Sifahamu chochote juu ya siasa za kimataifa ndio maana si mjengaji hoja humu ndani kama wataalamu wengineo.
Bahati nzuri nimekuwa mfuatiliaji wa hii thread tokea nyakati wadau wanabishana humu ndani kwa maana ya kabla ya february 23
Je russia ataivamia ukraine?
Je marekani na wenzake watakubali uvamizi huo?
Ndio maswalinyaliotawala humu ndani.
Baada ya russia kuvamia ndipo nikachagua team russia, nimemchagua urusi kwa sababu niligundua ndiye mkubwa ndio maana akaingia ukraine bila kuhofia majibu ya marekani na wenzake waliopambwa humu ndani kwa kila neno zuri
Leo kiko wapi, kwenye hii operesheni nimefanikiwa kumfahamu ukweli kidogo na muongo sana kwa nyakati tofauti.
Wote wanadanganya na wote wanasema ukweli kwa kiwango tofauti
Nashangaa kuona vijana wajengaji hoja wanaingizwa kwenye mtego wa kitoto Wa kuamini au kupinga kila neno linazongumzwa na pande husika.
Kwa jinsi movie hii ilivyokuwa inakwenda ilikuwa rahisi kufahamu ya kwamba mission ya wagner itaishia bakhmut na si kwamba wanaondoka kwa sababu ya silaha na ndipo walipoweka mtego wa kusaga nyama za ukraine Ili kufikia lengo la denazification.
Wagner wapo bakhmut kwa zaidi ya miezi 8, sasa tujiulize hizo silaha wanatoa wapi na wana supply vipi kutoka command moja kwenda nyengine.
Ok hawana silaha sasa kwa nini hawatandikwi sana kama ukraine, ni juzi tuliambiwa urusi wameishiwa silaha na wanatumia makoleo.
Warusi waliokusudiwa hapo ni wagner kwa sababu ndio wapelekaji moto hapo bakhmut hivyo ilihitajika njia ya kuwadanganya ukraine na wafuasi wao waamini huyu dubu atapigika tu huko mbeleni bahati mbaya dubu mwenyewe ndio kwanza anaendelea kuzaa.
Ni upi muelekeo wa wagner?
Kuna mgogoro mengi sana huku afrika, nadhani baada ya biashara ya kuitangaza vizuri wagner hapo ukraine nadhani kituo kinachofuata ni kusambaratisha mtandao wa kin1yonyaji hapa Afrika.
Demilitarization na Denazification imefanywa kwa kiwango cha juu.
Wanaosubiri russia aendelee kuteka maeneo ya ukraine kuelekea kiev anajidanganya, itamhitaji mrusi kupigana miaka 10 au zaidi jambo ambalo haliwezekani kwa sasa