Mkuu samahani ila kwa kawaida Bwana Yoda anajielimisha kabla ya kujibu. Hivyo angeweza kukujibuAtakwambia libya gafaf alikuwa dikteta na Afghanistan hakukuwa na freedom
1) kuhusu Bwana Gadafi kulikuwa na azimio la Baraza la Usalama (ambako Urusi na China wana uwezo kuzuia kila azimio) kuzuia ndege zote za jeshi la anga la Gaddafi kwa sababu aliua raia wake hovyo, na katika utekelezaji wa azimio hili nchi mbalimbali zilianza kudhibiti anga juu ya Libia na kukandamiza majaribio yote ya jeshi la GAddafi kushambulia ndegevita zao na pia kuendelea kuua wananchi. Sababu kwa uhakika haikuwa udikteta wake maana aliuwa dikteta pia kabla ya azimio la Baraza la Usalama la UM.
2) Kuhusu Afghanistan atakujibu kwamba swali halikuwa uhuru. Jambo lilikuwa mahambulio dhidi New York na Washingtona yaliyoua watu zaidi ya 3000 yaliongozwa kutoka ardhi ya Afghanistan ilhali serikali ya Afghanistan ilikataa kukabishi watendaji hivyo kujiunga na shambulio hilo. Shambulio hilo kutoka Afghanistan lilisababisha mara ya kwanza katika historia hatua ya NATO kutangaza hali ya kusaidia mwanachama aliyeshambuliwa.
Swali haliuwa uhuru bali shambulio la 11 Septemba.