Putin alisema atakaye jitokeza adhalani na kuleta majeshi yake wazi wazi kwamba anasaidiana na majeshi ya Zelensky kupigana na Urusi - mpaka sasa hakuna Taifa lolote limejitangaza kwamba limengia vitani kusaidiana na jeshi la Zelensky ili kupigana vita na Urusi - hakuna.
Sana sana majeshi ya NATO/US wanajificha nyuma ya pazia ya jeshi la Ukraine, wanavaa uniform za jeshi la Ukraine na kwenda front line - wameuwawa wengi lakini Serikali zao wako kimya kabisa.
Sasa mlitaka Putin afanye nini akurupuke tu na kushambulia mataifa ambayo hayajajitokeza wazi wazi kwamba yanataka kupigana na jeshi la Urusi - hizi dhana zilizo jengeka humu kwamba eti sijui jeshi la Urusi lina ogopa jeshi la NATO/US kitu gani kinawafanya muwe na imani kwamba mnacho kifikiria mko sahihi kabisa - lini NATO iliwahi kupigana na a military powerful Nation kama Urusi, China au North Korea lini, sana sana NATO imezoea kuonea nchi ambazo ni weak kijeshi mfano: Iraq, Yugoslavia, Libya,Afghanistan,Syria etc.
Halafu watu wanakuja hapa na maoni ya ajabu ajabu eti Urusi haina lolote sana sana inajivunia missiles zake za thermonuclear basi, as if Amerika haina silaha za nuclear au Urusi kuwa na missiles mabom ya nuclear ni dhambi!!!
Sasa kama mnafikiri NATO/US wana uwezo mkubwa kijeshi kwa nini hawajiingizi kwenye mapigano ya Ukraine moja kwa moja moja badala yake wanaishia kwenye makongamano na maazimio lukuki vitisho tisho vya kitoto na sanctions chungu mzima, mpaka uchumi wao una fikia hatua ya kuyumba - mwisho wa siku wanakwenda kumbbeleza Putin yaishe kwa kupitia mawaziri wao wa ulizi -alianza waziri wa Ulinzi wa Merokani, juzi juzi kafuatia waziri wa Uingereza ambaye mwaka jana alikuwa anajifanya kifaru mwenye uwezo mkubwa wa kumumaliza Putin na jeshi lake - sasa kiko wapi na mikwala yao - wajaribu basi kuivamia Urusi kwa lengo la kumsaidia Zelensky halafu tuone kutatokea nini??