Kwani nani kasema Marekani ni Mungu na hakosei?
Kwahiyo mlitaka Marekani asiwahi kosea, na akikosea makosa yake mliyalinganishe sawa na Russia hata kama hayafanani kabisa.
Russia ina fleets tano za Navy, mwaka jana Ukraine imezamisha flagship ya fleet mojawapo. Ni lini tangu uwepo wa Marekani flagship yake iliwahi zamishwa na adui?
Kosa la Marekani pale Yemen ni la kiintelijensia, kosa la Urusi kwenye Black Sea ni la kijeshi. Haijalishi una intelligence au huna ukiwa vitani na meli inamshambulia adui jirani na ardhi yake unajipanga kumkabili.
Kwahiyo umekubali kwamba Urusi ilionyesha udhaifu kijeshi sasa twende kwenye makosa ya Marekani kiintelijensia. Aya KGB ilikuwa wapi mpaka USSR wanagawana mbao, Putin anakimbia na mafaili kule Eastern Germany?
Unadhani CIA itakaa tu wakati kuna watu wanapanga kuivunja Marekani iwe vinchi vidogo.