Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nini kinaendeleq nyuma ya pazia?
Siku za nyuma west hasa US na UK walikuwa na assets mbalimbali zilizokuwa zinafanya surveillance, intelligence na recconaissance na kuwapa hizi taarifa jeshi la Ukraine ambapo kupitia hizi taarifa Ukraine alikuwa anajua mwenendo wa majeshi ya Russia hivyo kumpiga counter za hatari na kipindi flani Russia wakaoneķana kuachia baadhi ya maeneo.
Nakumbuka ndege na drones kama RC-135 Joint Rivet, Northrop Grumman RQ-48 Global Hawk na E-8 ambazo zilikuwa zinakaa anga la baadhi ya nchi za Nato na kukusanya taarifa zote muhimu kuhusu formation za warusi then wanampa hizi taarifa Ukraine. Jee hizi assets zimeondolewa maeneo husika na hazifanyi tena kazi ya kumsaidia Ukraine au nini kimetokea maana kipigo Ukraine anachopewa siku za karibuni ni kama mtu unayepigana ukiwa umefungwa ndani ya gunia huzioni ngumi za adui zinatokea upande gani ujikinge au urudishe mapigo.
Bila hata siraha kali sana kama hayo mavifaru anayoahidiwa kupewa, uwepo wa hizi ndege ulimsaidia pakubwa sana maana battlefield aliielewa na kumfanya kufanya mashambulizi yaliyoleta hasara sana kwa warusi.
Je hiki kinachoendelea tuamini Russia wamepata mwarobaini wa hizi ndege kama ilivokuwa kwa drone za mturuki, himmars na machuma mengine yaliyotumwa kumsaidia Ukraine. Kama ni hivo hizi ndege amedeal nazo vp?

NB; Mzee wa chip za kwenye dry cleaners kuwekwa kwenye vifaa vya kijeshi sihitaji jibu lako maana utaniingiza chaka
Uchambuzi mzuri sana huu,wewe umeona wasiyoyaona wengi.
Kwa kifupi Russia wakifanyiwa shambulio la usumbufu mkubwa na silaha ngeni,Huwa wanakaa na kuangalia wachomoe silaha Gani kutoka stoo itayoweza kuzima usumbufu huo,Huwa hawana jazba.
Wakitoka na maamuzi hua ni maamuzi ya kudumu.himerz, juveline na drone za mturuki ni mifano hai.
Sasa zimekua ni hadithi TU.
 
Kwa sasa kinachoendelea china ya PMC Wagner ni wanajeshi wa NATO kupigana wao kwa wao.

Wagner wanachokifanya ni kuwakamata wanajeshi walioupande wa Ukraine na kuwabatiza wanakuwa upande wa Russia.

Wanajeshi wa Urusi walipigana mwanzoni kupitia Chechen, lengo lao lilikuwa ni kupata mtaji wa wanajeshi. Sasa hivi wapo na mtaji wa mateka wengi sana. Na hao mateka kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wanajeshi wa Russia.

Kuna General mmoja wa USA aliyekuwa amezungukwa kule Mariupol, walijaribu kila namna ya kumuokoa walishindwa. Sijajua alipotelea wapi maana hata taarifa za kifo chake hatukusikia. Huenda kwa sasa ni mwanajeshi wa Urusi.
Maneno haya sijali kama ni ya kweli ama la,lakini yananifurahisha sana.
Kitu ambacho Nina uhakika nacho ni kua yanawakera baadhi ya wenzetu humu.
 
Gazeti la Ujerumani la BILD linaripoti kwamba ile Russia Offensive iliyokuwa inasubiriwa imeshaanza na inashika kasi.

Wanazidi kusema kwamba, mpango wa sasa wa hii Offensive ni kwenda ndani zaidi ya 200km kutoka kwenye mipaka ya Donbass na Luhansky.

Yaani wana maanisha kwamba Russia wanampango wa kuimega zaidi Ukraine kwenye hii Offensive.

Screenshot_20230214-231129_Telegram.jpg
 
NATO ndo wataskiliza kwa umakini mkubwa zaidi. Putin hatabiriki. Hawamwamini hawajui atasema Nini na kitaleta athari gani.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa,na kwa Sasa hapa duniani Putin ndio Rais anaefuatiliwa kwa karibu sana matendo na tabia zake.
Huyu anafuatiliwa kuliko yule kibabu wa USA .
 
