Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hivi hao US kweli Ni wazungu Kama wa Russia?
 
Elewa kwa west Ni Vita Ila kwa Russia Ni SMO au leo hajasema hayo maneno kwenye hotuba yake?
Kwa West ile ni msaada wa silaha. Kama anavyotoa misaada ya vyandarua na ARVs.

US haijafanya mobilization hapa. Urusi imefanya mobilization na inasema ni operation sasa ikitokea vita yenyewe itafanyaje kingine. Kabla ya 2022 mara ya mwisho Urusi kufanya mobilization ni 1941
 
Sidhani kama nadharia ndio hiyo unayojaribu kuiweka hapa!Sitaki kuamini kama service ya ndege vita za Russia inaenda kufanyika nchi za west!
Majuzi tu hapa Russia alisuspend baadhi ya deals za military equipment na baadhi ya nchi Kwa sababu ya mazingira ya vita aliyonayo! Priority ikawa ni kulihudumia jeshi la Russia!
So Kwa mtizamo wangu,service centers za Russia ziko busy kulihudumia jeshi lao hivyo kufanya mazingira ya service kuwa magumu!
Labda nipe uhusiano wa sanctions na service Kwa Russian made military fighter jets!
 
We unalinganisha msaada wa chandarua na leopard au abram hivi we unafikiria kwenye kichwa au kisigino?
 
Mtazamo wako ni mzuri sana na uko sahihi, ila mwaka jana mimi niliandika humu kwamba Russia itapoteza wateja wa silaha kutokana na sanctions Warusi wakabisha. Niliandika ilipoanza Egypt kusitisha, ikaja nchi nyingine sikumbuki kama ni Indonesia au nani jirani yake, ikaja India kwenye deal la helicopters mwaka jana huohuo, ikaja India Airforce kwenye fighters ikachukua Rafales ikaachana na additional Russian jets probably Sukhoi 30 MKI ilizonazo.

Hata January hii Indian Navy ilinunua Rafales kwa ajili ya carriers
Inazo Russian Mig 29K ila haikuzitaka. Na hapo kwa Serbia ulivyosema kama Russia inaanza vita (wanayoita operation) kisha wanashindwa kufanya services ya silaha walizouza kwa wateja basi hao hawako serious. Hutokaa usikie eti Marekani imeshindwa kufanyia service ndege za washirika kisa imevamia wapi sijui. Na hii vita sio ya kufanya nchi inayojigamba ina nguvu kushindwa service ya ndege za wateja, mbona air warfare ni ndogo.

India, China, Egypt ndio wateja wakubwa wa ndege za Russia na hawanunui uko tena. Algeria sijui
 
Mrusi aendelea kutengwa na Dunia - Mashindano ya Olympic kuyasikilizia kwenye redio...

Australia says it backs Olympics ban for Russian, Belarusian athletes​

Australia’s government says it is aligned with 34 other nations on the call for the International Olympic Committee (IOC) to ban Russian and Belarusian athletes from its competitions, despite not being marked as a signatory to the statement.
The British government issued the joint statement on Monday on behalf of “more than 30 like-minded nations”, which held a summit addressed by Ukraine President Volodymyr Zelenskyy this month.
 
Naona tumekubaliana sio issue ya sanctions Kwa nchi kama Serbia ambapo wamesema service imekuwa shida!Ndio maana nikashtuka nikahoji Iweje Russia atengeneze ndege vita halafu service ategemee nchi za west?
Nimesema Russia ilisuspend baadhi ya mikataba ya kibiashara ya silaha baada ya hii anayoiita SMO!Priority ikawa ni kulihudumia jeshi lake!Vivyo hivyo Kwa hata kwenye upande wa service,focus kubwa Iko kwenye jeshi la Urusi!
Umetolea mfano wa US,lakini nikukumbushe tu US amelazimika kuongeza production Ili asikaushe stock yake ya ammunition Kwa kuisupport Ukraine!Na hapo Bado ni mataifa zaidi ya 30 yanaisaidia silaha Ukraine lakini tayari Kuna mataifa yameshapata fatigue ya silaha!
Hebu tuambie,ni lini US ameshakutana na mazingira kama ya Russia Ili tuweze kulinganisha kama ulivyotoa mfano!Yaani US aende vitani bila mshirika,halafu akutane na upinzani wa mataifa 30 yenye uchumi mkubwa yakimsaidia adui yake silaha, intelligence na fedha kuendesha serikali wakati wa vita?
Ni wapi ambapo US amepambana vita akiwa na vikwazo vya kiuchumi kutoka Kwa mataifa zaidi ya 30 kama ambavyo Russia anafanyiwa Ili uwanja uwe sawa?
Yaani unafananisha ya US kwenda na washirika wake Iraq na Afghan na hii ya Russia vs Ukraine?
Kiukweli vigezo na masharti havijazingatiwa kwenye ulinganyo wako!
 
Ha ha ha haa,da !
Hili ni bonge la mkwara aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…