Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Nikwambie kitu mkuu, nisikilize kwa umakini: kama Putin angehamua kutumia mbinu za kivita za Wamerikani ie "shock and awe"miji ya Ukraine na critical infrastructures zote zingekuwa bombed back to stone age ERA, na Senselessky angekimbilia uhamishoni US ilishayalishia helicopter ya kumuhamisha/torosha kwenda uhamishoni - mwanzo Putin alitumia ustaarabu sana hakutana kuiharibu Ukraine na hasa kuwapa shida/taabu raia wa Ukraine kumbuka Ukraine na Urusi ni kama ndugu wanagombamishwa tu naataifa ya magharibi yenye agenda zao za siriza kuitumia Ukraine kwa lengo la kuihujumu Urusi kiuchumi na kuidhoofisha kijeshi - hilo ndilo lengo lao kuu, hawajali cha Ukraine wala raia wake.

Tukija kwenye kutambua kimataifa majimbo ya kusini mashariki mwa Ukraine,je,umewahi kupitia hata siku moja kwenye makubaliano 12 ya Minsk2 yanayo husu Urusi na Ukraine ukaona yalikuwa yanagusia vitu gani muhimu kuhusu malidhiano ambayo yalisomamiwa na Angela Merkel na Rais wa Ufaransa - who can blame Putin kwa kuchukua hatua za haraka ku-pre empty njama zilizo kuwa zinasukwa na NATO/US kuhusu Urusi kwa kupitia jeshi la Ukraine na baadhi ya troops za NATO/US walio valia uniform za jeshi la Ukraine ili wasitambulike kirahisi - bottom line, is: Sio kwamba Putin alihamka asubui moja na kuhamua kuivamia Ukraine hiyo si kweli - alitaka kuondoa tishio lilokuwa dhahili dhidi ya Taifa lake,je,,wewe ungefanya nini - NATO/US walikuwa wanapuuzia Russian security concerns za Taifa lake licha ya Putin kuwakumbusha NATO/US mara kwa mara, walikuwa wanamcheka tu na kuzidi kuvimbisha kichwa Senselessky - kumbe mlitaka Putin afanye nini?? Mambo ya Putin kupitisha referamdum kwenye majimbo ya kusini mashariki hapo alitaka kutumia ustaarabu angeweza kabisa kuyachukua bila ya kujali NATO/US wanasema nini, Ukraine kuwndelea kurusha makombora wala hayatamsaidia chochote cha umujimu mi kwamba majimbo hayo hayatarudi tena Ukraine wanao amini tofauti wanajisumbua makimbo hayo yataendelea kuwa sehemu ya Urusi west watake wasitake - ukweli ndio huo.

Mani kawambia Putin kashindwa KHERSON wakati asili mia 70% bado hipo chini ya jeshi la Urusi - hata mtu ambaye hajui mbinu za kijeshi hawezi kushindwa kugundua kinacho endelea mjini KHERSON sikilizeni kauli za wateule wa Senselessky mjini KHERSON wanasema nini, mbona wote wanaonekana ni woga na hawaji amini Urusi inapanga nini kuhusu hatima ya mjini huo kiujumla hata Jenerali wao niliwahi kumsikia akitilia shaka uondokaji ghafla wa jeshi la Urusi mashariki mwa mji wa KHERSON -sasa sisi watu baki ndio tujifanye we know better than five star Generals!!

Nimalizie kwa kusema kwamba aslimia kubwa ya precision missiles zinazo rushwa kwenda kupiga designated targets inside Ukraine zinarushwa na Russian black sea fleet, unaposema kwamba fleet hizo ni mapambio sijui una maana gani mkuu, mwenye macho aliona jinsi meli hizo zinavyo tumika kikamilifu kutekeleza majukumu taka husitake ukweli ndio huo, zimesaidia sana kuharibu zaidi ya asilimia 40+ ya vyanzo na usambazaji wa umeme nchini Ukraine na tukiongrzea mashabulizi ya jana na leo sina shaka asili mia 50% za vyanzo vya umeme na usambazaji zinakuwa zimeharibiwa raia zaidi ya millioni 14 hawana umeme nisijue usamazaji wa maji huko hali gani hali ni tete sana we sema jamaa wanajikaza kisabuni tu-lakini kama Senselessky angekubaliana na masharti ya Minsk2 bila ya kuwasikiliza akina Biden na Boris Johnson walio mpoteza wala Ukraine hisingefikia hatua hii mbaya ya vita, vita ingesitishwa mwezi wa nne mwaka jana.
 


