Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Unajua Cuban missile crisis?Msiongee tu maneno ya rejareja!
Mkuu, tunaijua vema. Warusi walileta makombora ya kubeba mabomu ya nyuklia kisiwani. Hii ilikuwa tishio la kimakusudi. Marekani haikuandaa uvamizi, bali kuzuia meli zisifike tena Kuba na kutisha kubomoa vituo vya roketi kwa mashambulio kutoka hewani.

Hakuna aliyeleta makombora Ukraine. Ukraine kwa hiari yake iliwahi kuachane na silaha zake za nyuklia, na Urusi iliahidi kutunza na kutetea mipaka ya Ukraine daima. Urusi imeendelea kuvunja ahadi zake na mikataba yake tangu 2014.

Urusi iliamua kuvamia nchi jirani
a) kwa imani potovu kwamba ingekuwa kazi rahisi
b) bila kujali ahadi zake na haki.
 
Jana na leo umeondoa sifuri. Yaani mpaka tukufundishe kudanganya.

Kipanya kweli kweli
Alafu hii inaonyesha kwamba mnafuatilia takwimu ninapowaletea.., shukrani sana comred [emoji120]., kumbe sipigii ngoma majini.., kidogo nianze kukata tamaa nikidhani Huwa mnazipita tu takwimu zangu bila kuzichunguza vizuri..,hii imenipa nguvu ya kuzileta hapa kila siku[emoji1787][emoji28][emoji16]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
US ni taifa chochezi,litafanya chochote kuendelea kuwa namba Moja duniani!
Hata mahasimu wake wapo tayari kufanya chochote ili kumpokonya ufalme, hivyo hakuna cha kushangaza hapo.
US Kwa miaka 6 amekuwa akijaribu kuishawishi Philippines Ili iweke base ya kijeshi huko lakini Rais aliyepita aliwasikiliza wananchi ambao walikuwa hawataki tension yoyote kati ya Philippines na China na badala yake wawe na ujirani mwema!
Walipokataa kwani walilazimishwa kwa nguvu au kuvamiwa ?....si waliachwa na msimamo wao ?...
Rais huyu aliyeingia,amepuuza ya mtangulizi wake na ndani ya muda mfupi,a deal is made na tutaona US troops zikitua nanga Philippines!
Sasa hapo kosa ni la nani ?...Mkeo akitongozwa akakubali kuzini kosa si la kwake?....Sasa kwanini umlaumu US kwa maamuzi ya Rais wa Ufilipino ?
 
Huyo jamaa mm nilishamshtukia mda mrefu Sana Mia nane wamechinjwa hao Mia nane haleti link,picha Wala source ila ana edit tu sifuri zake sijui anazipata wapi hizo data tupuuze habari kutoka kwa huyu jamaa za kuchinjwa hazina ushirikiano Wala uhalisia.
Mkuu,Huwa naleta chanzo zaidi ya kimoja kuwaonyesha jinsi warusi wanavyochinjwa., hivyo kama hutaki kuamini,Hilo ni tatizo lako binafsi,

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Endelea kuandika mipasho ila ndio hivyo dawa inawaingia!
Endeleeni kujipodoa na kuvaa nguo za kike Ili msipelekwe frontline kufagiwa😃😃😃

Sio mipasho, tumekua humu, urusi ilivyo jaribu kuparamia Kyev na msafara wao wakafukuziwa mpaka leo wanagombea kamji ka chumvi, wameuawa zaidi ya 127,000 hiyo ni idadi mara nne ya JWTZ.
 
Urusi Hana shida ya maeneo yenye malighafi.Mwenyewe anayomalighafi ya kulisha dunia nzima.ameyachukua hayo maeneo Kwa Sababu ya kiulinzi.kwa mfano ameweka navy base Crimea,pili kachukua karibu maeneo mengi ya bahari ya Ukraine,Ukraine soon atabaki bila bahari haya yote ni kuendelea kujizatiti kiulinzi dhidi ya NATO.sababu kubwa ni ya kiulinzi Tu hakutaka hayo maeneo yaanguke mikononi mwa NATO.pili kuwalinda warusi waliokuwa wanaishi maeneo hayo Kwa sababu wakazi wa hayo maeneo ni warusi na wanapigana na serikali ya Ukraine Vita kuanzia siku nyingi Tu.Alafu urusi anataka kutumia hii Vita kuingia mkataba mpya wa kiulinzi na NATO baada ya misk agreement kufa.kwa kifupi haya yote yanatoke Kwa sababu urusi analinda ustahi wake na uhuru wake Kwa kuongea ulinzi.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Mkuu tafadhali usiamini hadithi za Abunuwasi! Wakazi wa Ukraine wa mashariki wanaongea mara Kirusi, mara Kiukraine. Walipiga kura mara kwa mara wanataka kuendelea kama raia wa Ukraine, pamoja na watu wa Donabas kabla hawajavamiwa na Putin.
Putin anatumia utamaduni wa watu kupika supu yake ya kisiasa.

