Naomba nikuulize swali dogo tu...kwa uelewa wako unadhani Putin anaweza kutoa agizo la mashambulizi ya nyuklia Marekani wasijue? Kweli unaamini Marekani na nchi za Ulaya Putin anaweza kuwashtukiza tu kwa mashambulizi ya nyuklia.Wewe Mag3 njoo na hoja ya maana. Hapa tupo kwenye social media, wewe hunijui nami sikujui. Cha msingi leta hoja. Weak people hujadili watu binafsi.
Ona sasa umeanza kunijadili mimi badala ya kujadili hoja.
Leta hoja.
Nataka Ulete hoja kuhusu Russia Federation na SMO. Mengine unayoyaongea ni upumbavu wako tu.
Kwa ufahamisho wako wewe na wajinga wenzio wanaomeza matango pori unayoyarusha humu, kila azimio linalofikiwa na Putin tayari linajulikana kwa Marekani na NATO. Russia haiko kwenye level hiyo unayoifikiria na mnajifurahisha tu.
Vipofu mnaongozana na kwa hilo hakuna cha ajabu...hamjui kuwa hamjui! Marekani inao watu hadi ndani ya serikali ya Putin na ukweli huo hata yeye Putin anaujua na ndio maana kazidisha propaganda za kujihami kwa kuwatumia hadi viongozi wa dini.
Nchini Russia hakuna uhuru wa kidini, je unajua sababu zake?