Bahati mbaya kwenye hii vita Sina upande, hivi ni vita vya mabeberu ,Mrusi anazuia ukoloni wa Marekani na Marekani anataka kuitawala ulaya yote na kikwazo kilochobaki ni Mrusi. Na huu ni mkakati wa muda mrefu. Ndo maama Marekani hataki wakae mezani wayamalize.anataka amzofishe Mrusi mdogomdogo. Na Mrusi nae kameshituka ndo maama hatumii Sana jeshi na nguvu nyingi baada ya kupata hasara mwanzoni anatumia Wegner anchofanya ni ku clear mwishoni. Mimi nawashauri tuache ushabiki tufutilie matukio Kwa kina bila upendeleo. Kila nchi Ina faida na hsara Kwa afrika. Wote wapo kwaajili ya maslahi Yao.
Nachukua nafasi hii kukufahamisha kua Mimi Niko upande wa Russia katika SMO hii,pia nachukua nafasi hii kukufahamisha kua Mimi na Pro Russia wote humu hatushabikii vita na Wala hatupendi vita kabisa maishani mwetu,isipokua tuna penda haki na kuchukia uonevu wa mabeberu,amabo Mkuu wao ni USA.
Iko hivi,kwa Nini tumechukua kua upande wa Urusi,sababu ni kwamba tumeona kua Urusi ndio iliyochokozwa.
Naamini unaweza kua na upeo mkubwa zaidi yangu ama kinyume chake,lkn ngoja nieleze TU,kwa faida ya wengine ambao mnajiweka kua hamko upande wowote.ingawa kutokua na upande nao ni upande,maana Kuna upande wa East,west na Non Alignment Movement.
Sisi Pro Russia kwa uwezo wetu wa uchunguzi na utambuzi tumegundua kwamba USA ndio kinara wa vurugu machafuko mapinduzi na vita zote hapa duniani.
USA kwao ni huko bara la Amerika,kilichomleta ulaya ni Nini?
USA ana makambi ya kijeshi na silaha za aina zote ulaya yote,je makambi na silaha hizo ni kwa ajili ya nani?
Tuanze,
USA ana silaha za nyukilia na zisizo za nyukilia ulaya,ana wanajeshi vifaru melivita na ngegevita na kadhalika ulaya,je zana zote nzito hizo ni kwa ajili ya nani?
Haya.
Hebu tujiulize,ulaya magharibi yote ni marafiki wa USA na ndiko alikoweka silaha zake,je ni nchi Gani nje ya ulaya magharibi inayoweza kuingia vitani na USA na kupelekea USA kutumia silaha za nyukilia?
Jibu unalo.
Basi tufanye hivi,hizo nyukilia sio kwa ajili ya Urusi,je ni kwa ajili ya nani basi?
Je ni kwa ajili ya nchi mojawapo ya ulaya magharibi?
Hapana.
Je ni kwa ajili ya nchi mojawapo ya Afrika?
Hapana.
Je ni kwa ajili ya nchi mojawapo ya middle east?
Hapana,
Je ya far east?
Hapana.
Kama ni hapana hapana hapana,ni kwa ajili ya nani Sasa?
Namaanisha ni nchi Gani duniani USA anaihofia kiasi Cha kusogeza silaha za nyukilia ulaya magharibi?
Haya tuendelee.
Je ni Nini kimempeleka USA kwenda kuunda umoja wa kijeshi ulaya magharibi NATO badala ya kubaki hukohuko kwao bara Amerika, na kuunda umoja wa kujihami hukohuko kwao?
USA inakaa bara la mbali sana Tena kuna bahari kubwa inaitengnisha na ulaya,kwa Nini ametoka umbali wote huo na kwenda kuunda umoja wa kujilinda huko?
Kimsingi pro Russia hawafurahii Ukraine kupigwa na Warusi wala hawapendi na hawafurahii kuipiga Ukraine,lkn pro Russia wanachofurahia ni kuona kua kupitia kipogo anachopewa Ukraine Marekani atakoma kuonea nchi nyingine kisiasa kiuchumi na kijeshi.
