Lini USA alimwambia Ukraine kwamba watairudisha Ukraine?!
Hizo nchi jirani na Russia haziwezi kuona Sawa ufedhuli anaufanya Urusi sababu wanajua na wao kitawapata kilichompata Ukraine Kwa kisingizio kilekile kwamba Urusi anaenda kulinda raia wanaoiunga mkono Urusi kwenye ardhi ya hizo nchi. Resources sio kigezo cha kufanya eti nchi ikijisogeze Kwa Russia,Russia ni Taifa kubwa lakini kwasasa halina ushawishi hata Kwa jirani zake kuizidi China ambayo haina resources kuizidi Urusi mfano mzuri ni Kazakhstan hivi sasa inajitoa kwenye kivuli cha Urusi na kuegemea Kwa Marekani & Europe na China. Wanajenga bomba jipya la mafuta ambalo litakwepa kupita kwenye ardhi ya Urusi na Rais wao alimwambia Putin live kwamba hawatatambua Donbass wala Luhansk matokeo wanasiasa wa Urusi wakaanza kusema Kazakhstan sio Taifa linatakiwa liungwe Kwa Urusi Yani sababu zilezile zilizotumika kuivamia Ukraine ndo wakaanza kuzisema sema dhidi ya Kazakhstan kisa tu haifuati matakwa ya Moscow. Russia ni Taifa kubwa lenye resources nyingi lakini wananchi wake hawali matunda ya hizo resources Ila Putin na Cycle yake ya maoligarchs,sasa hivi baada ya Mali zao kushikwa Putin anawaua kila kukicha sababu anajua siku watamgeuka.
Shekhe unazungumzia Ulaya ipi?! Juzi UK imesema itaongeza bajeti ya kusaidia silaha Ukraine kufikia $2.3 bilioni, Ursula kiongozi wa European Union alisema Kuna ela zimetengwa na zitaongezwa ili kununua silaha Kwa ajili ya Ukraine. Putin alidhani akiwablack mail Kwa kukata gas watampigia magoti matokeo yake imekua tofauti,Ulaya wanatafuta alternative za Gas ya Urusi,Qatar na Ujerumani wapo mbioni kukamilisha mkataba mkubwa wa kuuziana LNG. Alternative energy sources km Hydrogen zimeanza kuangalia Kwa jicho la tatu, Ujerumani imefungua tena coal plants,kuna vinu vya nyuklia ilitakiwa vistaafishwe wameamua kuviongezea muda ili kuziba gap lilioachwa na gas ambayo Putin amekata. Putin hakupiga hesabu vizuri kuingia kwenye vita ya kijinga kama hii maana kwenye kila kitu amepata matokeo tofauti,alikua anataka kudhibiti upanuzi wa Nato- matokeo yake NATO itapanuka zaidi Finland na Sweden soon watakua wanachama. Alitaka kuua cooperation Kati ya USA na Europe kupitia Nord stream 2 matokeo yake imefungwa,Putin mwenyewe juzijuzi hapa anakuja na demand eti Ulaya wakitaka gas bhas wafungue Nord Stream 2