Matokeo hayo yatafanya iwe vigumu kwa Kyiv kusafirisha wanajeshi hadi maeneo ya vita, Moscow imedai.

Moscow ilidhoofisha uwezo wa Ukraine wa kusambaza silaha na wanajeshi kwenye mstari wa mbele kwa kufanya mashambulio ya masafa marefu, yenye usahihi wa hali ya juu siku ya Jumatano dhidi ya vituo vya muhimu vya kijeshi na miundombinu ya nishati, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema.

“Lengo la mashambulizi hayo limetimia. Malengo yote yaliyowekwa yamefikiwa, "msemaji wa Wizara ya Ulinzi Luteni Jenerali Igor Konashenkov aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wake wa kila siku. Aliongeza kuwa mashambulizi ya ndege za nchi yake, meli za kivita na wanajeshi wa nchi kavu "zimetatiza usafirishaji wa vikosi vya Ukraine, silaha za kigeni, vifaa vya kijeshi na zana za kivita kwenye maeneo ya mapigano kwa njia ya reli."

Konashenkov alisisitiza kuwa wanajeshi wa Urusi hawakulenga kyiv. "Uharibifu wote ulioripotiwa na mamlaka ya Kyiv ulisababishwa na makombora yaliyoanguka ambayo [yalirushwa] kutoka kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Kiukreni iliyowekwa katika maeneo ya makazi ya mji mkuu wa Ukrain," alisema.
 
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza aliiambia CNN kwamba Berlin ilitaka Kyiv "kusalimu amri" kwa Moscow


Ujerumani imeelezea madai ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson kwamba serikali yake ilitaka Ukraine kusalimu amri kwa Urusi kama "upuuzi mtupu."

Msemaji Steffen Hebestreit alikuwa akijibu Jumatano kwa matamshi ambayo Johnson aliyatoa kwa CNN, ambapo alipendekeza kuwa Berlin ilitaka mzozo kati ya Urusi na Ukraine umalizike haraka kwa sababu za kiuchumi.

"Ni upuuzi mtupu alichosema Boris Johnson," Hebestreit aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa vyombo vya habari vya serikali mjini Berlin. "Tunajua kwamba waziri mkuu wa zamani anayeburudisha kila wakati ana uhusiano wake na ukweli," afisa huyo akaongeza, akipendekeza kwamba "hii sio tofauti katika kesi hii."

Alipoulizwa na waandishi wa habari kama angemwita Johnson mwongo, Heberstreit alisisitiza kauli yake ya awali, lakini hakujibu swali hilo moja kwa moja. “[Johnson] daima ana mtazamo wa kibinafsi kuelekea ukweli,” msemaji wa serikali alijibu. Aliongeza kuwa alilijua hili "mapema," kwa kuwa "alishiriki katika mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza wakati huo huko Munich siku chache kabla ya kuanza kwa vita."

Mapema Jumatano, Johnson aliiambia CNN Ureno kwamba Ujerumani inaamini "ingekuwa bora kwa jambo zima kumalizika haraka, na kwa Ukraine kusalimu amri" kabla ya Urusi kuzindua kampeni yake ya kijeshi huko Ukraine. Berlin pia iliunga mkono msimamo wake kwa "aina zote za sababu za kiuchumi," kiongozi huyo wa zamani wa Uingereza aliongeza.

Heberstreit alijibu kwa kusema kwamba dai kama hilo haliungwi mkono na ukweli. Kansela Olaf Scholz na serikali yake "waliachana na mazoea ya kitaifa ya miongo kadhaa ya kutotuma silaha katika maeneo yenye shida na maeneo ya vita," alisema, akiongeza kuwa msaada wa kijeshi wa Ujerumani kwa Kyiv "haujawahi kutokea katika suala la ubora na wingi."

My Take:
I repeat vita hii mchochezi na US na UK iko wazi. Rest of EU hawakutak. France ndo hawapendi kuminyan n Urusi kabisa..

