Sasa si ndo vizuri ili Ukraine washinde au mnataka nini tena.Naamini una uwezo wa kusoma mwenyewe habari. Sijui kama unataka kusikia habari halisi. Ni shauri lako. Siwezi kufurahia kama nchi kama Urusi inatuma watu wake wafe - na wasioandaliwa watakufa wengi.
Habari za Warusi eti wanatumwa bila maandalizi ni nyingi. Orodha zinazorushwa na askari wapya wakiambiwa wanunue hii na hii ni nyingi. Video ziko ambamo unaweza kuona jinsi wanaambiwa wanunue wenyewe nguo za baridi (inayoanza sasa polepole), sleeping bag na mengine ...
Hivyo ndivyo jinsi ilivyo wakati wa vita...
Umefanya Vizury kurejea humu mkuu, bila kusahau hii hoja yako yenye mashiko.Nimerudi tena wakuu baada ya majukumu kunitenganisha na JF kwa muda kidogo, Mijadala Mingi imenipita ila nimepata ABC mlipo kwasasa baada ya kutumia Skimming methodology kupitia Michango yenu.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO.
Mwanzoni kabisa mwa operation hii niliwahi kusema kati ya malengo ambayo russia itahakikisha yanatimia kwa njia yeyote ile, Moja nikulichukua eneo la Ukraine mashariki ( DRP na LRP) hizo kharison na Zaporizhzhia nikama bonus tu ilizo amua kujipatia Urusi baada ya zelensky kukaza fuvu na akiendelea kukaza fuvu atajikuta Kharkiv na Odesa nazo zinachukuliwa na Urusi. lengo la pili ni Ukraine kutojiunga NATO.
Kuhusu Ukraine kushambulia hayo majimbo yaliyo jitenga.
Russia ikishakamilisha taratibu zake za kuyaongeza hayo majimbo kwenye mipaka rasmi ya russia basi Ukraine itaishia kubweka tu na haitaweza kushambulia tena kama ifanyavyo sasa, Cremia ni mfano hai juu ya hili.
UJENZI NA UKARABATI WA MIJI YA MAJIMBO MAPYA UKIANZA:
Russia ikianza ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya hayo majimbo yakiwa kama sehemu ya Urusi, basi Ukraine haitakuwa na jeuri tena ya kushambulia majimbo ya russia kama ilivyo fyata mkia kuishambulia cremia (2014) na Mariupo (hivi karibuni) ambapo russia inaendelea na ujenzi pamoja na ukarabati wa miundo mbinu bila Ukraine kurusha hata jiwe kwenda Mariupo.
KWANINI?
Kwasababu: Ukraine anajua kabisa akishambulia hayo majimbo baada ya russia kuweka utawala wake rasmi pale, russia itapata sababu ya kuanzisha vita kamili kwa sababu ya kuvamiwa mipaka yake na hapo ndo Amri jeshi mkuu wa Urusi atatangaza vita rasmi dhidi ya Ukraine ambayo haitajali sehemu ya kupiga wala nani wa kupigwa na mwisho wa siku Ukraine inaweza ikabaki historia tu au "land locked County"
Mwisho: Russia anaijua vyema weakness ya bara la ulaya ipo kwenye msimu wa baridi, na katika kipindi anachokisubri kwa hamu basi ni hicho kipindi cha baridi. Katika hicho kipindi Ukraine akijaribu tu hata kurusha risasi moja ndani ya mipaka ya Russia (yakiwemo majimbo mapya) basi atatembezewa kipigo cha mbwa mwitu huku akiwa hana umeme wala ges kwajili ya kupasha joto raia wasigande. IKUMBUKWE kwasasa Ukraine ananunua baadhi ya power energy kwa Urusi baada ya Urusi kuchukua uthibiti wa eneo la Zaporizhzhia kilipo kinu kikubwa cha nuclear power nchini Ukraine na chapili kwa bara zima la ulaya. Na ikumbukwe kipindi cha baridi ulaya kila nchi itapambana na hali yake kuokoa raia wake na uchumi wake hivo tegemea makelele ya westerners kuja kupotea hapo baadae.
Pia niwakumbushe tu kupotea kwangu kwa muda hakujabadili Msimamo wangu wa kusimama na Russia katika hili kwajili ya afya ya dunia dhidi ya muovu USA na mashoga zake wa west.
Mungu aibariki Urusi [emoji635][emoji635] [emoji635] katika kutimiza malengo yake.
Nawasilisha[emoji120]
Kilanja wa dunia kashatoa msimamo wake kwa jeshi la Ukraine kwamba hayo maeneo yote yalikofanyika mazingaobwe uchwara yanayoitwa referendum ni target Halali kwa majeshi ya UkraineNgoja tuone kuanzia kesho hali itakuwaje
Gift kwa jinsi unavyotetea hoja zako..ni kama hujui kabisa ulimwengu huu unavokwenda, unatumia hisia zaidi....na ndo maana wadau kibao wamekushauri kidogo uende ukasomesoke kidogo mambo ya Geopolitics, utawala n.k..Sorry but
Umeamua mwenyewe kuwa mpumbavu so inabidi nikuite tu
Hivi unanzaje kuamulia nchi huru nchi za kushirikianazo
Ni sawa na Kenya itumamulie tusijiunge sadec kwa sababu ni tuko EAC, na ulivyo mpambavu ungekubali
Au enzi za Vita baridi pamoja na uchanga na umaskini wa nchi yetu mwalimu alikataa kupangiwa marafiki, lakini kwa akili zako hizi za ajabu ungekubali kupelekeshwa
Ww Kama ni baba naionea huruma familia yako, inaonyesha uko tayari kuachia familia kwa jirani yako tu kisa ni tajiri au Anna nguvu hata mke unaweza kunyanganywa we on
Tatizo unaonyesha una uwezo mkubwa wa kukariri mambo bila kuyaelewa na ndo maana unashindwa kujua mambo kwenye uhalisiaNasikitika kukuambia kua una uwezo mdogo sana juu ya haya mambo.
'It is Russia’s historical tradition and destiny to stop those seeking world domination'We are with you 🇷🇺
From Putin’s mobilization speech: Western elites have gone too far. It is Russia’s historical tradition and destiny to stop those seeking world domination.
European wanamtegemea sana kwa mengi mbona waliomba kwa kunyenyekea aachie Meli za ngano?We waache Tu wanawachukulia warusi poa
We jamaa akili yako nilivyo iacha na nilivyo ikuta haijakomaa japo hata kwa 1%!Walioyabutua mabomba ya ges ya NS1&2 wanastaili tuzo maalum.., ngoja tuone super pawer wa mchongo ataendelea kumlingishia nani hiyo ges yake[emoji16][emoji16][emoji16]
Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Viazi Ulaya hua Ni kwa ajili ya malisho ya mifugo gani mkuu?European wanamtegemea sana kwa mengi mbona waliomba kwa kunyenyekea aachie Meli za ngano?
Akifunga pipeline tumeisha
Huku mpaka chakula tunategemea nchi za nje hata Africa siku wakisema hatutumi kitu ulaya mtaona watakavyo konda
Maana huku wanalima viazi ulaya na Mahindi kwa ajili ya malisho na maua kwa ajili ya mafuta ya kupikia na sana zabibu kwa ajili ya wine
Sasa hapa tutakula zabibu na viazi tu na huko Putin anatishia maisha sio kutishia tu ni MBABE