Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kijana mwenye miaka 25 afanane na mtu mwenye sura ya under 18?

Aache cheap propaganda
 
Hivi ni mwaka wa pili? Ilianza lini hii SMO?
 
Wakipata mabaki ya droni, italeta faida gani kwa nani?
Kwa urusi ni faida
Manake baada ya hapo watachukua box yake maalumu inayochukua taarifa ambapo taarifa ni nguvu kwako dhidi ya adui yako

Pia inawasaidia kuichunguza asili yake ili wajue madhaifu yake na dawa yake hapo wanaixhunguza technology yake
 
Wakati mnaimba mapambio Asadi must go, alikuwa hajachaguliwa na wanachi wa syria ktkt uchaguzi huru?
Uchaguzi huru?? Syria ?? 😀 Je unajua punje tu ya historia ya Syria? Tangu Assad Mzee alimpindua dikteta aliyemtagulia katika miaka ya 1970 Syria haikuona chochote kinachofanana na uchguzi. Assad kijana alirithi tu udikteta akafaulu kuiendeleza.
 
Kwa urusi ni faida
Manake baada ya hapo watachukua box yake maalumu inayochukua taarifa ambapo taarifa ni nguvu kwako dhidi ya adui yako

Pia inawasaidia kuichunguza asili yake ili wajue madhaifu yake na dawa yake hapo wanaixhunguza technology yake
Picha yako ya dron ni ya zamani kidogo . . . Nafikiri hata droni za Urusi hazitunzi data kwenye boksi hadi kurudi bali kuzirusha online . . . .
 
Sidhani kile unachoongelea kipo. Kwanza fumo wa IRIS-T bado iko Kyiv (Ujerumani ilituma mifumo 2 pekee, baadaye ya tatu) na kama kile unachodai kingekuwepo, IRIS-T ingeharibika tayari. Kinyume inafanya kazi vizuri tangu nusu mwaka, haikupigwa hata kidogo kwa sababu inaangusha kila kombora linalokuja.
Zukiangalia taarifa kuhusu "dummy missiles" - ona hapa taarifa ya gazeti la Misri:

Wanarusha roketi zinazoweza kubeba silaha za nyuklia lakini bila bomu; roketi hizi zinatakiwa kuchosha ADS za Ukraine adi wimbi la pili linapita na kusababisha uharibifu.
Ukiona kuna mengine, taja jina na model ya roketi bandia na zile zinazofuata unazowaza kuwa na uwezo huo wa ajabu.
Karibu sana! (lakini usijaribu kudai eti yote ni siri kubwa!!!)
 
Una nafsi dhaifu Sana...anyway nilitaka nikutukane nikagundua sitakua na tofauti na wewe.
Mkuu umetenda jambo jema, mambo ya kutukanana sio utamaduni wetu sisi wa TZ. Hili ni javi la kuelimishana. Hakuna anaye jua yote ila ni MUNGU TU. Ahsante
Hahahahahah muda utaongea maana kila mtu anataka atest kuzikaanga silaha za NATO 🤣🤣🤣 bado kiduku na mchina hawajapeleka zana zao 😀
Mkuu Mchina na Iran mbona wamepeleka sample zao, ila kiduku sijamfuatilia! Mkuu nadhani unajuwa Ukreine alikua Urusi iliyosambaratika hivyo vifaa vya Putin vipo wazi ndio maana operation itachukua muda mrefu
 
Ndio maana nimesema tutakesha kwa kuwa ni wazi background zetu zaku analyse masuala haya ya kiufindi au teseme sayansi na tekinolojia ni tofauti kabisa!!
 
Ndugu..

Kama unaongelea vifaru vya ule msafara wa Km.60 ,ulifika nje ya mji wa Kyiv, ukakaa kwa siku kadhaa kisha Ukaamriwa urudi kuelekea Belareus, baada ya hapo yakaendelea mapambano Donbas..

Kimsingi ule msafara ulikuwa ni wa kuwatisha tu Ukrane, kwani lengo la urusi ni Donbas tu hana shida na nchi nzima ya Ukrane..

Hata ukisikia wameshambulia Kyiv wanapiga zile bases za majeshi ya ukrane, au maeneo muhimu yanayosaidi front kule Donbas..
 
Mkuu je uliishi sayari tofauti? Msafara wa kutisha tu kidogo? Ulirudi na kwenda Donbas??

Ule msafara ulikuwa na wanajeshi waliobeba sare zao za paredi (walikamatwa pamoja na sare hizo) kwa sababu walitegemea kumaliza haraka wakihitaji sare nzuri kwa paredi ya ushindi Kyiv.

Msafara haukurudi Belarus, ni mabaki kadhaa. Sehemu kubwa iliharibika. Ukraine walikamata vifaru 400 - 500 (ona takwimu ya vifaru vya Ukraine - wangepata wapi T-72 nyingi tangu Februari 2922 ?). Waliweza kukamata vifaru vingi hivi kwa sababu askari Warusi waliviacha njiani na shambani - maana vilipelekwa huko bila mafuta ya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…