Mkuu hii kitu inawezekan kbsa, mateka wa kijeshi wanaweza kutekwa na kupgiania upande waliotekaa?

Nalinafanywa kweli ?!
Kwa sasa kinachoendelea chini ya PMC Wagner ni wanajeshi wa NATO kupigana wao kwa wao.

Wagner wanachokifanya ni kuwakamata wanajeshi walioupande wa Ukraine na kuwabatiza wanakuwa upande wa Russia.

Wanajeshi wa Urusi walipigana mwanzoni kupitia Chechen, lengo lao lilikuwa ni kupata mtaji wa wanajeshi. Sasa hivi wapo na mtaji wa mateka wengi sana. Na hao mateka kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wanajeshi wa Russia.

Kuna General mmoja wa USA aliyekuwa amezungukwa kule Mariupol, walijaribu kila namna ya kumuokoa walishindwa. Sijajua alipotelea wapi maana hata taarifa za kifo chake hatukusikia. Huenda kwa sasa ni mwanajeshi wa Urusi.
 
Jamani ehh...
britanicca Yuko wapi siku hizi? Kipindi flani alikua akiishi Russia mjini Moscow. Ni yeye huyu aliyekulia akiona live maandamano ya warusi dhidi SMO.
NI Yeye aliyetwambia Hali ya kiuchumi Ni mbaya Sana nchini humo kiasi kwamba warusi wamekuwa wakipigania silesi ndogo TU ya mkate.
Asee britanicca Rudi bwana tumemisi elimu yako

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Mkuu kutetea uongo ni gharama sana.
Sio huyo TU aliekimbia,wapo wengi.
 
Ni kweli kabisa,na kwa Sasa hapa duniani Putin ndio Rais anaefuatiliwa kwa karibu sana matendo na tabia zake.
Huyu anafuatiliwa kuliko yule kibabu wa USA .
Huyo mwanadamu namuombea aendeleee kuwa hai kila leo.
  1. Vladimir putin
  2. Sergei lavrov
Hawa wanadamu wana pepo yao, ukiwasikiliza pindi wanapozungumza juu ya siasa za kimagharibi wanakuachia taathira kubwa sana.

Nafikiri watastaafu pamoja siasa na utawala pamoja na sergei shoigu.

Wote wameshagonga miaka 70.
 
Putin ana kimsemo chake,
Kama sijakosea anasemaga hivi,lengo lilikua kuikomboa Ukraine,lkni kajikuta anahitajika kuikomboa Dunia.
😀😀😀Sijui kama nimemnukuu sawa.
 
Kwa sasa kinachoendelea chini ya PMC Wagner ni wanajeshi wa NATO kupigana wao kwa wao.

Wagner wanachokifanya ni kuwakamata wanajeshi walioupande wa Ukraine na kuwabatiza wanakuwa upande wa Russia.

Wanajeshi wa Urusi walipigana mwanzoni kupitia Chechen, lengo lao lilikuwa ni kupata mtaji wa wanajeshi. Sasa hivi wapo na mtaji wa mateka wengi sana. Na hao mateka kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wanajeshi wa Russia.

Kuna General mmoja wa USA aliyekuwa amezungukwa kule Mariupol, walijaribu kila namna ya kumuokoa walishindwa. Sijajua alipotelea wapi maana hata taarifa za kifo chake hatukusikia. Huenda kwa sasa ni mwanajeshi wa Urusi.

Swali langu hawawezi kuwazunguka au kuwa shida kwa Russia??
 
Biashara imeisha .
Kama mtoa silaha na fedha kasema ,mtumiaji atabisha Nini?
Wataondoka mwezi march, unakumbuka ile habari ya kuanguka kwa mji wa soledar, iliwachukua wiki mbili ukraine kutangaza kuanguka kwa huo mji licha ya kwamba russia, wagner na hata wamagharibi walitangaza kuanguka mji huo mapema.

Lengo isionekane remote control ya ukraine ipo USA au ishu ya morali

huo ndio mtazamo wangu.

Hata ishu ya mariopol ilichukua muda kwa ukraine kutangaza kuanguka kwake
 
Back
Top Bottom