Uelewa wako wa maswala ya Kijeshi ni mdogo sana. Jasusi ni nani na mwanajeshi ni nani?
Anaweza kua Sahihi.Jasusi now days sio lazima awe mwanajeshi kama zamani.
Saivi dunia ishabadilika sana ujasusi umegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni
1.Ujasusi wa kiuchumi,majasusi hawa sio lazima wawe wanajeshi bali inabidi wawe wabobezi wa biashara, utafiti wa kibiashara na hujuma za kibishara KWA nchi zingine au taasisi ,technolojia n.k kwa manufaa ya nchi yake.Na ndio wanatakiwa wawe washauri wa mambo ya kibiashara katika nchi husika ikiwemo ushauri wa miradi ya kimkakati
2.Ujasusi wa kidola.Huu ni ujasusi mkongwe zaidi hasa kwenye nchi za kijama asilimia kubwa ya majasusi hawa wanakuwa na elimu ya kijeshi kwa mfano kwa hapa bongo wengi wanakua recruited kutoka jeshi la polisi, magereza , uhamiaji,pamoja na JWTZ..Hawa wanahusiku na dola kuhakikisha dola inakua salama na mamlaka yake ndani na nje ya mipaka pamoja na usalama wa nchi kwa ujimla.
Na kwa hapa bongo ujasusi huu wa kidola upo imara sana, Ndio maana tunajivunia hii amani tuliyonayo. Ila ujasusi wa kiuchumi mhhh naona report ya CAG inajieleza.
3.Kuna ujasusi wa diplomasia ,propaganda na siasa katika nchi husika.Hawa jamaa ukiwapa nafasi ya kuongea umekwisha hapa kuna wapatanishi,washawishi,kuna wakubadilisha nyekundu kja nyeusi kwa maneno tu.
Tukiridi kwenye mada putin alikua anafanya ujasusi unaohusiana na jeshi,kupata taarifa nyeti za kijeshi siraha na n.k.kwa mktadhaa huu lazima alikuwa na elimu ya kijeshi hakua raia.
Kipindi cha zamani majasususi wengi walikua na elimu ya kijeshi kwa sababu mda mwingi kulikua na matishio ya kivita.
Lakini kwa sasa ujasusi umebezi sana kwenye kutumia technolojia na hakili sana, taarifa nyingi zinatafuwta kwa njia ya kitecknolojia zaidi.
KWA wezetu mtu anaweza kua amekaa zake nchi moja lakini anachunguza nchi nyingine kwa kutumia mitambo.lakini pia kwa kuiba document nyeti kwa njia ya hacking.Ujasusi wa kutumia minguvu na wakuapear physically kwenye eneo la uchunguzi umeanza kupotea.japo hajwezi potea kabisa.
Nb.ili nchi iweze kuendelea lazima nyanja zote za ujasusi zishirikiane, pia lazima wao ndio wawe wa zarendo wa kwanza wa nchi yao.
Pili wanasiasa wasiwatumie kwa maslahi yao binafsi.lazima wajue wao wapo kwa ajili ya maslahi ya nchi kwanza na sio wanasiasa au mtu maana mtu anapita ila nchi itabaki kuwepo.