Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nimekuelewa ila ndugu zetu wana mahaba ya kuongeza namba ajabu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kuna vitu vingine ni vichekesho kwa kweli.yani unaongelea msaada wa kirafiki wa vifaru vya sherman.

Vifaru vya kwanza vikifika mwishoni mwaka 1944 na vingine vikaenda mwaka 1945. Vita si ilikuwa ipo berlin.sasa hapo utasema wamemsaidia kumshinda mjerumani kweli.[emoji23][emoji23][emoji23] ebu kuweni serious[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu jaribu kukusanya data kidogo. Jumla ya vifaru kutoka uingereza kwa umoja wa kisovyeti ni zaidi ya 5,000 si 300. Pamoja na zile 13,000 kutoka Marekani si idadi ndogo kabisa! Muhimu zilikuwa pia ndege 14,000.

Halafu misaada kutoka Marekani zilikuwa muhimu kabisa hadi kurudishwa kwa uwezo wa tasnia ya kirusi baada ya uvamizi wa ujerumani. Maana mwanzoni mwaka 1941 Wajerumani walishika mara moja maeneo kama Ukraine na Belarus ambako sehemu kubwa ya viwanda vilikuwepo. Warusi walijitahidi kuhamisha viwanda na wafanya kazi kwa reli kuelekea mashariki, mbali na mapigano, na kuanzisha viwanda viypa. Hii ilichukua muda.

Halafu hujui Khrushchev allandika nini katika kitabu chake? Ukijua Kirusi, soma hapa (nakala ya Kiingereza sijui): ВОЕННАЯ ЛИТЕРАТУРА --[ Мемуары ]-- Хрущёв Н.С. Время. Люди. Власть. (Воспоминания). Книга I (Mwandishi alikuwa kiongozi chini ya Stalin akamfuata kama mkuu wa Umoja wa Kisovyeti)

Anakumbuka jinsi gani Stalin mwenyewe aliseme: "ikiwa Marekani isingetusaidia, tusingeshinda vita hii: ana kwa ana na Ujerumani ya Wanazi, tusingestahimili mashambulizi yake na tungeshindwa vita."
Kwa hiyo, tafadhali ujisomee halafu usipambane na mimi, pambana na Stalin na Khrushchev na wanahistoria waliochungulia mambo hayo.
 
Basi Hitla alikuwa anatisha sana. Kama dunia yote ilipigana naye kwa miaka 5 basi jamaa alikuwa bonge la dude.
 
Ivyo vifaru 5000 Kutoka wingereza na 13000 kutoka Marekani vinaitwaje[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].na vilienda lini
 
Na hivo captured kumbuka vinakuwa recaptured au destroyed
 
Usitupe maneno matupu weka ushahidi wa kuonyesha Warusi walipokea vifaru 13000 vya aina flani kutoka USA na vifaru 5000 vya aina fulani kutoka UK.
 
Mkuu naona unapenda shairi au visa kama Abunuwasi basi nenda mahali pake. Nimeleta hapa picha za kifaru cha kiingereza kwneye mapigano ya Kursk 1943 na wee und dai eti hakuna kitu kilichofika hadi mwisho wa 1944... (Labda hujui mapigano ya Kursk? Basi hii ni mapigano makubwa ya vifaru katika historia... Lakini mshairi si lazima kujua historia, nakubali)

Misaada ilianza kufika mwaka 1941 ilikuwa lazima kwa Urusi kutoshindwa.
Labda nikusaie historia nyingine: mapigano yote kwenye bahari ya Atlantiki yalihusu hasa majaribio ya Wajerumani kuzuia misaada ya Marekani kufika urusi. Jaribu kujisomea!

Pia uvamizi wa Iran mwaka 1941 na Uningereza ilitokea kwa sababu Uingereza na marekani walihitaji Iran kufikisha vifaru na malori yao kufika Urusi kupitia bahari ya kaspi.

Ila ukiona ugumu kushika hayo yote: tulia, maana wewe ni mshairi, una uhuru wote kuwaza unavyopenda-
 
Vita zote huwa kuna coalition....US vita zote NATO wapo, haendi peke yake, na akienda peke yake cha moto anakiona:Vietnam...

