzi[emoji1787][emoji1787]
 
Tazama hii Donetsk Region Russian ammunition imekwenda na maji kitu kizito kimetua tutaelewana baadae nani anapiga sehemu muhimu kwenye mshono.

Mkuu, hii Thread haitaki video za uongo za Youtube. Hizi ka post kule kwenye uzi wenu wa mapambio.
Hii lete video zenye source kama The Sun, Reuters, nk. Una boa na video za uongo.
 
Mkuu, hii Thread haitaki video za uongo za Youtube. Hizi ka post kule kwenye uzi wenu wa mapambio.
Hii lete video zenye source kama The Sun, Reuters, nk. Una boa na video za uongo.
Huyu jamaa ana argument za kitoto Sana,ni vyema kama mtu anajiheshimu akampuuza wala usijibishane nae,kwa sababu hajengi Hona zenye mashiko zaidi ya kubidhana kama kule Facebook.
 
Urusi katumia kila kitu, patia picha US wangetuma tomahawk missiles je
Au akituma f22 apo si ndo ingesambalatisha, ingetumwa apo Tomhawk si ndo ingekuwa noma
Hizo Tomhawk zilizoshindwa Syria [emoji16][emoji16][emoji16]

Kuna watu wameingia humu na hawatumii akili kubwa kwenye kujenga, kutetea na kuibua hoja hivyo nendeni nao kwa uelewa wao na mbinu zao wanashambulia bila kutumia akili.

Nadhani hawa ni alien waliovamia jamii forum.

N.B Kuna zoezi la stories of change ambalo JF wanatumia kujitangaza na kuongeza member.
Hivyo Facebook, Instagram na TikTok wameingia humu.
 
Urusi katumia kila kitu, patia picha US wangetuma tomahawk missiles je
Au akituma f22 apo si ndo ingesambalatisha, ingetumwa apo Blackhawk si ndo ingekuwa noma
Black hawk unaijua lakini Ni helicopter ya kizamani kabisa naona unaiongelea Hapa Kama silaha ya upekee Sana.
Hiyo ndio moja ya zile zilidondondoshwa Mogadishu .

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Katikati ya vita aljaeezira Bbc Dw na mashirika mengine yalikuwa yanasifu na mapambio kuwa Russia anashambuliwa na amekata moto. Baadae waliacha kabisa kutoa habari.

Naona ule upepo tena umerudi kwa kasi ya 5G.

Sasa hivi wanachoma maghala ya silaha za Russia. Hawataki kusonga mbele wala kukomboa maeneo na miji iliyotekwa..

Baada ya muda hatutawasikiza ziadi ya kusema Putin ni dikteta

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Duh. , Masikini Putin [emoji848].., jamaa kapoteza dira ya vita, hajui atamaliza vita kivipi, anachofanya ni kuendelea kupigana kiume Ili kuficha aibu anayopata lakini kihualisia jamaa ana uchungu sana moyoni kwa kuingizwa mkenge na washauri vilaza [emoji848]
Vita imeshaenda kombo hii na haina dalili ya kumalizika.
dudus Yoda MK254
 
Back
Top Bottom