Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Humjui Putin,alikuwa anasubiri winter,aminye Nord stream 1,halafu awaambie kama mnataka gas,ni ninyi wenyewe kuchagua!
Na hapo Bado Wana vi akiba,subiri mzigo uanze kukata!Wataonza kupigana vikumbo,nani amsikilize Marekani wakati Kwake hali mbaya!Wakikaa vibaya maandamano!
Kama Italy ndio hawataki kabisa serikali Yao kujihusisha na sanctions dhidi ya Russia ila serikali imekomaa,winter ikikaza wanaingia Barabarani!
Winter hii inaenda kuangauka na serikali kadhaa huko Ulaya!
 
Ndio ile demu unamnunulia gari alafu jamaa kamwekea mafuta ya ten anamwona yeye ndiye wa maana.Mimi bwana nimefanya kweye mashirika ya misaada meng huwez kuta taifa la kidictetor likitoa misaada kwa nchi maskin,watasaidiana wenyewe kwa wenyewe ,kama unabisha lete shirika la msaada lolote unalolijua linatoka Russia au China. Japan kuna JICA,US kuna USAid,UK UK aid,Demak kuna DANIDA,bado kuna France ,Australia, Norway, South Korea,Germany, Canada, nchi zote hizi zikekua mstari wa mbele kutupiga tafu kiuchumi ,kiukweli kama hujashirik kuchakata bajet ya tz hutaelewa haya mambo sisi bado choka mbaya wenzetu bajet zao zinacheza na surplus kila mwaka ila sisi full deficit kila mwaka tangu. tupate Uhuru .chance za kimaisha ni chache sana tunaogelea kwenye umaskini yan tunanuka shida,ukisaidiwa use na angalau shukran
 
Putin anachokifanya ni kujaribu kutengeneza propaganda ya uhusiano wa kidunia ,lengo ni kuua dhana kwamba yeye alichokifanya Ukraine hakijamuharibia mahusiano ya kimataifa,kwamba bado ana marafik,ila ukweli unabak palepale sasa hivi Russia anakwepwa sana na mataifa mengi,even in Africa, Putin siyo mtu mzur China anamjua sana Putin ila wameunganishwa na kamba ambayo hakuna asiyejua ,tukisema biashara ni uongo
 
Kwani kabla ya Gas ya Urus huko Ulaya walipitaje hicho kipindi cha winter?!

Shida ya serikali za Ulaya ni kwamba,sio kwamba kila kiongozi anayekuja anakuja na mambo yake kama huku kwetu, wenzetu wanafuata Sera za nchi tena hao wanaotoka wanaweza kua afadhali kuliko watakaowapokea kijiti. Mfano mzuri ni hapo Uingereza katoka Boris kaingia Yule Mama lakini Sera zake dhidi ya mataifa hasimu ni zilezile hazijabadilika.
 
Kingine kinachonishangaza ni kwanini atake Nord stream 2 ifunguliwe wakati alishasema kapata soko la Gas huko Asia Ulaya hana habari napo tena.
 
Kingine kinachonishangaza ni kwanini atake Nord stream 2 ifunguliwe wakati alishasema kapata soko la Gas huko Asia Ulaya hana habari napo tena.
Hizo pipeline kukamilika kwenda huko China,India, Pakistan NK sio Leo,Kama ambavyo EU kupata mbadala wa gas ya Urusi sio Leo!
Nord stream 2 imekula Hela,so walau lazima irudishe gharama za instalment winter hii!
watu walitabiri,Ile kupunguza volume kwe pipelines zake ni kuhakikisha hakuna nchi inaweka reserve badala yake Gase yote anayopump inatumika!
Huu Sasa ni wakati wa Putin kushika usukani!Silaha hii ya gas sio poa kabisa!
 
Kuna nchi zilikuwa na Nyuklia power plant,baadae zikafunga!Kama France,ikazifunga!Kuzifungua ni shughuli ya miaka!
Au unataka turudi zama za nyuma zaidi za Kuni?
Yaani mfano Pale Roma,watu waanze kupambana kutafuta Kuni!!!Halafu pia Kwa Sasa tech ipo juu,mambo mengi ni gas!Na inapokosena hasa winter hii basi gharama ndio zinaenda ku sky rocket!
 
