Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu mbona unaamini propaganda bila kuuliza kama ni kweli? Je una mfano 1 kuhusu watoto chini ya miaka 18 katika jeshi la Ukraine? Sidhani.
Propaganda hii inasimama kwenye video moja Facebook. Inaonyesha wafuatao na kudai ni watoto:

View attachment 2554277
Wa kwanza anaitwa Elizabeth, ni dereva wa ambulance akiwa na umri wa miaka 23, si 14. Wanahabari walimhoji pia wazazi wake waliosema binti amemaliza digrii mbili akajitolea jeshini wakati Putin aliposhambilia.

Huyu mwingine anaitwa Andrea Sidis. Aliwaambia wanahabri kwamba alikuwa na miaka 25 alipopost video yake iliyotuiwa katika facebook ya Kirusi. Naye alijitolea kwa huduma ya kijeshi.

propaganda ni sanaa naufundi. Wako wanaoweza, wengine wanashindwa. Ila hata wanaoshindwa wanaweza kupata waamini.

Kijana mwenye miaka 25 afanane na mtu mwenye sura ya under 18?

Aache cheap propaganda
 
Mkuu natambua kuwa wewe huna ushabiki uliopitiliza. Uhalisia wa jambo hili ni kuwa Putin aliwadharau sana wa Ukraine na ndio maana akaita ni operation lakini akakutana na nguvu ambazo hakutarajia, leo tupo mwaka wa pili hivyo huwezi kuita operation tena. Ila nasema muda utaongea.
Hivi ni mwaka wa pili? Ilianza lini hii SMO?
 
Wakipata mabaki ya droni, italeta faida gani kwa nani?
Kwa urusi ni faida
Manake baada ya hapo watachukua box yake maalumu inayochukua taarifa ambapo taarifa ni nguvu kwako dhidi ya adui yako

Pia inawasaidia kuichunguza asili yake ili wajue madhaifu yake na dawa yake hapo wanaixhunguza technology yake
 
Wakati mnaimba mapambio Asadi must go, alikuwa hajachaguliwa na wanachi wa syria ktkt uchaguzi huru?
Uchaguzi huru?? Syria ?? 😀 Je unajua punje tu ya historia ya Syria? Tangu Assad Mzee alimpindua dikteta aliyemtagulia katika miaka ya 1970 Syria haikuona chochote kinachofanana na uchguzi. Assad kijana alirithi tu udikteta akafaulu kuiendeleza.
 
Kwa urusi ni faida
Manake baada ya hapo watachukua box yake maalumu inayochukua taarifa ambapo taarifa ni nguvu kwako dhidi ya adui yako

Pia inawasaidia kuichunguza asili yake ili wajue madhaifu yake na dawa yake hapo wanaixhunguza technology yake
Picha yako ya dron ni ya zamani kidogo . . . Nafikiri hata droni za Urusi hazitunzi data kwenye boksi hadi kurudi bali kuzirusha online . . . .
 
Naona tutakesha hapa tukibishana kwa vitu ambavyo ni so obvious - kama huwezi kutofautisha kati Dummy missiles na virokeri vya DIY (backyard) vinavyo undwa na wapalestina na waasi wa Yemeni basi tena.

Labda nikusaidie kitu kimoja hapa, hatuzungumzii swarms of home made rockets au vi-drones vyenye lengo la ku-overwhelm ADS kutokana na wingi wake - tunacho zungumzia hapa ni missile inayonekana kwa sura na kwenye rada kama ni real one lakini inside imewekewa systems za kielectronic kwa lengo la kunasa vital information kuhusu mifumo ya ADS za Ujerumani na USA, taarifa hizo zinanaswa in real time wakati German or USA rada zinapo jaribu kumulika Dummy missiles za Urusi kwa lengo la kizitungua, kumbe zinatumwa kama chambo cha kurecord vital spec zote za ADS na zinatumwa in real time kwa real missiles ambazo ziko armed kwa mashambilizi ya kulipua hizo ADS za Ukraine, real missiles zinakuwa nyuma ya Dummy missile kwa dakika au sekunfe chache zinakuja ziko well armed kwa vilipuzi vile vile na uwezo wa electronic wenye lengo la kujam system nzima including radar kwa kutimia taarifa zilizo kuwa uploaded kutoka kweye Dummy kabla ndio maana watu walio shuhudia matukio hayo wanasema ADS za Ujerumani na US zilionekana kama a sitting duck wakati zikishambuliwa na missiles za Urusi.

