Kabla majeshi ya Urusi hayajaenda mpakani, Marekani ishatoa angalizo watavamia. Na Urusi ikapinga kama kawaida yake.
Siku tatu kabla ya uvamizi, Uingereza, Marekani na Israel zikaanza kuita watu wake waondoke haraka Ukraine. Sisi madongo kuinama tukawa wabishi. Russia ikakataa kupitia vyombo vya habari vya taifa. Hapa ni 4 days before
View attachment 2397581
Sasa nimuulize yeyote anayedhani Russia anaweza ivamia Marekani. Hivi Urusi iliyojiandaa miezi kuvamia Ukraine ambapo wanavuka ardhi pande tatu tofauti kupitia kwake na Belarus, na bado performance ndio hii, ndio hiyo Urusi ya kuivamia Marekani? Yani ufanye mission ya kubeba mamia ya maelfu ya wanajeshi baharini uende kuivamia Marekani kirahisi hivi?
Kwanza Russian Navy haina means ya kutoa air cover kwa invading force yake, watakuwa na floating coffins baharini.
Jeshi lililoshindwa kuilinda Snake island eneo dogo lisilo hata na 10km square, lililoshindwa kulinda flagship Moskva cruiser moja ya Black Sea fleet ndio hilo hilo tunaambiwa linafanya mission ya kuvamia Marekani.
Jeshi linalolalamikia HIMARS chini ya 20 zilizotolewa kwa nyakati tofauti wakati kuna HIMARS zaidi ya 300 Marekani kwenye peacetime, ukianzisha vita uzalishaji unapanda. Ushindwe kuwa na air cover Ukraine inayoomba ndege inanyimwa, uje uipate kwenye anga la Marekani