Ila Marekani inanistaajabisha sana!
Licha ya kuwa wanajitahidi kwenye teknolojia ya kijeshi (zana) lakini wanajeshi wake hawana ukomavu kabisa!
Vita vya Iraq walikuwa wanalia sana na machozi yanawatoka mapambano ya ardhini yakipamba moto. Wanajeshi wa UK ndiyo walikuwa wakipambana wakimsaidia mpaka wanapata msaada wa anga.
----------------
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa kila Russia wanavyobadilisha makamanda wa operation kuna phase mpya wanaingia.
Kuhusu Urusi kubadili makamanda kila phase nakubaliana na wewe na huwa ina upgrade makamanda kulingana na moto wao hata syria ilikuwa inaendesha operation yake kwa mtindo huo na aliekuja kupewa phase ya kutembeza kichapo cha mbwa mwitu ni huyu Gen.Sergei Surovikin A.k.A The hero of Russian federation.
Hebu ngoja nimuelezee kidogo huyu shujaa wa Operation za kijeshi na moto wake.
Majina yake ni Gen.Sergei Vladimirovich Surovikin, huyu ni mwamba wa vita vya ardhini na angani, huwa hakopeshi wala kulemba anapokuwa kwenye operation ya kijeshi au vita. Siyo USA, Ukraine wala NATO wasio jua mziki wa huyu Mwamba. Hii siyo kwa mjibu wangu bali nikwa mjibu wa waliowahi kukutana na moto wa huyu General kwenye uwanja wa Vita kama vile Ukraine na USA-Syria (ndo maana unaona wamepanic baada ya jamaa kuteuliwa) pitia hii nukuu kuhusu mziki wa huyu mbabe;
☆Amy commander Surovinkin led the Russian forces that intervened in Syria starting in 2015, and American commanders sometimes consulted directly with him there to avoid clashes☆ Syria War news
Huko syria baada ya kukabidhiwa ukamanda wa vikosi vyote vya operation (2017) alitembeza moto hadi makamanda wa USA wakawa wanaenda kwake kuomba poo ili ashushe moto wake(rejea nukuu hapo juu) lakini mwamba aliendeleza kichapo kilichopelekea ushindi ndani ya miezi mitatu tu. Hadi leo serikali ya Assad haiwezi kumsahau huyu Mwamba alivyo isaidia dhidi ya wahuni wa IS na USA.
TURUDI KUONA MOTO WAKE PALE UKRAINE.
●Kama mnakumbuka mwezi june Putin alimuondoa kwenye uwanja wa vita Gen.Alexander Dvornikov baada ya kutolidhishwa na kasi yake ya moto. Guess whom replaced him[emoji3], He was a great General and the hero of Russian federation Gen. Sergei Vladimirovich Surovikin. baada ya Mwamba kuchukua kijiti nazan wote ni mashahidi moto uliotembezwa Donbas kutokea kusini mwa Ukraine kuanzia june mpaka August ambapo ndo miezi Ukraine ilianza kupoteza maeneo yake kila siku na kukimbia hovyo huko Donbas kwasababu ya Moto wa Gen.Surovikin.
Baada ya kumaliza kazi yake alirudishwa kusini mwa Ukraine (kherson) kwenda kuwa commander in chief wa vikosi vya Russia vilivyo kusini mwa Ukraine. Kama mnakumbuka wale askari zaidi 800 wa Ukraine waliokufa siku moja wakijaribu kufanya counter offensive kherson basi alie wapa hiyo dozi alikuwa si mwingine bali huyu huyu Mwamba General. Surovikin.
Gen.Sergei Vladimirovich Surovikin Alitembeza moto mpaka majenerali wa Ukraine wakawa wanakubali mziki wake.
Ushahidi:
☆Surovikin knows how to fight with bombers and missiles — that’s what he does☆ Gen. Kyrylo O. Budanov, the head of Ukraine’s military intelligence service, said in June.
☆Russia's Gen Surovikin makes 'headway' in the battle for Donbas☆ The national news - July 7, 2022.
Sasa naona Russia imeona ni muda sahihi wa kumkabidhi mwamba wa operation Vikosi vyote vya operation afanye kazi yake baada ya kumaliza justification za kidiplomasia dhidi ya maeneo mapya ya Russia.
Huyo ndo General Surovikin the hero of Russian federation akihusudiwa na watabe wenzake wa Vita kama kina Gen.Shougu, Gen.Gerasimo, Gen. Kadyrov na n.k[emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635]
Inaendelea post inayofuataa.........