The crux of the matter here is: Warusi waliwazidi kete NATO/US kwa kutumia dummy missiles kwanza ili ku-fool air defense system za Ukraine halafu baada ya muda mfupi kitu kizito kinafuata kwenye nyayo zilizotengenezwa na Dummy missiles kwanza, a very clevel stuff - Warusi kitu ingine nawambieni kila siku.
Sidhani kile unachoongelea kipo. Kwanza fumo wa IRIS-T bado iko Kyiv (Ujerumani ilituma mifumo 2 pekee, baadaye ya tatu) na kama kile unachodai kingekuwepo, IRIS-T ingeharibika tayari. Kinyume inafanya kazi vizuri tangu nusu mwaka, haikupigwa hata kidogo kwa sababu inaangusha kila kombora linalokuja.
Zukiangalia taarifa kuhusu "dummy missiles" - ona hapa taarifa ya gazeti la Misri:

Wanarusha roketi zinazoweza kubeba silaha za nyuklia lakini bila bomu; roketi hizi zinatakiwa kuchosha ADS za Ukraine adi wimbi la pili linapita na kusababisha uharibifu.
Ukiona kuna mengine, taja jina na model ya roketi bandia na zile zinazofuata unazowaza kuwa na uwezo huo wa ajabu.
Karibu sana! (lakini usijaribu kudai eti yote ni siri kubwa!!!)
 
Una nafsi dhaifu Sana...anyway nilitaka nikutukane nikagundua sitakua na tofauti na wewe.
Mkuu umetenda jambo jema, mambo ya kutukanana sio utamaduni wetu sisi wa TZ. Hili ni javi la kuelimishana. Hakuna anaye jua yote ila ni MUNGU TU. Ahsante
Hahahahahah muda utaongea maana kila mtu anataka atest kuzikaanga silaha za NATO 🤣🤣🤣 bado kiduku na mchina hawajapeleka zana zao 😀
Mkuu Mchina na Iran mbona wamepeleka sample zao, ila kiduku sijamfuatilia! Mkuu nadhani unajuwa Ukreine alikua Urusi iliyosambaratika hivyo vifaa vya Putin vipo wazi ndio maana operation itachukua muda mrefu
 
Sidhani kile unachoongelea kipo. Kwanza fumo wa IRIS-T bado iko Kyiv (Ujerumani ilituma mifumo 2 pekee, baadaye ya tatu) na kama kile unachodai kingekuwepo, IRIS-T ingeharibika tayari. Kinyume inafanya kazi vizuri tangu nusu mwaka, haikupigwa hata kidogo kwa sababu inaangusha kila kombora linalokuja.
Zukiangalia taarifa kuhusu "dummy missiles" - ona hapa taarifa ya gazeti la Misri:

Wanarusha roketi zinazoweza kubeba silaha za nyuklia lakini bila bomu; roketi hizi zinatakiwa kuchosha ADS za Ukraine adi wimbi la pili linapita na kusababisha uharibifu.
Ukiona kuna mengine, taja jina na model ya roketi bandia na zile zinazofuata unazowaza kuwa na uwezo huo wa ajabu.
Karibu sana! (lakini usijaribu kudai eti yote ni siri kubwa!!!)
Ndio maana nimesema tutakesha kwa kuwa ni wazi background zetu zaku analyse masuala haya ya kiufindi au teseme sayansi na tekinolojia ni tofauti kabisa!!
 
Mkuu ukweli ni kwamba Putin alikuwa anamtamani Ukraine sasa, hivyo sio kwamba Putin anapigana kishikaji, amejizatiti kabisa aitwae Ukraine, lakini hakujua kwamba naye ana rafiki ambao watamsaidia. Kama uliona day 1 alivyoingia kwa mbwembwe akisindikizwa na vifaru kibao lakini vifaru viliishia kuangamizwa kwa kipigo cha mbwa koko.
Ndugu..

Kama unaongelea vifaru vya ule msafara wa Km.60 ,ulifika nje ya mji wa Kyiv, ukakaa kwa siku kadhaa kisha Ukaamriwa urudi kuelekea Belareus, baada ya hapo yakaendelea mapambano Donbas..

Kimsingi ule msafara ulikuwa ni wa kuwatisha tu Ukrane, kwani lengo la urusi ni Donbas tu hana shida na nchi nzima ya Ukrane..

Hata ukisikia wameshambulia Kyiv wanapiga zile bases za majeshi ya ukrane, au maeneo muhimu yanayosaidi front kule Donbas..
 
Mkuu je uliishi sayari tofauti? Msafara wa kutisha tu kidogo? Ulirudi na kwenda Donbas??

Ule msafara ulikuwa na wanajeshi waliobeba sare zao za paredi (walikamatwa pamoja na sare hizo) kwa sababu walitegemea kumaliza haraka wakihitaji sare nzuri kwa paredi ya ushindi Kyiv.

Msafara haukurudi Belarus, ni mabaki kadhaa. Sehemu kubwa iliharibika. Ukraine walikamata vifaru 400 - 500 (ona takwimu ya vifaru vya Ukraine - wangepata wapi T-72 nyingi tangu Februari 2922 ?). Waliweza kukamata vifaru vingi hivi kwa sababu askari Warusi waliviacha njiani na shambani - maana vilipelekwa huko bila mafuta ya kutosha.
 
Back
Top Bottom