Ukraine imeshapata IRIS-T SLM kutoka Ujerumani - bora kuliko Patriot. Ingawa hadi sasa beteri 1 tu. Waingereza wameleta ya vyao... Gepard inafanya kazi vizuri kupunguza droni, tuone akiba ya Urusi inadumu hadi lini.
Swali vilevile kuhusu cruise missiles. Hadi sasa tumeona shambulio 1 kubwa tu. Kwa nini hawakuwahi kuleta nyingi? Ila kati ya hizo takriban 100, asilimia 80 zilipigwa kabla ya kufika.
Uharibifu ya 20% zilizofika ulikuwa mbaya. Idadi kubwa inahakikisha kwamba kadhaa zitafika.
Ila, je wataweza kurudia? Wanazo bado roketi za kutosha?
Ukilinganisha na vita nyngine kama Iraki unashangaa jinsi Urusi imeleta vifaa vichache kidogokidogo.
Na jinsi walivyoshindwa kudhibiti anga juu ya Ukraine. Hapo siri kwamba Zele aliweza kusafiri kutoka Kyiv hadi Kherson bila matatizo. Ndege za Kirusi zilizoweza kumwamgalia kumtambua na kumzuia hazipo. . .
Mashambulio zaidi yameripotiwa kote Ukraine, siku chache baada ya moja ya mashambulizi makali zaidi ya Urusi katika vita hivyo.
Maafisa wanasema kituo cha kuzalisha gesi na kiwanda cha makombora huko Dnipro vilikuwa miongoni mwa shabaha za hivi punde na kwamba takriban watu wanne walikufa katika eneo moja.
Katika wiki za hivi karibuni, Urusi imeazimia kulenga miundombinu muhimu ya nishati ya Ukraine.
Moscow bado haijatoa maoni yoyote juu ya madai ya mashambulizi ya Alhamisi. Watu wanne walifariki kutokana na mashambulizi ya usiku kucha kwenye majengo ya makazi katika eneo la Zaporizhzhia, kulingana na ofisi ya rais.
Wakati huo huo, makombora yalipiga moja ya miji mikubwa ya Ukraine, Dnipro, alisema mkuu wa mkoa - na kusababisha moto katika viwanda na majeruhi 14.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa kiwanda cha Pivdenmash mjini humo -
ambacho kinazalisha makombora, miongoni mwa bidhaa nyingine - kimeshambuliwa kwa bomu.
Karibu na hapo, makombora 70 yalisemekana kutua kuzunguka mji wa Nikopol, na kuharibu miundombinu na kuacha maelfu ya nyumba bila umeme na maji.
-British Broadcastng Corporation
My Take: Makombora 70 yanetoboa yote Je Himars, Nasams, Vampires ziko wapi?..
Je mvua ya Maelfu ya Makombora yenye Nukes yakisukumiwa Ulaya na US yatazuiwa yote?.. Je nao wakiretaliate Russia ataweza kuyazuia yote toka NATO?
Dunia inaendelea kujifunza vitu kuhusu AntiMissiles na Ufanisi wake!!..
Hakuna aliye tayari na WW III so far.
- Ni mimi Pro 4-Superpowers kutoka Usagara Mizani.
Soma :