Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nafikiri Iron Dome ni kwa Hamas na kwa mbali Hezbollah, siyo kwa giant kama Russia. Unaweza kutumia Iron Dome, lakini Russia akizigundua anabadili vifaa

Kwanza lazima ujue iron dome inafqnyaje kazi. Tech details, range, interceptions capability, israel walitengeneza ule mfumo kwa ajili yao… una fit mahitaji yao.
Unasema russia wanauweza sawa.. je wameujaribu? wamerusha kombora lolote israel?
 
Wamarekani ndio waanzilishi wa Internet na Google unayotafutia vi-propoganda vyako vya Urusi kuwaletea wavivu hapa.
Makampuni makubwa 10 ya IT duniani hakuna la Russia hata moja. Microsoft , Oracle, IBM, Cisco na mengine mengi ni ya US.
Kwani US aliwah nchi ambayo ipo tofauti nayeye iendelee kumzidi? Hilo hawezi kukubali kitokee na kama unabisha angalia issue ya Nord Stream 2 jinsi wakipinga mradi eti kisa Russia itakuwa na uchumi mkubwa itawasumbua huko mbelen na Europe itakuwa inaitegemea Russia!


Nenda China kwenye Issue ya Huawei uliza sababu nini za kuiwekea vikwazo Huawei asipate tender za kufunga 5G Europe! Marekan hataki anataka kampuni zake ndiyo zipewe tender kisa tu China atanufaika kwa kiasi kikubwa na ataanza kuwavumbua.

Itoshe kusema US ni Taifa lenye roho ya usda, ni wabinafsi na wazandiki.
 
We mzungu unaumizwa Sana na ubabe wa Putin Kwa NATO na USA. Kaa ukijua Putin anakwenda kuisambaratisha NATO kibabe sana.
Nimeona wananchi wa France wanaandamana waita Macron ajiuzulu huku wakitaka France ijitoe NATO.

Nakumbuka kipindi fulan Macron aliwah kupendekeza kuwa Europe iachane na NATO, ianzishe jeshi lake lenyewe ila kilanja wao aliwagimea.
 
Screenshot_2022-10-12-06-36-21-89_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
EU yote ni kidemokrasia, kama hao raia hawataki viongozi wao watawaondoa kwa njia ya kura.
Ufaransa uchaguzi umefanyika mwezi May na Macron alishinda kwa 66%.
Rais wa Sri Lanka aliondolewa Kwa kura?Nguvu ya Umma ikiamua,nayo ni demokrasia!Maana Kwa mujibu ya demokrasia ya west ni Kuwa power belongs to the people!
Mfano Leo Russia wananchi waandamane watake Putin aondoke madarakani,hatutaona kauli za hivi!Media zote za west na wafuata nyayo zao kama wewe mtakuwa mkiwapa airtime za kutosha na kusupport jambo Hilo,hamtakumbushia njia za kidemokrasia!
Huo ndio unafiki wa west!
Wakati Iran amezima internet Ili machafuko na maandamano yasitapakae nchi nzima,US wao wakaiondolea vikwazo Iran kwenye internet na kumlipa mkwanja Elon musk awawashie internet wananchi Ili waendelee kuhamasishana na kuleta vurugu nchi isitawalike!
Matokeo yake watu wengi wamekufa na wanaendelea kufa!
Naomba ieleweke siungi mkono sheria Kali za Irani dhidi ya mavazi Kwa wanawake!
Lakini usalama wa nchi ni muhimu!Civil unrest sio jambo la kuchezea,kama umetulia na familia Yako,una kamradi Kako na maisha yameanza kunyooka,unaweza kunielewa zaidi Ninaposema civil unrest can take you back to zeroo!
 
Putin atabaki kwenye vitabu vya historia kama dikteta katili aliyewahi kusababisha maafa na umwagaji damu mkubwa zaidi Ulaya tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.
Oooh Ulaya,na umwagaji mkubwa wa damu duniani baada ya vita ya pili ya Dunia ni nani hao?Hii OP ya Putin haijafika hata 10% ya Afgan,10%ya Libya,10% ya Iraq,10% ya Syria!

Hao viongozi waliosababisha maafa hayo wako kwenye vitabu gani vya historia?Washafikishwa ICC?
Hao wanaojiita wanademokrasia na uhuru wa vyombo vya habari,si ndio wanataka wakamfunge Julian Assange miaka 200 Kwa kutoa Siri za uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu wa majeshi Yao?
It's a shame!
 
