Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Kuna biscut special
 
Mbona sioni shimo mdogo wangu. Naona picha ya wazungu wawili na wewe LGBTQ. Au siyo wewe huyo?
Shimo lako mwenyewe utalionaje? Tunaliona sisi unapoanza kampeni zako za utangazaji kwa mtindo wa kupinga. Hiyo michezo ni mibaya iache, Watanzania WATAKULAANI.
 
Nini yalikuwa majukumu ya Ukraine katika mkataba huo.

Je Iliwaruhusu kujiunga NATO?
Je Haukuwataka kuwa Neutral State?

Vipi kuhusu Minsk Agreement?
Nani alivunja?
 
Ukiwaambia watakosa wateja kutoka Magharibi huoni umewalazimisha vile vile?

Tena mkuu acha uongo, yapo yaliyotishwa kuwekewa vikwazo iwapo yataendelea kufanya biashara na Urusi?

Sasa hii unaizungumziaje kama free trade na hayaongozwi na serikari Yao?
 

Sawa kabisa ,himaya ya Urusi ilianguka na kupelekea Warsaw pact kuvunjika.
Sasa NATO ya kazi Gani? Wakati mpinzani wake Warsaw pact ilishajifia?

Kibaya zaidi makubaliano yalikua NATO isiendelee kujitanua kuelekea east,je walitekeleza makubaliano hayo?
na hivyo nchi zile ilizokuwa

inazinganangaia kuuna USSR na Warsaw Pact zikawa huru. Ndiyo Maana Ukraine ni nchi huru.
Ukraine ni n hi huru sawa kabisa ,lkn pia si unakumbuka kua hata Cuba poa ni nchi huru?
Je USA alikua comfortable kwa Urusi kupeleka nuke pale Cuba?
USA ilotaka kuifanya Nini Cuba?
Na je Leo hii Urusi ikipelwla silaha na majeshi Cuba ama mexico USA itakua comfortable?
Kwa kifupi wasiwasi alionao Urusi ndio wasiwasi huohuo alionao USA
, na Poland (yenye jina la Warsaw) ni member wa Nato. Putin ndiye mwenye mawazo ya kiazamani kujaribu kurudisha USSR na Warsawa pact.

NATO ni muunganwo wa kijeshi wa nchi huru, nchi yoyote inaweza kujiunga na faida kubwa ya NATO ni kuwa wanachama hwake hawawezi kupigana vita, hali inaoongeza amani katika maeneo yao.

Ndugu yangu hebu tuwe kama watu matured bana.!
Hivi wewe kwa akili Yako unataka kutuaminisha humu Jukwaani kua NATO Haina shida na Urusi kweli?
He u kua serious kidogo basini mtoto mdogo TU asiejua kua NATO lengo lake ni kuivizia Urusi.
Documents zipo,wamarekani wenyewe wanasema hivyo na watu wote makini wanajua hivyo.
NATO ni kwa ajili ya Urusi baba kubali kataa.

Kama wewe unadhani kuwekeza nchi ni kuhujumu usalama basi hata Tanzania tuachane na kinachoitwa wawekezaji. Mtu akija kuweka raslimali zake kwako anakuwa amakuamaini kama nchi na anahitaji usalama. Hakuna vita inayoimarisha usala hata siku moja.

Sijasema kuwekekza ni kuihujumu usalama wa nchi
Kwa maelezo Yako kua nchi (USA) imewekeza Urusi na hata west,watawezaje kuihujumu?
NAMI ndio nikapigana na hoja Yako hiyo.
Ndio ni kweli wamewekeza,lkn bado wanaendelea kumhujumu.na ndio mgogoro huu wa ukraine

Urusi haikua na tatizo na uwekezaji toka USA ama west ndio maana hata hiyo Kampuni ya mafuta ya USA ikakaribishwa kuwekeza kiungwana TU.ndio maana pia Urusi ikawa inafanya biashara na Europe na hata mradi wa Bomba la gesi kati ya Urusi na ujerumani ukaanzishwa.
Lkn hayo hayo hayakuiondolea USAnia mbaya ya kutaka kuendelea kuihujumu Urusi kwa njia nyingine ili ije iishinde kijeshi.

Nikakupa na mfano kuwa,USA Ina uwekezaji mkubwa sana china,je Hali hiyo imeizuia USA kuvutana na china?