Taaratibu wafu wanaanza kuzikana, Time will tell; Naiona EU wakiparaganyika na kuvurugana kuhusu Ukraine. Hii ishu ya Ukraine itaacha alama kwenye EU... Nimekaa pale
 
Putin hana sababu za msingi za kuanzisha hii vita. Mwisho wa ubaya aibu
 
Warusi wameshindwa kuichukua Bakhmut wanapigana hapo tangu August wakati huo Ukraine kuanzia late August imechukua Kharkiv, Kupiansk, Izyum, Snake Island, Lyman na Kherson. Russia Vita vya ardhini akubali tu haviwezi anachoweza ni kulipua transfoma za Kiev[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukweli ni kwamba Putin hakutumia njia hizo mwanzoni sababu aliidharau Ukraine akijua yatajirudia yaleyale kama alivyoichukua Crimea kiulaini,alivyokua akiunga mkono waasi kupigana na majeshi ya Ukraine kule Donbass,kama alivyoipiga Georgia kwa siku kumi. Hata mwanzoni CIA walitabiri Ukraine ingeanguka ndani ya wiki tu,wanajeshi wa Urusi wangekua Kiev lakini kilichowakuta Urusi hawatokuja kusahau.
Unakumbuka wale special forces wa Russia kina Spetsnaz walivyochinjwa kama kuku pale Hostomel air port?!
Unakumbuka majeshi ya Urusi yalishaingia Kiev lakini yalifurushwa kama wezi na wanajeshi maelfu wa Urusi kuuawa huku Urusi ikipoteza vifaru kibao na silaha nyingine nyingi?!
Si kwamba Russia hapendi kutumia mbinu za Wamerekani Ila ukweli ni kwamba huwezi aliodhani anao HANA, Airforce ya Urusi mpaka sasa imeonyesha kwamba ni Simba wa karatasi,mwezi wa 9 sasa Urusi hana air supremacy sasa hizo shock and awe atafanya kwa kutumia nini?! Parashuti?!
Ukraine isingetaka kujiunga NATO kama ingekua na jirani asiyetabirika kama Urusi,Urusi hapo kwa backyard yake kila siku anapoteza ushawishi kwa tabia zake za kutaka kulazimisha ufate matakwa yake la sivyo anakuvamia na kuchukua eneo lako kinguvu sasa this time around watu wamesema inatosha lazima ashughulikiwe ndio kinachomkuta hivi sasa huko Ukraine. Hakuna jirani hata mmoja wa Urusi ukiacha North Korea hata wale ambao ana treaty nao ya CTSO kama sikosei aliyemsapoti kwenye Umoja wa mataifa, mpaka Armenia hua ina abstain au inapiga Kura ya against dhidi ya Russia.
Hivyo si kweli kwamba Ukraine ilikua inatishia usalama wa Urusi ila tabia za Urusi ndio zimefanya Ukraine ijihami na kutaka kuingia NATO ili kujihakikishia usalama wake.
Juzijuzi hapa baada ya Kazakhstan kupinga kuyatambua majimbo ya DPR na LPR tulianza kusikia maneno toka wanasiasa wa Urusi wakianza kuquestion utaifa wa Kazakhstan wakisema kwamba ni sehemu ya Urusi kisa tu imekataa kukubali uhuni wa Putin,miaka ijayo Urusi ikiivamia Kazakhstan itakuja na sababu hizihizi kwamba inatishia usalama wa Urusi.

Kujiunga Kwa NATO wala haikua sababu kuu ya Putin kuivamia Ukraine ila Putin anataka kuirejesha USSR na hili ameshalizungumza mara nyingi Sana kwamba kuvunjika kwa USSR ilikua ni kosa kubwa kihistoria,tatizo ni kwamba hizo ni ndoto za alinacha USSR is dead &gone na haiwezi rejea tena.
 
Unasema majimbo hayarudi tena Ukraine wakati theluthi ya Kherson imesharejea na bado Ukraine inaendelea na counteroffensive kuchukua sehemu iliyobaki!!!!!! Na tukiangalia trend ya Vita hii Urusi akipoteza eneo kulichukua tena inakua mtihani wakati Ukraine hali ni tofauti ikichukua eneo inahakikisha Urusi hawezi kulichukua tena.

Mwanzo ulisema Ukraine na Urusi ni ndugu sasa hivi unatueleza Urusi imeharibu 50% ya miundombinu ya nishati na Raia 14m hawana Umeme. Kwahiyo Urusi baada ya kushindwa kivita imeamua kutesa Raia wa Ukraine?!!!!!!
 
Kimoja Jana kabla ya mechi kilitangaza kwa hereni mechi ilipoanza kikavua na penalty kikafunga licha ya kunduwazi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…