Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Anatetea nchi yake hiyo miundombinu ina thamani gani kuliko nchi nzima na uhuru wake kubebwa na dictetor putin
 
Urusi kuivamia Ukraine tu CIA walijua kabla November mwaka jana haijaisha, uvamizi ukafanyika February 24. Urusi anaivamia Marekani kwa kutumia nini?

Hivi mnajua kwenye peer to peer enemies jeshi vamizi linabidi liwe three times ya jeshi linalolinda kwenye eneo fulani. Hayo maelfu ya wanajeshi wa kufanya assault unayakusanya wapi Marekani isikufanyie preemptive strike. Na una naval vessels za kuvamia Marekani au unafanyaje. Alaska haijaungana kwa ardhi na Russia kuna gap ya kama 4km. A very weak point kufanya shambulizi eneo lile, njia ya uhakika ni kufanya amphibious landing kwingineko ambapo hakuna jeshi la kufanya hivyo, China ndio inaweza jaribu kiasi chake ila kama China haitaki kuivamia Taiwan sembuse Marekani.

Na kama unaitaja Mexico Kasome Zimmerman telegram ya World War 1 kutoka kwa huyo Mjerumani kwenda kwa Rais wa Mexico ujue ni namna gani Mexico haioti hata kuivamia Marekani.

Ili uivamie Marekani unahitaji jeshi la majini kubwa na uwe na amphibious landing capability kubwa mno kuizidi hata Marekani yenyewe. Hakuna kichaa wa kufanya suicide mission hiyo. Watajaribu hit and run ila sio kuweka majeshi, hata supply lines unazipataje au ndio kutoa kafara wanajeshi wako
 
Submarine zinafanya invasion na beach landing? Sasa hilo si ni game tena la Android.

Iran haijawahi chukuliwa poa na mahasimu wake hasa Israel. Nyinyi wa kuja ndio mlikuwa mnaichukulia poa. Israel iko inapambana na silaha za Iran inazijua fika kuliko mlioanza kuziona mwaka huu. Na ina sorties inafanya miaka yote kuharibu supply ya hizo silaha nchi jirani. Kama ingechukuliwa poa basi usingesikia Israel inafanya airstrikes Syria au Saudi Arabia inafanya airstrikes Yemen kwa Houthi
 
Angekuwa analalamika tu na hapambani basi Warusi wangelikuwa Kyiv tayari.

Kyiv,Kyiv - nani kawambieni Putin alikuwa na mpango wa kuikalia/teka jiji la Kyiv au kuteka Ukraine nzima-Putin hajawahi kusema hivyo, watu wanatunga stori zao hasa wakisha soma propaganda za magharibi wanazichukulia kama ni Gospel truth!!

Putin alitangazia Dunia kwamba lengo lake la special operation ni ku-demilitarise jeshi la Ukraine, kuangamiza vikosi vya kijambazi vya ki-neo NAZI (Azov) na kuwalinda wa Ukraine wa kusini mashariki mwa Ukraine wenye asili ya Urusi wanao uuwawa kila siku na utawala wa kikatiri wa Zelensky ambao hauwataki/chukia Waukraine wenye asili ya Urusi mpaka sasa Zelensky alisha wauuwa ethnic Russian in Ukraine zaidi ya 14,000 so far ndio maana mikoa hiyo inataka kujiunga na Taifa la Urusi ili kijihakikishia amani ya kudumu, can you blame Putin kwa kutaka kuwalinda Warusi wenzake??

Licha ya Zelensky kuwauuwa raia 14,000 wenye asili ya Urusi hatujawahi kusikia Serikali ya Merukani au za Ulaya wakilaani/shutumu mauuaji hayo, wako kimya kabisa kazi yao masaa yote ni kumsakama na kujaribu kumtisha tisha Putin na viongozi wenzake kwamba wataburuzwa kwenye mahakama ya kimataifa washitakiwe for war crimes - hawazungumzii chochote kuhusu Bill Clinton, Madellin Albright (for Yugoslavia war crimes) - Bush Sr,Bush Jr (for war crimes in Iraq),wapo kimya kabisa, wanajichukulia kwamba wao wapo above the LAW, mtu unashangazwa na baadhi ya waswahili wanao support watu wa ajabu kama hao, wanarudia rudia propaganda wanazo zisikia/ona kwenye western media inept propaganda specifically CNN,BBC,FoxNews, SkyNews etc.
 
Tunasema Ukraine watashinda hivi vita full stop. Putin atajutia kuanzisha hivi vita. Mnaoshabikia Urusi mnajisumbua tu. Putin ameamua kutoa watu wake kafara kwa kisingizio we are fighting for our mother land.

Motherland unaenda kupigana na bwana mdogo. Bwana mdogo atapewa nguvu na Mungu wa Mbinguni. Soon Putin will go down like other dictators.
 
Na wewe umeamini kabisa.
Kwamva walichimba mahabdaki Kwa mikono bila koleo
 
Ukraine siyo mbali nenda kwenye ubalozi wao ukajitolee uwe mstari wa mbele au utaki kufa ukiitwa shujaaa[emoji1787][emoji1787]
 
Rekebisha diaper hio,imekaa upande.
 
Hao warabu kama wananguvu kwanin wanaruhusu Israel anajimegea maeneo kila siku
 
Daaaaaah Ila comments za humu ukizisoma unabaki hoiiii
Kuna mwamba humu anajinasibu ana data zote za majeshi duniani
Kuanzia idadii ya askari mpaka zana za kivita na ubora wake...
Hahahahahaha yaani mwamba anaijua Korea kaskazini in and out
Hahahahahaha hatariii saaana aiseee
Wabongo mfuniko kwa chaii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…