Ujue bora ukose Pesa, unaweza pata wasamalia wema wakakupatia. Ila mtu akikosa akili kisha akajikuta mjuaji siku zote huwa anaachwa na Upumbavu wake.
Nasoma zangu hapa comments nimeiona hiyo binafsi nimecheka sana, but kicheko cha masikitiko. That's why kila mda huwa nasema hawa wenzetu wana namna yao ya kufikiri ambayo haifanan na yetu. I mean wapo kwenye dunia yao full of illusions!
Finland weka mbali silaha iwe mshale, ama mkuki. Ni nchi yenye Idadi ya watu wachache kuliko Mkoa wa Dar es Salaam hapa Tanzania. Finland ina idadi ya watu takriban Mil 5.47
Hapo tumesema Idadi ya watu, So ni Jumla ya Wazee Vijana na watoto kwa pamoja. Ila kwa upande wa Russia tusizungumzie Idadi ya watu bali Total reserves ya wanaoweza kupigana endapo ikitangazwa Vita. Ni zaidi ya Mil 25.
Number hazidanganyi msemo wa
lee van cliff
Idadi ya wapiganaji tu waliopo Russia ni almost five times ya Idadi yote ya watu waliopo Finland including Vijizee, Vijana hadi Vitoto. Bila hata kutumia Silaha ima bunduki wala mishale, kwamba wazichape ulingoni kama Mwakinyo na Mandonga bila kupepesa jicho ushajua nini kitajiri.
Population vs Fighters, 1 to 5 af bado kuna mtu anawaza mtoto wa miaka miwil, Mzee wa miaka 90, mama mwenye kijusi, wagonjwa, walemavu ambao ni katika wanaochangia idadi hiyo ya watu watamudu pambano la wapiganaji wa 5 kwa kila mmoja.
Kwamba kuna toto moja baada ya kuvuta alichovuta sijui ndio niseme milango iko wazi hawezi bana pumzi ikabaki mwilini kuleta afya ya akili anakurupuka anakuja sema eti "Russia bila Nukes" Finland pekee tu anam-mudu. Hivi wanawaza kwa kutumia nini ndugu zetu hawa?
Ok kama wana mmudu wamekimbilia NATO kufanya nn? Nukes? Ndani ya Europe zipo France na UK. Tena kwa idadi kisoda watazifanyia nini ndani ya huo Muungano? Kama France mwenyewe, Germany, UK, Poland... top dog hapo EU wanaogopa kukutana ana kwa ana na Russia. Finland atafanya nn?
Russia anatengeneza silaha zake mwenyewe, almost nchi zote EU ama ndani ya NATO ukizitoa zile top zinategemea silaha kwa manunuzi kutoka kwa shangazi yao US. Watafanya nini?
The farthest distance kutoka Russia ndani ya Europe ni UK, ambapo Russia anaweza fikisha madhara ndani ya dk 3-4 ukitokea Kaliningrad. Je hawa waliopo kikwapani watafanywa nini?
Mahaba ya upande flan kwa kila mtu yapo ila this is too much 😏, sijui ndio kuishiwa hoja comments nyingi kutoka kwao zimekua kama mipasho isiyo na uhalisia. Ni kutype ilimradi kiumbe kime'type.
Unajionaje mchambuzi kama Unashindwa tofautisha Politics vs Reality.
Matumizi mabaya ya mwili yanaharibu sana akili. Vijana wenzetu em acheni hizo mambo muweze kubana pumzi ubongo upate hewa ufanye kazi kwa ufasaha. Mnaboa sio siri nyie wazee!