Kama mwakumbuka, nilisema hapo awali kwamba US na NATO watatengeneza tukio ambalo litapekelea kuhitaji Ukraine kupewa ndege za kivita za F-16.
Marekani kuna sintofahamu kwa wananchi kwamba hawakubali kuunga mkono moja kwa moja vita na Russia.
Hiyo AUV ya Marekani ilikuwa ikiruka umbali wa maili 6000 kutokea kituo cha kijeshi cha NATO na US na ilikuwa ikiruka umbali wa maili 75 kutoka kisiwa cha Crimea. Pia Marekani hawajakataa kwamba kifaa cha mawasiliano kwenye hiyo AUV yaani "transponder" kilizimwa.
Ukizima "transponder" wamaanisha kwamba katika ujasusi wa kuchungua eneo la adui yaani surveiilance hutataka kujulikana wataka kuchukua picha za eneo la adui kugundua amejipanga vipi, vifaa vyake vya kijeshi na masuala mengine mazito.
Na kwa kuwa Russia waliona AUV hiyo yajongelea anga lake pale Crimea kama taifa lililo vitani Russia hawakuwa na jinsi bali ni kuidungua hiyo AUV.
Ili kuweza kufanya mashambulizi ya kimkakati dhidi ya Russia yanoitwa "Spring Offensive" Ukraine wahitaji sana hizo picha za satelite na za "Surveillance" kuweza kuwa na mashambulizi yenye kutoa ipnact kubwa.
Mida hii yaelezwa kwamba kuna maseneta wapenda vita tayari wazoza kuhusu kutuma ndege za F-16 jambo linoashiria kwamba sasa Marekani na washirika wake wapo tayari kwa vita kamili ya angani na Russia lakini bila kutuma vikosi vya ardhini nchini Ukraine kama walivyokubaliana na Russia.