Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,010
- 6,766
Mkuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Mark Milley anasema Kyiv inaweza tu kutumainia suluhu za kisiasa
Uwezekano wa Ukraine kupata ushindi wa karibu wa kijeshi dhidi ya Urusi si mkubwa, Jenerali huyo wa ngazi za juu huko Marekan ameonya. "Nimegundua kuwa licha ya maendeleo ya hivi karibuni ya Kyiv kwenye uwanja wa vita na kutekwa kwa jiji la Kherson, Moscow bado ina uwezo mkubwa wa mapigano nchini humo."
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Pentagon siku ya Jumatano, Milley alisema kwamba "uwezekano wa ushindi wa kijeshi wa Ukraine unamaanisha kama kuwafukuza Warusi kutoka Ukraine yote ikiwemo kujumuisha madai ya kuirudisha Crimea, uwezekano wa kutokea hilo wakati wowote hivi karibuni ni mdogo kijeshi."
Jenerali huyo alibainisha, hata hivyo, kwamba kuna uwezekano wa "suluhisho la kisiasa" ambalo lingeiona Urusi ikijiondoa katika maeneo ambayo Ukraine inadai kuwa ni yake, na kuongeza kuwa Urusi "imekaa chini hivi sasa haijasimama kupambana kwa nguvu zote" na kwamba Ukraine inahitaji mazungumzo kutokana na "advantage ya uwezo iliouonesha mpaka sasa."
Milley pia alisisitiza uungaji mkono wa Washington kwa kyiv na kuapa kuendelea kwa muda mrefu kama ikibidi - kauli ambayo iliungwa mkono na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ambaye pia alishiriki katika mkutano huo na waandishi wa habari.