Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kumbe tatizo sio Ukraine kutaka kujiunga NATO tena, wa-Nazi au ushoga??!
 
Tunachojua ni kwamba kamanda Armageddon amelalamika Jana kwa super pawer wa mchongo ana Hali mbaya..,hayo mengine ni chai, [emoji2][emoji1787]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Na wataisoma number vizuri , we ngoja zile troops zilizokuwa mafunzoni Poland ,UK na US zije wiki chache zijazo waone shughuli ,na kuna mashine mpya zinakuja pia
 
Mkuu.. hivi unajua Spring Ni wakati gani na ni muda gani kuanzia Sasa...?
 
Msivurugwe ndugu zanguni, kuweni watulivu tafadhar, tutafika tu

Kama Ukraine akikubali kushindwa Leo hii,maana yake vita itaishia hapohapo.
Urusi haitaendelea kusonga mbele kijeshi.
Wala haitayaachia maeneo iliyoyashilikilia,na ndio kushindwa kwenyewe kwa Ukraine huko.
Ukraine itabidi ikubali kutojiunga na NATO,ndio kushindwa kwenyewe huko.
Ifahamike kuwa silaha za Ukraine kabla ya OP hii kuanza zote zulishaliwa na Urusi,hizi walizonazo Sasa hivi ni kutoka Kwa NATO.
Ikumbukwe kwamba NATO nao wanapunguza silaha zao kwa kiasi kikubwa mno,nao wanaishiwa silaha.
Kwa maana hiyo NATO wako vitani na Urusi kwa kuwatumia wapiganaji kutoka Ukraine.
Kama Zelensky akishupaza shingo askari wake wengi wataendelea kufa na silaha za NATO zitaendelea kuliwa.
Mwisho wa siku hata NATO wakiamua kuingia vitani na Urusi hawatakua na nguvu kama Ile ambayo wangekua nayo kabla ya kuanza kuiunga mkono Kijeshi Ukraine.
Urusi wanapunguza akiba Yao ya silaha na NATO pia wanapunguza.
Tumeshuhudia Canada,Poland,USA,UK na wengine wakilalamika kua akiba zao zimepungua,zimebaki kwa ajili ya ulinzi wa taifa lao TU.
Kadri wanavyoongeza kuipa silaha Ukraine ndivyo Urusi anavyoongeza ukali wa mashambulizi,toka makambi ya kijeshi Sasa ni miundombinu inayoiwezsha majeshi kupigana.
Huu ni uharibifu utakao ilazimisha Ukraine na NATO kuweka silaha chini na wakubali kuja mezani.

Kuna watu wanasema,silaha anazipewa Ukraine ni mkopo atalipa,lakini Ukraine sio wa kulipa Leo wala kesho,itaichukua Ukraine miaka mingi sana kuanza kulipa madeni hayo.
 
Gaddafi aliuwawa na raia wake na wanajeshi wake mwenyewe walioasi baada ya kuuchoka utawala wake wa kidikteta wa miaka 40, NATO walichofanya ni kukata tu nguvu zake kwa kumzuia asitumie makombora na ndege kuwaua waandamanaji waliokuwa wanataka aondoke madarakani. Mengine yote kama haya unayoleta hapa ni poroja

Lakini hata kama zisingekuwa porojo au conspiracy, mimi siungi mkono, siikubali na wala SITAKI kabisa kuisikia United States of Africa. EAC tu yenyewe inatutoa jasho huku ikiwa imejaa madikteta waliodumu madarakani hadi miaka 40 kuwaza hiyo United States of Africa ni wendawazimu.
 
Ujumbe wa kipumbavu na wa hovyo kutoka ngariba
 
Alietabiri kua Urusi ataziamgusha Serikali nyingi ulaya aliona mbali.
Kama sio Op hii BJ angeendelea kua PM UK
 
Halafu dakika mbili mbele wewe mwenyewe utaanza kuwatia wachangiaji wengine mashoga.
Proputin mko kama mateja wa gundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…