Maana hapa "anaepigwa ni Ukraine lakini anaeumia ni USA ."
Unajua kua kabla ya kuvunjika Soviet union,Ukraine ilikua ni sehemu ya Soviet union.?
Baada ya kuvunjika Soviet union Urusi haikua na shida wala mgogoro na Ukraine.
Sasa hapa itategemea na uelewa wako wa masuala ya intelijensia.
Urusi ilipendelea majimbo yaliyojitenga na USSR yabaki nyutro.
Lakini kama kawaida yake kivuruge USA akaanza tamaa zake juu ya Ukraine.
Akafanya figisu watu wakamtoa Rais aliekuwepo ukriane kwa maandamano.
USA Wakaanza kwa Siri kuwafunza wanajeshi wa Ukraine mbinu Bora kabisa za mapigano,ujenzi wa makambi na miundombinu ya kijeshi,Tena kwa ushirikiano wa NATO wote.
Je unafikiri ktk Hali kama hiyo Urusi wangekua wanapata usingizi kweli?
Pro Russia hatupendi vita,ndio maana tunaichukia USA Kwa sababu inaitia kiburi Ukraine,ila safari hii katika SMO hii USA imekutana na wajuzi wa vita.
USA imekua ndumila kuwili Leo watasema hili kesho watasema lile.
Tazama.
Baada ya Urusi kuivamia TU ukriane wakatangaza Kila aina ya vikwazo juu ya Urusi,
Sasa jiulize je USA ilipoivamia Iraq nani aliiwekea USA vikwazo?
Sio tu Iraq vipi Vietnam,Libya,panama, Afghanistan na hata Serbia?
Haya mambo ndio yanatufanya tuwe upande wa Urusi.
Hebu fikiria zaidi Kila vita,au mgogoro hapa duniani USA yupo,yeye ni nani?
Kwa Nini asitumie Umoja wa Mataifa kutatua migogoro hiyo ya vita badala ya yeye kujiingiza?
Marekani ndio chanzo Cha vita nyingi na migogoro mingi.
USA amesjiingiza migogoro hii,
Vietnam na ufaransa,
Korea Kaskazini na kusini,
Afghanistan na Urusi,
India na Pakistan,
Iraq na Iran,
Israel na arabs/Palestina,
Syria na waasi,
Somalia na waasi,
Urusi na Chechen,
Libya na waasi,
Waafrika na makaburu,
Cuba na waasi,
Yugoslavia na waasi,
Uturuki na wakurd,
China na Taiwan,
Na Sasa
Urusi na Ukraine.
Jamani huyu USA yeye ni nani na kwa nini yeye tu awepo Kila migogoro?
Anadai anaeneza demokrasia.
Hivi kweli USA ana demokrasia?
Mfano mdogo TU.
Nchi nyingi hapa duniani hazitaki kabisa ajenda ya ushoga,
Hata serikali za nchi zikipiga kura za maoni kidemokrasia kuruhusu ama kukataa ajenda za ushonga wananchi wa nchi hizo Nina uhakika kwa 99.9% watakataa ushoga.
zikikataa mambo hayo kwa mujibu wa Imani zao za kidini,Mila tamaduni ustaarabu wao na utashi wao USA atazitishia kuziadhibu kua zinakiuka haki za binadamu.
Kuchagua upande .
USA utaisikia mara kwa mara ikiikemea Urusi eti isizichagulie marafiki nchi za kisoviet za zamani,wakati yenyewe Kila siku inazikemea nchi zinazopendelea kua na urafiki na Urusi na china.Mfano nchi za kiafrika, latin Amerika mashariki ya kati na mashariki ya mbali.
Ndio maana Sasa baada ya kuona Urusi anaweza kuwakinga na vurugu za USA ndio unaona akina Saud Arabia na nchi nyingine zimeamua kuachana na utumwa wa USA.
Pro Russia hatushabikii vita tuanashabikia mpenda vita kuadhibiwa kupitia Ukraine.
Urusi ikimpiga Ukraine anaeumia ni USA .