Hebu hii iweke vzr kiongozi ili wewe ni kuelewe, yaani unamaanisha kitufe hicho kiko monitored au contrlled na west au USA?. Ukiniambia kombola na nuke likiruka lunakuwa detectable naelewa, lkn kabla hajabonyeza wanajua, jamani hata kama 1962 ulikuwepo hii sasa chai mno.
Siko kubishana siwapendi West na washirika wake lkn pia sifaidiki kitu toka Far East, ninachojua Afrika inabidi itoke kwenye pandora box ambapo wanaamini hawawezi pasipo white colour skin. Bora tuanze at sq 1
Mkuu, crisis ya Cuba wala kiukweli haikuwa hivyo - Kennedy alichokuwa akifanya ni mambo ya kisiasa kujaribu kukuza kura za maoni nchini mwake na kutaka kuonyesha yeye ni mwamba wa Dunia,for domestic consumption of course - lakini nyuma ya pazia mambo yalikuwa tofauti kabisa, vyombo vya habari vya magharibi hasa Merikani huwa haitaki kusema ukweli kwamba Urusi ililazimika kupeleka missiles za nuclear nchini Cuba baada ya kuionya Merikani mara kadhaa kwamba iondoe missiles zake zinazo lilenga Ťaifa la Urusi zikitokea huko Uturuki na Italy ambako Wamerikani walikuwa wamezitegeshea kuja kuishambulia Urusi hapa baadae.
Urusi ikaona hisiwe tabu na wao wakasafirisha missiles kwa meli au ndege kwenda kisiwani Cuba sikumbiki vizuri, baada ya ndege za upelelezi za Amerika kugundua kwamba missiles za Urusi zimekwisha ingizwa Cuba na kujengewa silos na launchers platform, basi, Kennedy na washauri wake wa kijeshi wakijifanya kuja juu-wakarusha ndege zao za kipelelezi kwenda Cuba kwa wakati tofauti ndege zote zikatunguliwa na marubani wake kupoteza maisha, Amerika haikuwai kutangaza kutunguliwa kwa ndege zake aina ya U-2 na wala Merikani hakufanya lolote kuhusu kutunguliwa kwa ndege zake za kipelelezi-walikaa kimya kabisa!!
Mwishowe Krustchve alimwandika telegram Kennedy kwamba Urusi haitatoa missiles zake Cuba mpaka Amerika itakapo ondoa missiles zake huko Uturuki na Italy zinazo lenga Taifa la Urusi - Kennedy ali-comply matakwa ya Kiongozi wa Urusi akaondoa missiles za Merikani huko Italy na Uturuki, mgogoro ukaisha lakini nyuma ya pazia ili kulinda masuala ya siasa ndani Merikani, Kennedy hakutala aonekane weak mbele ya wapiga kura.
NB:Niliwahi kusoma telegram Krushchev aliyo mwandikia Kennedy kwamba:-
Kwanza: Aondoe missiles nchini Italy na Turkey.
Pili: Merikani isitishe kutishia Cuba na maisha ya Fidel Catro.
Tuta: Merikani hisiwe inatishia ushirika wa Warsaw pact.
Nne: Merikani hisiwe inatishia marafiki wa Soviet Union.
Mengine sijui ni kipi kilitekelezwa lakini missiles za Merikani ziliondolewa huko Utaly na Uturuki, vile vile vitisho kwa Castro vilikoma.
Bottom line is: Missiles za Urusi ziliondolewa Cuba Russia ilipo hakikisha kwamba missiles za Kimerikani huko Italy na Turkey zimeondolewa - tofauti kabisa na habari zinazo tolewa na media za magharibi kwamba Warusi walinywea - hiyo si kweli hata kidogo ni uongo ulio pitiliza mipaka wenye lengo la kujitutumua tu.