Nje kidogo ya mada. Kwanini uliamua kutumia T14 Armata kama ID yako ya JF mkuu?
Napenda kufuatilia silaha kuliko vita yenyewe. That time najiunga JF nilikuwa nasoma sana silaha za Urusi kuliko wengine, tangu mwaka jana nafuatilia silaha za China zaidi. Nilikuwa na imani hiyo MBT itakuwa tishio kulingana na data zilizokuwepo kwamba inatakiwa iweje. Na report ya wizara ilisema vifaru vitakuwa accepted 2020 kama sikosei.
Pia naipenda Russia na tamaduni zao, nimehudhuria matamasha yao pale Russian Culture Centre
Nimesoma waandishi wao kina Fyodor Dostoevsky na Leon Torstoy. Watu wao maarufu na wenye tuzo kama kina Mikoyan, Molotov, Pavel Sukhoi. Nimetazama movie kama Anna ambazo plot ni Soviet Union, movie zao sio nzuri sana na actors wao wanafanania na anachofanya Steven Seagal mzaliwa wao.
Nimeisoma historia ya Russian empire kuanzia ikiwa Rus, wakaja kina Ivan The Terrible, Czars kama Catherine the Great na Alexander, Bolsheviks, USSR mpaka the making of modern Russia.
Watu wengi wa karibu yangu wanadhani mimi ni pro Russia mkubwa ila ukweli sio shabiki wa sera na mwenendo wa Putin na serikali yake. Kutoipenda serikali iliyopo madarakani na vitendo vyake haimaanishi huipendi hiyo nchi, in fact Putin atakufa na Russia itabaki kwahiyo anayempenda Putin anaweza ishia hapo. Na kuipenda nchi sio unakubali kila inachofanya.
Hivyo naipenda T-14 Armata, naipenda Russia, napenda silaha ila sipendi kulazimisha vita sababu naamini kitu muhimu the military can do is to avoid war (deterrence). Kuwa na jeshi kubwa kiasi adui asiwaze hata kukuvamia ila usiwe na jeshi kubwa kuonea wengine, ukiwa na jeshi dhaifu ndio yale ya Rwanda kuichokoza DRC na ukubwa wake. Ikitokea kuna ulazima wa vita basi pigana kwa utu kufuata Geneva convention kama human rights, haki za POWs, n.k