Ina maana Supa-pawa kapoteza askari 100,000 (mpaka kafanya mobilisation ya wengine 300,000) na mamia vifaa (ndege, vifaru, IFV, helicopter, moskova, howitzers n.k ) vyote vimeteketea ndani ya SMO tu?.........Sasa ikiwa full war si itakuwa janga ?
Rafiki yangu Proved.
Anaepigana full scale war ni Ukraine,Urusi ndio ilikua kwenye SMO.
Kama Mwamba Putin keshatangaza Full scale war hakika nakuambia Hali itakua mbaya zaidi.
Kama ni kweli unasema Urusi kapata hasara hiyo,basi ujue hiyo imetokana na SMO kua ya kistaarabu.
Akianza Vita kamili Ukraine itavurugwa vibaya mno.
Najua huipendi Urusi,lakini ni lazima ukubali kua Urusi Ina nguvu mno.
Urusi saizi yake ni NATO sio ukraine.
Kama Urusi Ingekua ni dhaifu kama ambavyo mnaaminishana humu nakuhakikishia kabisa pasipo na shaka kua NATO wange ingiza majeshi kamili kama walivyofanya Yugoslavia.
Kwa jinsi wanavyoionea huruma Ukraine na kwa jinsi Urusi anavyoipiga Ukraine nakuambia NATO wanaumia mno.
Sasa hata wewe jiulize TU swali jepesi.
Mbona hawakuwapa silaha waasi wa Libya? Waliingiza ndege zao kuwapiga wanajeshi wa Gaddafi.
Mbona hawakuwapa silaha Kuwait?
Waliingiza majeshi kamili kumpiga Sadam.
Mbona hawakuwapa silaha Wakosovo na wahanga wengine wa Yugoslavia?waliingiza majeshi.
Mbona hawakuwapa silaha waasi wa Syria?
Waliingiza majeshi ingawa waliondolewa na Urusi baadae,lkn walishapeleka melivita na ahadi ya Assad "must" go.
Na Kuna baadhi ya nchi NATO "waliweka no fly zone"
Ukiangalia mateso anayoyapitia Ukraine na ukiangalia michango ya silaha, intelligence,pesa na vikwazo ili kumdhiofisha Urusi,na ukiangalia hii SMO jinsi inavyowaathili Europe,USA na Dunia,inaonekana hii SMO ya Urusi dhidi ya Ukraine imewagusa sana na wanaionea huruma sana Ukraine,ndio utaona kua,Sasa ulikua ndio wakati sahihi na sababu tosha kabisa za NATO na west kumpiga Urusi,hasa ukizingatia hoja zenu kua Urusi ni dhaifu na Supapawa wa mchongo.
Sasa NATO wanasubiri Nini?Ukraine inazidi kuharibika na Europe inazidi kuathirika,wakimbizi,maisha yamepanda,biashara zimeharibika,usalama umeondoka,silaha zao kwenye maghala zimepungua.
NATO wanasubiri Nini Tena? Huu ndio wakati sahihi wa kuingiza majeshi kamili,sio misaada ya silaha.
Full scale war kwa Urusi maana yake ni kuangamizwa kwa Ukraine.