Umenena Vema mkuu, hawa US sijawahi kuwaamini kwenye kitu chochote. Acha PUT IN awaadabishe, mdogomdogo wataelewa.
Hah haa 😄
Karibu tena Rafiki siku nyingi sijaona nondo zako hpa jamvini
Shukran bro!
Hizi mambo hazitokei bahati mbaya mdogo wangu.
View attachment 2560933
Hiyo ndio Africa yetu, so hawa vijana usiwashangae saaaaaana.
Video Credit kwa
howardlite
Duh ni hatari 🤔
Kingine kuna jambo naona kaliongelea bro
Champagnee na
Labani og hapo juu kuhusu hali inavyoendelea kwa sasa na mie wacha niongezee maneno mahsusi kwa wale tulio na "macho ya kufanana" tusuuze akili.
Hali ilivyokua mwanzo (Under US Hegemony)
Nianze kwa kutoa short intro ya baadhi ya yaliyokuepo ama kutokea mwanzoni mwa miaka 1900+(Karne ya 20). Na maelezo yangu yatajikita kwenye hizi "currencies" katika kuzielezea zina maana gani kwenye Ulimwengu huu tulio nao.
Kikawaida, thamani ya pesa yoyote inategemea na Assets zinazomilikiwa na Nchi husika yenye hiyo pesa. Mwanzoni mwa karne ya 20 tulikua na Pound as global currency sio US dollar hii inayotizamwa sasa.
Baada ya vita ya kwanza ya Dunia, ambapo US haikupiganwa kwao walipokea reserves ya dhahabu nyingi tu kutoka Europe vita ilikokua ikipiganwa na hapa ndio taratibu US dollar ikaanza kui'replace Pound as a currency of Global trade.
Mwaka 1944 US akaingia makubaliano yanafahamika kama "Bretton Woods Agreement" ikihamasisha bilateral trade baina ya nchi zifanyike kwa US dollars. Miaka 26 baadae haya makubaliano yakawa nullfied baada ya London Gold Pool kua dissolved.
Ikiwa unaendelea kufatilia maelezo haya kwa hapo hapo jiulize kwanini US anaingia makubaliano ya kutaka biashara katika nchi na nchi zifanyike kwa pesa yake na sio pesa za nchi husika. Nini alichokua anakitafuta? Kila mtu ana majibu yake hapo.
Ok twendelee...
Baada ya mkasa huo, US dollar ni kama vile iliyumba na Asian economies ukaanza kukua kwa mara nyingine. Mwaka mmoja baadae, I mean 1971, aliyekua rais wa US wa kipindi hicho... Nixon, akaondoa convertibility ya US dollar kwa gold maana ake dollar ikawa de-linked kutoka kwenye asset za nchi hiyo ni currency hiyo rasmi value ake kuwa determined na global demand. Na ndio mwanzo ama ujio wa Petro dollar ukaanza.
So demand ya dollar ikabustiwa kwa mapana na hii tunayoita petro dollar. Sasa ili kukidhi hiyo demand US akawa anafanya kuprint pesa zaidi na zaidi ili ku'maintain certain values. Hapa nitoe mfano wa demand na supply. Ni kama mzani ili usiegemee upande m1 yapasa upande mmoja ukiongezeka basi ujazie na upande mwingine otherwise inalala upande mmoja en vice versa is true. So as demand ilipokua inazidi ndivyo US alivyozidi kuziprint hizo karatasi zake na kuzikopesha kwa mataifa kadha wa kadha duniani kupitia IMF na World Bank (Taasisi za mchongo hizi 😂). I bet ndio maana wajuvi wa mambo huuona ule uchumi wa taifa lile ni uchumi wa mchongo vile vile.
So mwishoni mwa miaka ya 90+ karibu 90% ya biashara za kimataifa (Global trade) zilikua zikifanyika kwa US dollars huku US akiziprint za kutosha ku-cover hiyo demand.
Sasa tuje yaliyopo leo hii (A road to Multipolar world)
US ana gold reserves worth about $500bn, ilhali tayari ame issued hard currency zenye thaman kama ya $4trillion huku akiwa na taifa likiwa na treasurery bond (Mideni) ya takriban $38trillions. Yani hii ni kama 80 times ya Gold reserves alizo nazo US.
Sasa mahusiano ya Currency ya US na Vita yake dhidi ya Russia nyuma ya pazia yakoje?
Turudi nyuma kidogo.
Mwaka 2014, baada ya Russia kuichukua Crimean peninsular kutoka Ukraine, US ali impose economic restrictions kwa Russia na huu ndio ulikua mwanzo wa hii tunaita "De-dollarization"... Nchi nyingi zikaanza kufanya kile tunachokiona leo kwa speed ya aina ake.
Uanzishwaji wa Euro mnamo mwaka 1999 pia ulikua ni moja ya vitu ambavyo vimesababisha kuvunjika kwa monopoly ya US dollar. So mkiona kwanini hata EU wanasota ijapokua ni marafiki wa US tafuta popcorn kaa pale utulie uienjoy show. Wale wehu linapokuja swala linalogusa interest zao huwa hawana rafiki wala adui.
Wapo wanao ona namna Ukraine alivyokua na anavyotumika kuiharibu Europe na Russia kwa pa1 ndio hao kila kukicha wanaingia barabaran kuandamana hapo Ulaya but no one give a f... Hakuna anayewasikiliza oh labda ni demo la "krasia" pia, who knows mmh?
Hapa ukiangalia stats ndani ya miaka mi8 iliyopita nchi nyingi duniani zimekua zikiingia bilateral agreement kama hii yetu tuliyofanya karibuni na India ili yasiwakute kama yaliowakuta Russia. So hii imezidi kuichochea dolari kwenye mteremko share yake kwenye global trade ikipungua na sasa ipo around 57% hv kwa data za 2021. Hapo ikiwa ni poromoko kutoka 71% tangu kuanzishwa kwa Euro 1999 na yakadiriwa within miaka 2-3 ijayo may decline further to 40-45%.
Naweza nikasema toka 37th Prezdaa wa US afanye ku de-link US dollar from national asset held by his government na kuiweka katika ulinganyo wa demand sokoni alitengeneza spot ambayo ilihitajia nyakati mahsusi kama sasa kuwadhibiti uhuni wao.
Wapo waliotangulia kutaka kuutoa huo utumwa ila waliambulia kuuwawa na kupinduliwa kwenye nchi zao. Notable katika wao akiwa ni Muammar Gadafi aliyetaka Afrika turudi kutrade rasilimali zetu kwa dhahabu.
What we can say ni kua, a journey to multipolar powers, to multipolar world have been started. Gari lishawaka, Speed kubwa af brake zimekata, there is no going back. TUTAHESHIMIANA tu 😂😂😂.
Some idiots wanadai haiwezekani, ila kwa waerevu wanajua yalikotoka na yanakoelekea haya mambo.