Halafu hakuna haki kuvamia maeneo ya majirani ukisikia "sababu za kiusalama". Hii ilikuwa siasa miaka 200 iliyopita. Tangu 1945 viongozi wa madola wamepelekwa mahakamani wakivunja haki ya kimataifa (na kuwa wadhaifu ili waweze kukamatwa...) Tuone Putin ataendeleaje!
 
Hata mahasimu wake wapo tayari kufanya chochote ili kumpokonya ufalme, hivyo hakuna cha kushangaza hapo.

Walipokataa kwani walilazimishwa kwa nguvu au kuvamiwa ?....si waliachwa na msimamo wao ?...

Sasa hapo kosa ni la nani ?...Mkeo akitongozwa akakubali kuzini kosa si la kwake?....Sasa kwanini umlaumu US kwa maamuzi ya Rais wa Ufilipino ?
Napendaga unavyowajibu,ndio maana sometimes Huwa Wanahamaki na kutoa mitusi maana ukweli unauma[emoji16][emoji28][emoji1787]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Hata mahasimu wake wapo tayari kufanya chochote ili kumpokonya ufalme, hivyo hakuna cha kushangaza hapo.

Walipokataa kwani walilazimishwa kwa nguvu au kuvamiwa ?....si waliachwa na msimamo wao ?...

Sasa hapo kosa ni la nani ?...Mkeo akitongozwa akakubali kuzini kosa si la kwake?....Sasa kwanini umlaumu US kwa maamuzi ya Rais wa Ufilipino ?
Hapo Naona umeelewa kuwa US ndiye huzishawishi hizi nchi kuungana naye kijeshi!
Ndio nikasema,ikitokea Russia au China wakafanya hivyo Venezuela,Cuba na Mexico,Je US atakubali?Jibu ni hapana na atakuwa tayari kuzivamia hizo nchi Ili kuzuia Hilo lisitokee!
Ndio maana nikakuwekea hapo Cuban missile crisis Ili ujikumbushe US alivyo mnafiki!
Ndio maana kwenye historia,US ndio taifa ambalo limepigana vita nyingi sana!
Muelewe,Juzi tu hapa Tony Blair ameomba radhi na kutubu Kwa kushiriki kuivamia Iraq Kwa taarifa za uongo za kubumba za US!Wameenda wameua raia wa Iraq bila sababu,ila interests za US !
 
Sio mipasho, tumekua humu, urusi ilivyo jaribu kuparamia Kyev na msafara wao wakafukuziwa mpaka leo wanagombea kamji ka chumvi, wameuawa zaidi ya 127,000 hiyo ni idadi mara nne ya JWTZ.
Ndio maana Putin analialia kwamba anapigana na wanazi.., maana kaona wazi kwamba kipigo kinakuwa kikali mno 🥱🥱

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tafadhali usiamini hadithi za Abunuwasi! Wakazi wa Ukraine wa mashariki wanaongea mara Kirusi, mara Kiukraine. Walipiga kura mara kwa mara wanataka kuendelea kama raia wa Ukraine, pamoja na watu wa Donabas kabla hawajavamiwa na Putin.
Putin anatumia utamaduni wa watu kupika supu yake ya kisiasa.

Halafu hakuna haki kuvamia maeneo ya majirani ukisikia "sababu za kiusalama". Hii ilikuwa siasa miaka 200 iliyopita. Tangu 1945 viongozi wa madola wamepelekwa mahakamani wakivunja haki ya kimataifa (na kuwa wadhaifu ili waweze kukamatwa...) Tuone Putin ataendeleaje!
Nimeshaona nyie team NATO hamjui kitu.urusi Hana uhaba wa ardhi lakini hayo maeneo yamekuwa na shida na serikali ya Ukraine since siku ya Kwanza kuhamishiwa Ukraine kutoka urusi walikataa kuwa chini ya serikali ya Ukraine kwahiyo zelisky alipoingia madarakani akaanza kuwaua viongozi na watu wa hayo maeneo ya kirusi.kwa hiyo urusi akaamua kuingia kuwasaidia.Thank God maeneo yamesharudi urusi yakiwa salama .