Kaka gharama zilizotumika kujenga hilo bomba haziwezi rudishwa kwa miezi michache ya winter.

Nchi za Ulaya zilishatabiri kitambo (kama unakumbuka) kwamba wana taarifa za intelligensia kwamba Urusi itasitisha uuzaji wa Gas ifikapo winter,na imekua kweli ndio maana wakaanza kupunguza matumizi ili kusave gas kwa ajili ya Winter na Kwa hilo wamefanikiwa Jana Mkuu wa Umoja wa Ulaya Bi Ursula alisema gas reserves zao zimejaa kufikia 85% na utegemezi wa Gas ya Russia umefikia 9% toka 40% iliyokua awali kabla ya Vita.

Ujerumani na nchi nyinginezo za EU ameanza kununua coal Kwa wingi kufidia gas ya Russia wakati wa winter plus kuna vinu vya nyuklia ambazo vilipaswa kustaafishwa vimeongezewa muda kufidia nishati iliyokua inatoka Urusi.

Yote kwa yote muda ndo hakimu mzuri,ngoja tusubiri winter haipo mbali tutaona matokeo.
 
Hivyo vinu vinaweza kufufuliwa Mkuu kama vilikua havijabomolewa. Hata Elon musk aliwashauri EU warudishe vinu vya nyuklia waachane na mambo Yao ya net-zero Kwa sasa

Elon Musk has called for a boost in Europe's nuclear-energy output amid fears of a gas shortage on the back of Russia's invasion of Ukraine.

Musk tweeted on Sunday evening that it's "extremely obvious" that Europe should restart dormant nuclear power plants and boost the output of those that are operational.

"This is critical to national and international security," wrote the CEO of Tesla. Tesla runs a clean energy business alongside its electric vehicle unit.

Elon Musk says Europe should restart its dormant nuclear power stations amid fears the Russian invasion of Ukraine will trigger a gas-supply shortage
 
Ulitaka kujua Kuna jambo, Zelensky alimuomba huyo mama wa EU sanctions zaidi Kwa Urusi kipindi hiki!Bi Ursula akaishia kumuahidi fedha zaidi Zelensky ila suala la sanctions akaliacha kabisa!
EU wanajaribu kucheza na akili Putin Ila uhalisia utaonekana soon!
 
Vikwazo gani tena Mkuu (maana EU mpk sasa wana package 6 za vikwazo dhidi ya Russia) kama Una link iweke nipitie
 
Washirika wa Putin hawaelewi somo
 

Attachments

  • Screenshot_2022-09-17-06-45-41-883_com.google.android.youtube.jpg
    610.6 KB · Views: 19
Mkuu Vinu hivyo vimekaa muda mrefu,sio kama generator ya kufanyika service mwezi mmoja tayari inakuwa hewani!Lazima vipitie series of tests maana hiyo ni nuclear!Lazima wacheki leakage na kama vimeshalika na kutu Ili visilete disaster!Bado kuanza kuzalisha control rods!
Zoezi hilo linachukua muda!Lakini pia hata ikiwezekana ni gharama kuliko gas hivyo inflation juu!Mbebaji wa hizo gharama ni mwananchi!
Tuvute subira tuone!
 
Chukua hii jifunze, ni rahisi sana kuelewa.
 
Kuna kitu kinaitwa constitutional monarchy/ufalme wa katiba ambao unadhibitiwa na katiba huu unaweza kuwa utawala wa kidemokrasia kabisa kama U.K, Denmark na Sweden. Kuna absolute monarchy/ ufalme mtimilifu, huu ni ufalme ambao haudhibitiwi na katiba na mfalme anaweza kuamua jambo lolote bila kufungwa na katiba hizi ni falme za Saudi Arabia, Oman, Swaziland, Abu dhabi.

Hii ni CIVICS ya O-level, bahati mbaya wengine mnaonekana hamkuweza kubahatika kuipata elimu nyepesi kama hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…