Mimi nimekujibu uliposema kuivamia nchi nyingine kisa sababu za kiusalama ni mambo ya miaka 200 iliyopita!
Hao wananchi wa Donbas walipiga kura chini ya usimamizi wa nani?Kama unazikataa kura zilizopigwa chini ya Urusi,unawezaje kuzikubali zilizopigwa chini ya Regime ya Zelensky?
Issue ni kwamba,media za west zilifumbia macho mauaji alikuwa akifanya Zele huko Donbas!
Yaani huwezi kujua kamacwatu walikuwa wanauwawa lakini ukweli ndio Huo!
Sasa utaanzaje kuziamini hizo kura?
Mikataba ipo Kwa mazingira fulani,iwapo masharti ya mkataba yanakiukwa basi hata makubaliano yanaweza batilishwa!
Je,Unajua content ya mkataba walioingia?
Mkuu, yale mauaji unayodai Zelenski alifanya ni propaganda, tena ya duni kabisa.
Kwanza kabisa sehemu kubwa ya mapigano na vifo ilitokea wakati Zelenski hakuwa na nafasi yoyote Ukraine.
Wewe unashiriki kuendesha propaganda ile ambayo ni kijinga kweli kutumia jina lake mkijaribu kumwonyesha ndiye mtu anayemiliki vita hii mkijaribu kuunganisha chochote na jina lake. Hii unafanya bila kujali historia hata kidogo.
Tangu uvamizi wa Urusi katika Donbas 2014 kulikuwa na mstari wa mapigano katikati ya Donbas, askari na silaha tele pande zote mbili. Ilhali pande mbili ziliwahi kuahidi kutotumia silaha, tangu 2015 mapigano yalitokea mara kwa mara.
Ni dhahiri mara walianza Warusi, mara Waukraine. Katika hali ya kufyatuliana risasi juu ya mstari wa mpaka ule wa muda, watu waliathiriwa kila upande na kwa bahati mbaya wengine waliuawa. Pande zote mbili.
Urusi ilipiga propaganda "Waukraine wanaua watu wa Donbas" ilhali askari wao walitenda vilevile.
Jisomee hapa
Humanitarian situation during the war in Donbas - Wikipedia
makala inataja jinai pande zote mbili.
Taarifa ziko tele za watazamaji rasmi wa Umoja wa mataifa. Ona kwa mfano hapa taarifa ya tarehe 13 December 2017 ambako watazamaji wanatoa taarifa juu ya kupigwa na mizinga huko Popasna. Yaani Warusi walipiga kwa mizinga katika eneo lililoshikwa na Ukraine.
This report is for the media and the general public. On 13 December at 00:05, while at its forward patrol base on the northern edge of government-controlled Popasna (69km west of Luhansk), the SMM heard ten explosions assessed as outgoing artillery fire 200-500m west to west-north-west, and...
www.osce.org
Mi mfano tu, unaweza kuona taarifa zao siku kwa siku. Si propaganda, wanjitahidi kuwa neutral (hata katika mfano ninayoleta hawasemi Warusi wanavunja amani, wanatoa taarifa tu kwamba wanapigwa kwa mizinga ilhali wanakaa upande wa Ukraine..)