Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kuna taarifa kuwa Russia wamezuia hadi watu wao wasifungue baadhi ya mitandao ya jamii. Sidhani kama kuna TV kutoka huko itakayokuwa na uhuru wa kueleza what is going on exactly. Hata hivyo Russian wamekaribia sana kumiliki Eukraine.
Baada ya kukaribia kumiliki Ukraine,ni kipi kilifuatia?

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 

Katika watu ambao wanatamani hii vita iishe mapema bhas ni Putin ndio maana walianza kupiga miundombinu ya nishati ili Ukraine ikubali kukaa mezani lkn hilo limefeli

1. Vita ikichukua muda mrefu si Ukraine tu atakaefirisika hata huyo Russia atafirisika,Uchumi wake mwaka Jana ulipungua kwa -4%.
Unasema Russia apigane vita mpk 2030,nadhani unajua kwamba Russia inategemea Sana uuzaji wa mafuta na Gas na ndio sekta zinazochangia pakubwa kwenye pato pamoja na bajeti ya Taifa.Vipi kabla ya mwaka 2030 Bei ya Mafuta ikashuka Sana mfano pipa chini ya $40,unadhani huyo Urusi atapata wapi fedha za kuendesha hiyo vita?! Maana kuna taarifa zinadai Russia inatumia $1 BN kwa siku kwenye hii vita,na hiyo ilikua karibu miezi 6 iliyopita hatujui Kwa sasa inatumia kiasi gani cha fedha.

2.Kwani malengo ya Marekani hapo Ukraine ni yapi?!

3.Naweza kusema tishio la NATO ndo limeongezeka baada ya hii vita maana Russia ilitaka Ukraine isijiunge NATO ili kuzuia majeshi ya NATO yasiwe mpakani mwake lkn baada ya Vita nchi mbili zilizokua Neutral karibu miaka 100 zimeona tishio la Urusi zimeomba uanachama wa NATO. Soon Finland na Sweden zinajiunga NATO,na Finland ina mpaka mkubwa na Urusi.Putin alitaka azuie NATO matokeo yake kapata NATO zaidi.

4. Unaididimizaje USA na NATO wakati hii vita imekua kama wake-up call kwao,kila ya nchi ya NATO na West kiujumla inajihami kwa masilaha si Poland,Baltic State mpk Ujerumani iliyokua inasuasua kwenye Ulinzi imetenga $100 BN ili kulijenga jeshi. Bajeti za Ulinzi za Ufaransa, Uingereza mpaka vile viBaltic states zote zimeongezwa.
Ukija kwenye suala la biashara na ushawishi ndio kabisa hii vita imeongeza ushawishi wa Marekani hapo Europe, kibiashara Kwa sasa Marekani inauza Gas ya kutosha hapo Europe baada ya Urusi kupunguza kiwango cha Gas kinachoenda Europe. Kiulinzi karibu nchi zote hapo zimepanga foleni ya kununua silaha toka Marekani,Ujerumani alikua hana mpango wa kununua F-35 lkn baada ya hii vita wanataka F-35. Demand ya HIMARS imeongezeka mpk Lockheed Martin wameongeza uzalishaji wake mara mbili. Poland tu imeweka order ya kununua Himars 500. Hapo bado kuna Estonia, Lithuania na wengineo wote wanataka hiyo silaha. Kiufupi NATO ndio imezidi kuimarika.

5. Unatanuaje himaya wakati hujashinda kijeshi?!
 
Dikiteta ana mikwara mbuzi kweli..,baada ya Finland na Sweden kutuma maombi ya kujiunga NATO ikawaje Tena [emoji16][emoji16]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Endelea kuota.
Russia akitaka Vita iishe si hata kesho ana ondoa tu majeshi yake.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

"Zakharova said during a news briefing: "Finland and Sweden should not base their security on damaging the security of other countries and their accession to NATO can have detrimental consequences and face some military and political consequences."
 
Halafu tukiwaambia Putin alidhamilia kutumia saa 72 katika operation ya kijeshi kuwaondoa wanazimamboleo mnatuona wakorofi

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Ataongeza MKUU maana nasikia mobilize ipo njiani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RUSSIA na PUT IN wakitaka SMO iishe nirahisi tu c wanaondoka UKRAINE

Ila kwakua hawataki SMO imalize punde wamesema wazi ili SMO imaliE UKRAINE wayatambue hayo maeneo kama ni RUSSIA la sivyo wanaendelea na SMO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni SMO, Vita kamili bado haijatangazwa....labda tusubiri mwaka huu
 
Kwani we hujui siraha za URUSI.
Sasa kama alitumia hypersonic missile muliifanya nini, maana hata Nato Na USA HAWANA hio.
Kwanza nikukumbushe
HII NI SPECIAL MILITARY OPERATION ZONE.
na wameweka limit ya matumizi ya siraha hata USA wanajua,
INGIA YOUTUBE TAFUTA DOCUMENTARY YA SPECIAL MILITARY OPERATION UTAIONA.
ILIKUWA CHANNEL NYINGI TUU YOUTUBE , NA WANZEE WA MAGHARIBI WALIIONDOA
ILA STILL IPO.
 
Kama hawana equipment nzuri inakuwaje bdo anazid kusonga mbele na Ukraine kila cku inaharibiwa ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…