Hakuna kudharaulika tumejidharau wenyewe.
Wewe hapo ulipo unatumia kifaa kinachotoka hukohuko kwa mabeberu kwa nini hatutengenezi vya kwetu tukawauzia wao ili na sisi tujigambe kama tuko vizur kiteknologia?
Itakua huwajui wazungu vizuri...huwajui kwakua hufuatilii kwa upana, na wanadamu ndivyo walivyowekewa ule moyo wa kufanya kinachoendelea, nakupa mfano wa karibu kbs...familia yako..!!!
Nadan ya familia yako kuanzia babu yako na ndugu zake...(nimechagua kizazi hicho kwakua ndicho kilichotawaliwa na mkolon mzungu) babu yako na ndugu zake hawalingani kipato, elimu wala uwezo wa kujiendesha kimaisha, kizazi hcho kina watoto ambao ndio baba yko, baba wakubwa na wadogo na mashangazi zako wajomba na mama wakubwa na wadogo, wote hawalingani hali ya maisha...kizazi cha tatu ambacho ni wewe na ndugu zako na binamu zako nanyi hamlingani kipato, wala elimu, wala hamlingani namna ya maelewano..wala hamlingani ujuzi wa aina fulan..mnabaguana, kuna ndugu unazungumza nao vizur wengine bora liende na wengine basi, kuna wale matawi ya juu na wale kiporo cha ugali na chai kwao ndio jadi..je umewahi kuweka kikao cha familia ukawauliza kwanini mnatofautiana hivo? Kwanini familia zenye uwezo mnabaguana na zisizo na uwezo ndani ya kizazi cha kwanza nilichokitaja?
Mmejikuta tuu alie nacho hataki mwingine apate, na juhud za kukwepana au kusaidiana kwa wale mnaopendana hadi wewe mtoa mada unazifanya, kwanini unafanya hvo?
Ukiweza kuelewa jinsi familia yako kuanzia babu imekuaje mkawa hivo basi utaelewa familia dunia inavyoishi..alie nacho anapendelea yule anaempenda tuu, yule usiempenda unafanyiwa uzibe asifikie level yako...uzibe unaweza kuwa maneno ya ya kufifisha uwezo wa usiempenda hata km anaweza kukuzid, zikitokea conections humjulish nduguyo..unahis atakupita, unahis akifanikiwa hatakuheshim km mwanzo, hutajigamba km mwanzo, atakua level yko..atakua na sauti kama wewe, hutakua na nguvu ya kum-comand utakavyo, ......
Ndivyo nchi zilizoendelea ziliishi na zinakazia hapohapk...umasikin wetu sio kupenda kwetu..ni desturi iliyojijenga ndani ya nafsi zetu wanadamu na ikawa fursa kwa mataifa yenye nguvu...ukiendelea wewe wao wataishije kwa furaha na rasilimali za kufurahia hapa duniani ni chache watu ni wengi? Huoni hata kwenye familia za watu unaowajua au kuskia stor zao wanatamani wengine wafe ili wao warithi mali? Sisi tunafanyiana hayo kifamilia, ila wazungu wanafanyiana hivo ngazi ya kifamilia kiukoo kitaifa hadi kidunia maana walianza zamani wakati sisi tuliishi kijamaa chini ya machifu..wao wanaishi kikoloni kukaba kupora na kuiba maeneo ya jamii nyingine na kuweka mfumo wa kunufaika hata wakiwa mbali..
Ndugu za baba wa babu yangu wamechapwa sana mijeledi na wakoloni, wengine waliuliwa wengine walichukuliwa watumwa wapo german na uk wengine waliuzwa kwa matajiri wa mashamba US