Nilikuwa sitaki kuandika lolote kwenye mjadala huu tena ila wewe nitakujibu. Kwanza tumia lugha nzuri kujibizana hoja, ukianza lugha mbovu hata mimi ninazijua sana. Naona unaanza na lugha mbovu lakini nitaziacha kwa wakati huu.
Urusi haikuvunja Warsaw Pact bali himaya ya urusi ilianguka kwa kuishiwa nguvu,
Sawa kabisa ,himaya ya Urusi ilianguka na kupelekea Warsaw pact kuvunjika.
Sasa NATO ya kazi Gani? Wakati mpinzani wake Warsaw pact ilishajifia?
Kibaya zaidi makubaliano yalikua NATO isiendelee kujitanua kuelekea east,je walitekeleza makubaliano hayo?
na hivyo nchi zile ilizokuwa
inazinganangaia kuuna USSR na Warsaw Pact zikawa huru. Ndiyo Maana Ukraine ni nchi huru.
Ukraine ni n hi huru sawa kabisa ,lkn pia si unakumbuka kua hata Cuba poa ni nchi huru?
Je USA alikua comfortable kwa Urusi kupeleka nuke pale Cuba?
USA ilotaka kuifanya Nini Cuba?
Na je Leo hii Urusi ikipelwla silaha na majeshi Cuba ama mexico USA itakua comfortable?
Kwa kifupi wasiwasi alionao Urusi ndio wasiwasi huohuo alionao USA
, na Poland (yenye jina la Warsaw) ni member wa Nato. Putin ndiye mwenye mawazo ya kiazamani kujaribu kurudisha USSR na Warsawa pact.
NATO ni muunganwo wa kijeshi wa nchi huru, nchi yoyote inaweza kujiunga na faida kubwa ya NATO ni kuwa wanachama hwake hawawezi kupigana vita, hali inaoongeza amani katika maeneo yao.
Ndugu yangu hebu tuwe kama watu matured bana.!
Hivi wewe kwa akili Yako unataka kutuaminisha humu Jukwaani kua NATO Haina shida na Urusi kweli?
He u kua serious kidogo basini mtoto mdogo TU asiejua kua NATO lengo lake ni kuivizia Urusi.
Documents zipo,wamarekani wenyewe wanasema hivyo na watu wote makini wanajua hivyo.
NATO ni kwa ajili ya Urusi baba kubali kataa.
Kama wewe unadhani kuwekeza nchi ni kuhujumu usalama basi hata Tanzania tuachane na kinachoitwa wawekezaji. Mtu akija kuweka raslimali zake kwako anakuwa amakuamaini kama nchi na anahitaji usalama. Hakuna vita inayoimarisha usala hata siku moja.
Sijasema kuwekekza ni kuihujumu usalama wa nchi
Kwa maelezo Yako kua nchi (USA) imewekeza Urusi na hata west,watawezaje kuihujumu?
NAMI ndio nikapigana na hoja Yako hiyo.
Ndio ni kweli wamewekeza,lkn bado wanaendelea kumhujumu.na ndio mgogoro huu wa ukraine
Urusi haikua na tatizo na uwekezaji toka USA ama west ndio maana hata hiyo Kampuni ya mafuta ya USA ikakaribishwa kuwekeza kiungwana TU.ndio maana pia Urusi ikawa inafanya biashara na Europe na hata mradi wa Bomba la gesi kati ya Urusi na ujerumani ukaanzishwa.
Lkn hayo hayo hayakuiondolea USAnia mbaya ya kutaka kuendelea kuihujumu Urusi kwa njia nyingine ili ije iishinde kijeshi.
Nikakupa na mfano kuwa,USA Ina uwekezaji mkubwa sana china,je Hali hiyo imeizuia USA kuvutana na china?
Notion ya uadui baina ya nchi za mashariki na magharibi imeanza kuwa kubwa sana miaka ya hivi karibuni wakati wa utawala wa Putin na Xi Jinping. Miaka yote ya tisini baada ya kuanguka kwa USSR na China kuana biashara na nchi za west hadi 2010 hakukuwa na hostility hiyo hadi pale walipojisiskia wana nguvu.
Baada ya china kuwa na nguvu.
Dah aisee!
Sasa niambie china kamchokoza nani hapo? Au kamtishia nani hapo?
Kama ni mgogoro wa Taiwan upo miaka na miaka na hakuna Rais wa uchina aliezubaa katika jambo hilo.
Uadui baina ya west na east ama kwa kifupi baina ya Urusi na china dhidiya USA na NATO unakuzwa na USA kubali kataa.
Miaka ya 2000 USA ilotaka kujenga mtambo wa Lada nchi Romania na mtambo wa kudungua makombora nchini Checks,je hiyo mitambo ilikua. Ni kwa ajili ya kujilinda dhidi ya nchi Gani?
Na unafikiri ni Kwa nini haikujengwa?
ndipo wameamua kuanza hostility tena kwa kutatumia vigezo vya "uadui". Adui wako hawezi kushirkiana nawe kwa kuwekeza kwako ili kusaidia uchumi wako.
Da kwa hiyo kuwekeza kwenye nchi nyingine ni kuisaidia kiuchumi nchi hiyo?
Kwa hiyo sio kwa ajili ya nchi mwekezaji kupata faida?