Kumbe Iran anapeleka shehena za silaha huko urusi eeh??
Basi tusisikie Tena zile ngonjera kwamba urusi anapigana peke yake na taifa linalosaidiwa na washirika kadhaa.., Russia Naye ana washirika kadhaa wanampa msaada,
Sent from my Infinix X660B using
JamiiForums mobile app
Raisi Putin alisema kwamba Russia bado haijaanza vita rasmi na ndo maana Wagner Group na wapiganaji wa Chechen watumika hadi sasa.
Pia Russia bado hajaanza kutumia silaha nzito hivyo huagiza silaha ambazo amewafundisha Iran na Korea Kaskazini kutengeneza.
Hivyo huagiza mizigo ili nae ajaribu ufanisi wake.
Kuna mahali humu nimesema kwamba Ukraine ni uwanja (theatre) ya majaribio ya silaha za aina zote na hata NATO/ USA wakisema watapeleka silaha Ukraine ni kwamba order zapelekwa viwandani na kisha kuletwa Ukraine kwa majaribio na matumizi.
Hili ni moja ya maeneo ambayo yana upigaji mkubwa sana (lucrative) na kuna watu wanatajirika kila kukicha kwa maana order zatumwa kwa kila aina ya kifaa cha kutumika Ukraine.
Ndo maana huwa nasisitiza kuangalia mgogoro huu kwa picha kubwa inohusu kila aina ya topic.
Lakini licha ya hivyo bado Russia aonekana apigana na mataifa 54 ambayo mengi hutengeneza silaha na vifaa kama mizinga kwa vibali.
Hiyo mizinga ya Leopard 2 baadhi ya nchi nyingi za Ulaya na NATO zatengeneza kwa kibali kutoka Ujerumani.
Ndege za kivita nyingi zatengenezwa Ufaransa na nchi zingine kwa order maalum. Ndo maana UK wamesema wao wana ujuzi wa kufundisha namna ya kuzitumia lakini wao wenyewe hawana ndege za F-16.
Uingereza wana ndege za aina ya Typhoon ambazo zitakuwa chakula kwa Russia kwani hizo huruka chinichini na si juu sana.
Hata hivyo hakuna ndege zinazopelekwa Ukraine kwani hiyo itakuwa ni "escalation".