Tanzania ilivamiwa na Uganda chini ya utawala wa Idi Amin mwaka 1978. Kagera ilikuwa annexed. Mimi kama mTZ it's natural ku side na Ukraine kwenye vita yake na Russia kwa sababu Ukraine inapitia the same thing TZ ilipitia na Uganda. Watz logical hawawezi kumshangilia Putin.
Amin wa uganda yeye alipokula tu ugali na kushiba basi akaona anaweza akafanya lolote na asitokee yeyote wa kumzuia, kuna mataifa wakamhakikishia support (kama tu UKRAINE alivyohakikishiwa support) basi bwana Amin akaukwaa mtimbwi wa vibwengo [emoji23][emoji23][emoji23].
By the way mie sikua nimezaliwa kipindi hicho,ila nasikiaga tu kua Mwalimu alitamka maneno matatu tu ya kwamba NIA YA KUMPIGA AMINI TUNAYO, SABABU PIA TUNAZO, na kubwa kuliko vyote UWEZO TUNAO.
kilichofuatia hapo ni kama kwa PUTIN tu, Mobilization moja ya kibabe sana na wanaume wakatinga rasmi mzigoni [emoji23][emoji23][emoji23] matokeo yake jamaa aliishi uhamishoni mpaka anarejea kwa MUUMBA
Idi Amin hatofautiani kabisa na USA,EU na NATO yao
Yapo makubaliano yaliwekwa baina ya NATO na iliyokua USSR kipindi kile East German inaunganishwa na West German.
Ya kwamba kwa upande wa Mashariki, mpaka wa NATO hautakiwi kuvuka ulipo mpaka wa East Germany, na USA iliahidi bila kushurutishwa na mtu ya kwamba haingeongezeka hata sentimita moja.
Kilichofuata baada ya hapo USSR ikavunjika mataifa kama Poland, lithuani, estoni,latvia nk yakatangaza uhuru,kwa kiburi kikubwa kabisa USA na EU wakayashawishi mataifa hayo kujiunga na NATO, hawakuridhika wakachokonoa na kule kosovo, wakaona bado wakamjaza upepo na Georgia,wakaona haitoshi wakataka mpaka na UKRAINE nayo waichukue [emoji23][emoji23][emoji23] Na wao wameukwaa mtumbwi wa vibwengo.
Mwamba PUTIN ni kama Nyerere tu, yeye kaanza na Special Military Operation, then partial Mobilization (anaiondolea UKRAINE Jeshi). Hapo anawatamanisha NATO ili waingie kingi , wakijaa tu [emoji2957][emoji2957]. DUNIA ITAANDIKA HISTORIA MPYA.