Udikteta ni nini??..
Wewe umekula udikteta acording to West.
Udikteta ni autocracy ambapo mara nyingi kuna totalitarianism(mtu mmoja au watu wachache wanafanya maamuzi yote), halafu wananchi hawana maamuzi yoyote juu ya serikali.
Udikteta Unaweza kuwa wa mtu mmoja kama Hitler, monarchy(wachache kutawala kwa kurithi) au oligarchy (kikundi cha watu wachache wanatawala)....Oligarchy inaweza kuwa Theocracy(kikundi cha kidini kinatawala kama kina Ayatollah wa Iran), plutocracy(wenye hela wachache ndio wanatawala kama urusi) au stratocracy(utawala wa kijeshi).
udikteta wa Ukoo una tofauti gani na Monarch ya uingereza??
yes Monarchy ndio udikteta wa ukoo, lakini england sio monarchy wale ni Perliament democracy maana executive power inatokana na Bunge wala sio hao kina Kings na Queen, zamani england ilikuwa monarchy lakin baada ya kuhamia democracy ndio hao makings na queens wamebaki kama pambo tu la traditionally.
Huwezi kulinganisha Uingereza na North Korea.
Mwisho nani anamfuata mwenzake kumsumbua??… Nani Chokonozi la mifumo ya mataifa mengine??..
Kuhusu kumfuata mwenzake kumsumbua wala usishangae. Hio ni nature ya binadamu.
Binadamu tunapenda kulazimisha binadamu wengine waamini tunachoamini, maana tunajua hiyo ndio njia pekee ya kuacha alama hapa duniani. Tunajua miili yetu itakufa ila ideas zetu zitabaki vichwani kwa wengine na wao watarithisha wengine.
Ndiosababu tunakesha kubishana humu jukwaani,
Ndio sababu tunahubiriana makanisani na misikitini,
Ndio sababu tunafundishana mashuleni
Ndio sababu tunavamiana jamii moja na nyingine.
Ndiomaana kila kabila hapa bongo linataka lenyewe ndio liwe na power
Ndiomaana wazazi wanataka watoto wawe kama wao
Sasa kwasababu kila mtu ana nature hivyo, Nani sasa amsikilize mwenzake na nani amwaminishe mwenzake? Ndio hapo inakuja mwenye nguvu hutumia nguvu yake kufanikisha.
Nguvu inaweza kuwa ya kiuchumi, kimaarifa, kisiasa, kimamlaka nk.
Mchungaji/sheikh ana nguvu ya kuaminisha wengine kwasababu za kimaarifa/kimamlaka
Mwalimu ana nguvu kwasababu za kimaarifa
Raisi ana nguvu kwasababu za kimadaraka
Mzazi kwasababu za kijamii
Sasaivi mnaona kama US ndio bingwa wa kuvamia kwasababu ana nguvu kiuchumi.
Lakini nchi/Jamii yoyote ikiwa na hiyo nguvu lazima ifanye hivyo..lazima ivamie jamii iliyo weak ili kuibadilisha .
Ndiomaana waislam walipopata nguvu kupitia Ottoman empire walivamia nchi nyingi na kuueneza uislam kuanzia medina mpaka middle east yote, uturuki, spain mpaka Afrika mashariki yote.
Waroma kupitia roman empire walipokuwa na nguvu walivamia ulaya nzima.
Urusi walivamia kuitengeneza USSR
Uingereza na Ujerumani nao walivamia karibia dunia nzima nk. Nk. Nk.
Hizo jamii zote zimeacha legacy..waingereza wameacha kiingereza, waroma wameacha ukristo na waarabu wameacha uislam. Nk. Nk.
Kwahyo hata ikitokea Marekani akaanguka akaja mchina, Basi lazima nayeye ataanza kulazimisha ideas zake zitumike duniani kote.
Hiyo ni nature ya binadamu na huwezi kuipinga.
Labda uruke mkojo huu utue kwenye mavi mengine.
Kwahyo solution, ni kuwa na identity yetu sisi kama sisi waafrika, na kujikuza kiuchumi, ili nasisi tuanze kuinfluence majirani kuwa kama sisi ili nasisi tuache legacy...maana tukiwa weak lazima tuvamiwe tubadilishwe na identity yetu ipotee.
Kama ilivyo saivi kijana wa kawaida wa kitanzania hajui kilugha chake ila anajua kiingereza utadhani kazaliwa washington.