Ukiona Lukashenko katangaza vita ujue pressure aliyopewa na Putin ni kubwa mno. Hata hivyo bado ni risk kwa Putin kulazimisha Belarus iingie vitani. Hapo anahatarisha serikali ya Lukashenko iliyoko rehani ambayo Putin mwenyewe ndio anailinda. Kupotea kwa Luka linakuwa pigo kwa Putin. Watafanya calculations zao vizuri ila makosa yapo. Mbona hata kabla ya hii vita intelligence service ya Russia ilimhakikishia Putin kwamba Ukraine ni wanyonge na watajisalimisha kama walivyofanya Crimea
vita ya Russia dhidi ya Ukraine iliisha ndani ya siku tatu baada ya vita kuanza kwa Russia kufanikiwa kulisambaratisha jeshi la ulinzi la Ukraine. Kinachoendelea sasa nchini Ukraine ni vita kati ya Russia na mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani.
 
Hongera sana mkuu1

Yaani hii comment imenitia jazba dhidi ya hawa west,natamani nimkamate biden nimchanechane vipandevipande
Hii comment ni ya upande mmoja, na kama mtoa post amekasirishwa bila unafiki na hoja zake, basi anapaswa kuchukia West, Urusi pamoja na China.
 
Ushoga.
Wazungu walipofika Africa waliukuta ushoga. Waafrika hamjafundishwa ushoga au kufirana na wazung. Wazungu walipofika Buganda mwaka 1884 walimkuta Kabaka Mwanga II tayari ni shoga na sababu mojawapo kubwa ya kufanya mauaji yake kwa mashahidi wamisionari 45 wanaume wa Kikristo ni wao kuwa kinyume na ushoga wake.

Ndoa za mitaala.
Hakuna mzungu aliyewakataza Waafrika kuwa na mke zaidi ya mmoja, wewe ukitaka oa hata wanawakwe 20 uone kama kuna mzungu yoyote atakuja kukugusa au kukupigia kelele, huku ni kujilalamisha kitoto.

Watoto kupata mimba na kurudi shule.
Unalalamika watoto wanaopata mimba kurudi shule wakati nchi imewahi kuwa hadi na elimu ya ngumbaru ya kufundisha wazee wenye mvi darasani kusoma na kuandika ili kufuta ujinga. Mmeshindwa kuwajengea watoto wa maskini mabweni, mmeshindwa kuwapa mabasi yawapeleke shule mmewaacha katika mikono ya bodaboda na makondokta karne ya 21 bado mmeshindwa kupeleka maji ya bomba majumbani na kwa haya na mingine mengi mnasababisha wabakwe na kupewa mimba halafu mnataka kuwafukuza shulen! Hamna akili.
#Arudi shule kusoma

Kupangiwa bei za Mazao
Kama hutaki kupangiwa bei mazao na madini yako pangeni bei wenyewe au msiuze. Halafu Wakenya na Watanzania au Waganda na Rwanda wanaoutibuana, kukorifishana na kununiana mara kadhaa huko mipakani hadi hawataki kuuziana bidhaa zao nao ni wazungu??! Hamna akili
Kwani lazima uchangie maana kuna mda unaandika upupu kama vile umelazimishwa kuandika
 
Umeona jeshi au polisi wa Ufaransa wakizuia au kuua waandamanaji wanaotaka Macroni aondoke kuwa Rais kama ilivyo Iran ambapo waandamanaji wanaotaka Ma-Ayatollah waondoke na wasiwafundishe wanawake jinsi ya kuvaa wanavyoendelea kufa chini ya majeshi tiifu kwa Ayatollah??
Rais wa Sri Lanka aliondolewa Kwa kura?Nguvu ya Umma ikiamua,nayo ni demokrasia!Maana Kwa mujibu ya demokrasia ya west ni Kuwa power belongs to the people!
Mfano Leo Russia wananchi waandamane watake Putin aondoke madarakani,hatutaona kauli za hivi!Media zote za west na wafuata nyayo zao kama wewe mtakuwa mkiwapa airtime za kutosha na kusupport jambo Hilo,hamtakumbushia njia za kidemokrasia!
Huo ndio unafiki wa west!
Wakati Iran amezima internet Ili machafuko na maandamano yasitapakae nchi nzima,US wao wakaiondolea vikwazo Iran kwenye internet na kumlipa mkwanja Elon musk awawashie internet wananchi Ili waendelee kuhamasishana na kuleta vurugu nchi isitawalike!
Matokeo yake watu wengi wamekufa na wanaendelea kufa!
Naomba ieleweke siungi mkono sheria Kali za Irani dhidi ya mavazi Kwa wanawake!
Lakini usalama wa nchi ni muhimu!Civil unrest sio jambo la kuchezea,kama umetulia na familia Yako,una kamradi Kako na maisha yameanza kunyooka,unaweza kunielewa zaidi Ninaposema civil unrest can take you back to zeroo!
 
Back
Top Bottom