Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Huyu ni nani? Sasa zimetoka wapi hizo drones? Kwenye dunia yako ni kwamba hakuna drones za Iran zipo Russia. Baki kwenye dunia hiyohiyo, haiwezekani leo useme hiki, kesho kile. Unakuwa kama benderaView attachment 2367368
Haaa mkuu huwa mnanichekesha na huyu jamaa yako.
Katika sekta ambazo Urusi anazipuuza ni sekta ya drone yaani jamaa hawana muda nazo sijui kwanini ila naamini baada ya hii vita hawatarudia kuipuuza hii sekta na tutegemee uwekezaji mkubwa kwenye hiyo sekta.

Ila tuambizane ukweli mkuu uliziponda sana drone za Iran ila sasa hivi zipo zina wahenyesha kwenye uwanja wa vita.

Leo hasubuhi zimefanya uharibufu mkubwa sana kwenye mji wa Odessa.

Na ndizo zimevi kwamisha vikosi vya Ukraine kulidhibiti jiji la liyminal kwenye mkoa wa karkiv.

Juzi wizara ya ulinzi ya Urusi ilichapisha video ya drone za Iran zikiharibu msafara wa vifaru na mizinga vya Ukraine huko kherson, na jana hiyo hiyo rais wa Ukraine akatangaza kupunguza uhusiano wa kidpromasia na Iran.
Ila sasa hivi nasikia Ukraine imeagiza mfumo wa ulinzi wenye uwezo mkubwa wa kuharibu drone kutoka Israel ngoja tuone ufanishi wake.
 
Tunataka source ya madai yako kwamba Baykar hawajatengeneza drones 100 za tb2 mpaka sasa hv!? Au ulitunga!? [emoji16]

Hiyo source yako kuhusu russia kudungua zaidi ya drones 100 za uturuki ni kichekesho kingine.

Acha blah blah!
 
Nimezitaja nchi zinazoitambua crimea kua ni sehemu ya urusi. Wewe unakuja na habari za ukr-Russia conflict, sorry bro are you nuts!? Wapi mm nimetaja russoukro conflict hapo!?.

Lakini Wewe kwa mihemko ushazoeleka.
 
Msimamo wangu ni huu mpaka sasa. Mnasema niliziponda na sioni mkionyesha, au nyie mnaelewaje yani.

Russia itakuwa ni kilaza zaidi kwenye drones kama hizi cheap Iranian suicide drones zinaonekana game changer kupitiliza. Drones hata wale Houthi pale Yemen wanazo na mwezi huu kwenye military parade yao kubwa zilikuwepo nyingi tu. Iran simuweki kwenye top 4 ya mabingwa wa drones
 
Wewe na Mathanzua mnawapenda sana "former" na "ex" so so wa West ambao sasa hivi ni laughing stocks tu na hakuna anayewatilia maanani.
 
Nimezitaja nchi zinazoitambua crimea kua ni sehemu ya urusi. Wewe unakuja na habari za ukr-Russia conflict, sorry bro are you nuts!? Wapi mm nimetaja russoukro conflict hapo!?.

Lakini Wewe kwa mihemko ushazoeleka.
Tuletee source ya Zimbabwe na Burundi kutambua Crimea kama sehemu ya Urusi,na sio propaganda uchwara.

Halafu angalia unavyojiuma Una,kwahiyo Crimea haipo kwenye ukr-Russia conflict?!
 
Urusi wasifie kwenye vodka nzuri kwenye movies hata Pro Russia wenzako watakuona kituko ukijaribu kuwalinganisha na Hollywood au hata Nollywood ya Nigeria.
 
Mbolea kwa ulimaji wa Alizeti, mavuno yatakuwa mengi msimu ujao
 
Yesterday, the Ukrainian General Staff claimed troops shot down two Russian Su-30SM Flankers, a Su-25SM Frogfoot, a Su-34 Fullback, five drones, and a cruise missile.

Footage showed a Su-34 trailing fire from its right engine over the frontline in Kharkiv Oblast, with a later clip showing a fireball and crash site in the area.

Tena hizo ndege nyingine zimepigwa na Stinger MANPADS
 
Mwenzako vunjo analetega hapa habari ambazo kwa siku ya jana tu Russians wamepoteza ndege zaidi ya 20.

Sasa tukuamini wewe au tumuamini huyo vunjo
 
Uliyo yasema yana ukweli fulani ila ukuaji wa teknolojia ya kijeshi wa Iran si haba na si wakubeza kabisa.
Ndani ya miaka 10 ijayo watakuwa si haba.
 
Mimi kama proRussia napinga hii taarifa,si tulikubaliana Ndege za Russia zimefungwa mifumo ya Umeme (Khibiny EWS) ya kuzima mpaka Meli (USS Donald Cook) sasa inakuaje zinashindwa kuzima mifumo ya vikombora vya zamani kama Stingers?!
 
Wananchi wake wenyewe wanakimbia hakuna mtu timamu ataenda kushiriki vita isiyo muhusu.
Ulimwenguni watu wanatembea wanakua mercenaries.

Watanzania ndo tumujifungua humu ndani kama tupo kwenye kibuyu....watu wanazaliwa mkoani..wanatembea humuhumu mpaka wanazeeka

Nchi nyingine watu wanatake risk sana....wachezaji wangapi mfano WaTz wanacheza nje??,Wangapi WaTz wanafanya kazi/biashara nje??
Mwezi wa tatu..waethiopia walijaa ubalozi wa Urusi wakitaka wakaajiliwe kama wapiganaji, Waarabu etc....Wagner wale full mchanfanyiko kule..

Ulimwengu hauko kama wewe unavyotamani uwe....na haijalishi kwamba uko sahihi au hapana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…