Baada ya china kuwa na nguvu.
Dah aisee!
Sasa niambie china kamchokoza nani hapo? Au kamtishia nani hapo?
Kama ni mgogoro wa Taiwan upo miaka na miaka na hakuna Rais wa uchina aliezubaa katika jambo hilo.
Uadui baina ya west na east ama kwa kifupi baina ya Urusi na china dhidiya USA na NATO unakuzwa na USA kubali kataa.
Miaka ya 2000 USA ilotaka kujenga mtambo wa Lada nchi Romania na mtambo wa kudungua makombora nchini Checks,je hiyo mitambo ilikua. Ni kwa ajili ya kujilinda dhidi ya nchi Gani?
Na unafikiri ni Kwa nini haikujengwa?
ndipo wameamua kuanza hostility tena kwa kutatumia vigezo vya "uadui". Adui wako hawezi kushirkiana nawe kwa kuwekeza kwako ili kusaidia uchumi wako.
Da kwa hiyo kuwekeza kwenye nchi nyingine ni kuisaidia kiuchumi nchi hiyo?
Kwa hiyo sio kwa ajili ya nchi mwekezaji kupata faida?
 
Acha uwongo na wewe. Kampuni Kama MacDonalds inayouza Burgers haiwezi kuingiliwa na serikali ya Marekani.
 
Kwa hiyo huko kujihami ndio kuizunguka Urusi?

Kwa hiyo ni Swala la kipaumbele na sio uwezo wa kiuchumi?

Kwa hiyo Urusi akifungua Kambi Mexico,Puerto au Cuba ni sawa?
Maana ni Swala la kiuchumi na kipaumbele?

Hivi unajua hata ulichojibu?

Vipi Australia kung'aka kwa Solomon Island baada ya China kutaka kufungua kituo chake Cha kijeshi?

Tena walipendekeza ikiwezekana waivamie kijeshi?
 
Hujui kutume ujumbe haraka, unaandika maneno mengi (wordy) sitaweza kukujibu kwa vile ninafanya kazi nyinge pia, kwa kwa hiyo siweza kusoma post yako ndefu sana.
 
Acha uwongo na wewe. Kampuni Kama MacDonalds inayouza Burgers haiwezi kuingiliwa na serikali ya Marekani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Waungwana mmemsoma huyu?

Kama haiwezi ingiliwa kwa nini iliondoka Urusi?

Walifunga rasmi biashara yao mwezi wa 12 mwaka 2022.

Unadhani kwa nini hawawezi kuingiliwa?
Kwamba wenyewe Wana immunity na vikwazo vya Magharibi?

Au ipo juu ya serikari ya Marekani na Ulaya?
 
Hujui makampuni ya kimarekani unadhani kuwa ni kama shirika la umma. Unajua umuhimu wa kutunza hisa za wawekezaji wewe? Wamarekani wakisema wanauza hisa zao zote za MacDolds kwa vile hawakubaliana na mwenendo wao kampuni hiyo hujui kuwa itakufa siyo kwa kuuwawa na serikali. Rais wa marekani wana hisa nyingi sana kwenye makampuni hayo na vile vile Marekani ni soko kubwa sana kwa makampuni mbalimbali. Serikali inaweka chachu tu kwa raia wake halafu kampuni yenyewe inaamua la kufanya; usidhani Marekani ni nchi ya kiditeta kama unazotetea.

Serikali inaweza kutoa tamko kuwa kampuni inayofanya biashara na mtu fulani haitapata contract za serikali. Inabaki ni kazi ya kampuni kuamua iwapo contract za serikali ni muhimu au vipi. Hawalazimishwi.
 
Hii unafahamu unachokizungumzia hapa?
Kwanza asilimia 70 ya hisa za macdonald ni za kitaasisi hivyo hao watu sijui nini hakuna.

Pili sera za makampuni huwa zinaathiriwa na sera za Serikari zao.

Sera ya Marekani ilikuwa kuidhoofisha Urusi kiuchumi na kushinikiza makampuni ya Magharibi kujiondoa ndio maana alizishirikisha nchi zilizopo Umoja wa Ulaya.
Sasa niambie, je sera ya nchi haijaathiri biashara ya Mac?
Kama imeathiri, hao Wana hisa wamejiondoa?
Na kama hawajajiondo kwa nini?

Kumbuka Kuna reputation risk kwenye makampuni lakini sio kwa blunder iliyofanyika kipindi hiki Cha Dementia joe.

Kwenye hii op, tumegundua kuwa kumbe duniani hakuna free trade achilia mbali fair.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…