Mkuu sidhani yeyote anategemea Putin atimize matakwa ya wengine. Ila wengi wanataka aheshimu ahadi na mikataba ya nchi yake, kama vile huheshimu na kulinda uzima wa mipaka ya Ukraine (mkataba wa 1994) na mikataba ya Helsinki na mikataba na ahadi kuhusu kuheshimu na kutunza haki ya kimataifa.
Mimi siamini katika innocence ya West, west wako very cunning kuliko tunavowaona..wana-agenda zao za chini kwa chini nyingi sana....Mikataba wanayosaini mingi inakuwa kwenye kuwafavour kiasi fulani...Deep state ya west inafanyakazi nje ya haya maneno wanasiasa wao wanaongea..
1.Angalia mfano wa hilo bomba lililolipuliwa NORD STREAM...angelikua kafanya Urusi..makelele yangekuwa kama yote...sasa kafanya US akishirikiana na Norway na wanajua kabisa..wako kimya (Unafiki huu)
2.Minsk 2 Agreements: Wote wamekiri kabisa walikua wanavuta subira..hawakua kwenye mpango wa kutekeleza.
3.Uongo wa US kuishambulia Iraq 2003..(Huwezi ukasikia West wanasema chochote
4.Jana Putin kasema kabisa walikua na taarifa zote za kiinteligensia kuwa Ukraine wanajiandaa..watashambulia Donbass na baadae wataenda hadi Crimea...mpango huu walikuwa wanapewa taarifa etc na kila kitu ba West.
5.Donbass..imetandikwa mabomu tangu mwaka 2014....watu wameuliwa kule kisa hawataki kuwa ndani ya Ukraine sababu ya Uhaini wa kumpindua kiongozi aliyechaguliwa kwa kura kabisa..haijalishi ni mrengo wa Urusi..(2010)
6.Nato kwa nini wanatengeneza mazingira ya nchi kujiunga nazo...(Military blocks huwa zinaelekea kwenye vita tu)..yaani mfano leo Tz, Kenya, Rwanda tutengeneze military alliance, kitakachofuata nchi nyingine nazo zitaanza kuunda alliance zao kulingana na ideology au urafiki...(Refer WWI & 2)
7 NATO waliitandika Yugoslavia..kosovo ikatoka na wakassupport...leo kwa nini hawataki Donbas wajitenge??Kwa nini wasiseme waitishe kura ya wazi chini ya UN..watu waamue kwa uwazi...??
8.Ulimwenguni vita au machafuko yako kila sehemu..angalia mfano Afrika:Afrika ya Kati, Somalia, DRC..watu wanakufa kila siku..mbona hatuoni nguvu iliyotumika UKRAINE kutumika kwenye hizi nchi nyingine au Kisa ni Ulaya na Russia yuko involved????(Unafiki tu)
9.Kwa nini wasiitie moyo Ukraine kuwa ikawa na sera zake zenyewe kuliko kuichochea kuchukua upande??
10.Wakati wa Obama: CIA waliingilia mazungumzo ya Markel-Councillor wa Ujerumani-mshirika wao namba moja Ulaya.ni colony lao tu....Hiyo scandal angekuwa kafanya Russia ungesikia makelele yake...
Hao west sio wazuri kama mnavolazimisha wawe, na hata Russia naye sio mzuri pia..lakini kwa hili la unafiki wa West dhidi ya nchi nyingine (Russia CASE study)..ni vizuri West wafundishwe adabu...na mtu pekee wa kufanya hivyo ni Putin kwa sasa..
Viva Putin
Sent from my SM-A205F using
JamiiForums mobile app