Unatumia justification za ajabu sana kujustfy kuwa Urusi hana nguvu....Nafikiri nenda katembelee sources za west zinazoongelea powerful countries- (military)

Usiongee kwa hisia na wishes zako tu...

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tafadhali nionyeshe iko wapi nilisema Urusi haina nguvu? Iliharibu Afghanistan kabla ya kushindwa kule, iliharibu Chechnya , leo inaharibu sehemu za Ukraine vibaya sana.

Nilimjibu jamaa aliyedai eti jeshi la Marekani linatetemeka likikumbuka jinsi Urusi ilishinda ujerumani. Hii siamini, hasa kwa sababu wanakumbuka kwamba bila msaada wa marekani urusi isingeshinda.

Na pia sasa wakiona hali ya silaha na jeshi la kirusi. Ni hiyo tu.
 
Usitupe maneno matupu weka ushahidi wa kuonyesha Warusi walipokea vifaru 13000 vya aina flani kutoka USA na vifaru 5000 vya aina fulani kutoka UK.
Mkuu ukiamua kuwa peupe na kubaki vile basi shauri lako.
Ukiweza kusoma, jisomee kuhusu "Lend and Lease".
Menginevyo jaribu kuonyesha kwamba nimeleta nukuu ya Stalin isiyo kweli. Nimekupa chanzo. Stalin mwenyewe alisema: "ikiwa Marekani isingetusaidia, tusingeshinda vita hii: ana kwa ana na Ujerumani ya Wanazi, tusingestahimili mashambulizi yake na tungeshindwa vita."
 
Mbona unabadilika badilika kama kinyonga.ni wapi nilipokwambia Vifaru vya wingereza vilichelewa kufika Urusi.wewe si umeweka picha na maelezo juu kuwa vifaru vya Marekani vikiwa na warusi mwaka 1945. Au sio wewe pacha wako[emoji23][emoji23][emoji23]


Wapi niliposema kuwa vifaru vya wingereza vimefika mwaka 1945 Urusi.nimekwambia vifaru vya wingereza alivyopewa Urusi ni vifaru 300 tu.sasa ivyo 5000 vimetoka wapi na vinaitwaje
 
Lete iyo speech ya Stalin akisema ivyo
 
Mkuu pole sana, naona mambo mengi mapya yanakuchanganya kidogo.
Kwanza ulidai msaada wa vifaru ulifika 1944, pili unaonyesha mwenyewe picha ya kifaru cha kiingereza mwaka 1943 huko Urusi,
tatu sihitaji picha kuthibitisha kwamba vitu hivi vilifika urusi mapema maana hii ni topic ye elimu ya historia ianyojulikana.

Nne unakuja na kuuliza "Wapi hotuba ya Stalin" ilhali nimekuonyehsa hapo juu pamoja na kuleta chanzo kabisa nukuu nimepata wapi. Pole sana!
 
Haya si binadamu yoyote yule anaweza kuandika.kwani hayo maneno alisema akiwa chumbani.si mbele za watu, kama ni mbele za watu lazima kuna ushahidi.tuletee tunasubiri iyo kauli ya Stalin kuwa bila Marekani na Uk wasingeshinda vita.
Basi uichukue kama kauli ya Nikita Sergeyevich Khrushchev. Huyu alikuwa A) binadamu B) aliweza kuandika na C) aliandika kitabu kuhusu maisha yake.

Alikuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu ya Urusi wakati wa Vita Kuu ya Pili, na baada ya kifo cha Stalin alikuwa kiongozi mkuu wa Umoja wa Kisovyeti.

Naukisoma katika chanzo nilichokupa, anakubali maneno yale anayoonyesha kama maneno ya Stalin. Ila ukipenda kumwona Stalin tofauti, si kitu. Uyachukue kama maneno ya kiongozi mkuu wa Umoja wa kisovyeti 1953 - 1964. Na ofisa muhimu katika utetezi wa Stalingrad wakati wa vita.
 
Hii si uliweka wewe au sio wewe huyu.vifaru vya sherman unajua vikienda lini Urusi.kama ujui basi angalia kwanza alafu urudi tena.naimani kusoma unajua ebu soma vizuri nimekuwekea hapo chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…