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Utajuaje hayo?Unajua yanayoongewa chini ya Kapeti?
US Kwa miaka 6 amekuwa akijaribu kuishawishi Philippines Ili iweke base ya kijeshi huko lakini Rais aliyepita aliwasikiliza wananchi ambao walikuwa hawataki tension yoyote kati ya Philippines na China na badala yake wawe na ujirani mwema!
Rais huyu aliyeingia,amepuuza ya mtangulizi wake na ndani ya muda mfupi,a deal is made na tutaona US troops zikitua nanga Philippines!
Mkuu ujielemishe kidogo kuhusu maoni ya wananchi wa Ufilipino. Wengi wanaoa China kuwa hatari kutokana na matendo ya Chini katika bahari. China imeingia hapa katika ugomvi na majirani wote (Japani, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino, Indonesia) kwa kudai mamlaka juu ya visiwa vingi, na kupeleka manowari zake kutisha wavuvi na pia shughuli za kutafuta mafuta na gesi baharini.
Wanatenda huko kidogo kama Marekani ilivyofanya kenye Karibi na Amerika ya Kati katika miaka iliyopita.
Hapa Wafilipino wengi wanaona China hatari, na kuwepo kwa Marekani kama ulinzi .
 
Soma hapa tovuti ya Kifilipino:
Relations between the Philippines and China, which span several centuries, have been predominantly warm and cordial. But in recent years, both countries have experienced fiery issues that have resulted in their “cooling off,” hitting a low point since the establishment of their diplomatic relations in June 1975.


Philippines-China relations have lately been dominated by the territorial disputes in the West Philippine Sea, which has escalated since the naval standoff over the Scarborough Shoal in April 2012 and aggravated by issues of Chinese illegal occupation, unlawful establishment of infrastructures, and incidents of incursions and encroachment within the Philippines’ exclusive economic zone (EEZ). Bilateral ties took a downturn when the Philippine government filed an arbitration case against China under the United Na-tional Convention on the Law of the Sea (UNCLOS) in January 2013 challenging the legality of China’s nine-dash line claim over the contested waters.
 
Ongeza hii:
Recently, the Philippines has been rapidly improving its relations and cooperation with China on various issues, developing a stronger and stable ties with the country, as well as a successful Code of conduct with China and the rest of ASEAN. However, the average trust view of Filipinos towards China is negative 33, dipping much lower in certain provinces such as Zambales and Palawan where it is at least negative 45.[3][4][5][6] In contrast, the average trust view towards the United States is positive 66.[7]
 
Mkuu, tunaijua vema. Warusi walileta makombora ya kubeba mabomu ya nyuklia kisiwani. Hii ilikuwa tishio la kimakusudi. Marekani haikuandaa uvamizi, bali kuzuia meli zisifike tena Kuba na kutisha kubomoa vituo vya roketi kwa mashambulio kutoka hewani.

Hakuna aliyeleta makombora Ukraine. Ukraine kwa hiari yake iliwahi kuachane na silaha zake za nyuklia, na Urusi iliahidi kutunza na kutetea mipaka ya Ukraine daima. Urusi imeendelea kuvunja ahadi zake na mikataba yake tangu 2014.

Urusi iliamua kuvamia nchi jirani
a) kwa imani potovu kwamba ingekuwa kazi rahisi
b) bila kujali ahadi zake na haki.
Mmeshaambiwa na Angela Merkel kuwa Ukraine Ilikuwa inabuy time Ili kujijenga kijeshi!Hayo sijasema Mimi Bali chancellor wa Ujerumani(NATO member state),mpaka Ukraine kuwa number one army Ulaya nzima baada ya Urusi!Ndio maana Moja ya lengo la Russia ni demilitarization!
Mpaka Putin anaamua kufanya demilitarization maana yake amejua ukubwa wa jeshi la Ukraine!
Ukitaka kujua kuwa Urusi hakuichukulia poa hii vita basi ni namna ambavyo ameweza kuruka vihunzi vya sanctions!
Waliomtabiria kutishiwa silaha ndani ya Miezi 6 wanashangaa mzigo ndio kwanza unazidi kuchanganya!
 
Back
Top Bottom