Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ni swala la muda tu, kuna kifurushi ambacho Germany kakitoa kina IRIS T 4

Nadhani dunia ishaona jinsi zana za Urusi zilivyo hadi EW inapigwa
 
Germany kafunguka zaidi.
Maana yake kadri muda unavyoenda mwisho wa huu mwaka Urusi hatakuwa na uwezo wa kuipiga Ukraine maana atakuwa ma defenses nyingi na ujuzi, uzoefu
 
Hizi Gepard mjerumani alishazistaafisha tangu 2010 (yeye hazitumii tena) na ni tech ya miaka ya 1960 lakini Leo hii (miaka 60 baadae) imekua mwiba mchungu dhidi ya suicide drone za Iran. Kweli mjerumani kwenye tech sio wa mchezo mchezo.
Hata patriot ni ya miaka ya zamani ila kombora la miaka ya 2010s limepigwa busu
 
Labda Urusi alikuwa na plan ya assassination ya uongozi mzima au coup ndo maana hakufanya uharibifu,

Maana Zelensky anadai siku yalile tukio viongozi wote waliwekwa sehemu tulivu kwa mwezi mzima
 
Nadhani hili ni tatizo la silaha nyingi za West,zinakua complex kupitiliza. Kama wamarekani walivyoweka jet engine kwenye Abrams tank pamoja na makorokoro mengine. Sasa hii Kwa Ukraine itakua ni logistical nightmare
Ukraine ndo itakuwa nchi yenye mifumo mingi kutoka nchi nyingi.
Tuwasifu kujifunza kwa haraka na mapema

Ipo siku utaambiwa wamepewa F16
 
Ndicho nachosema kwao inawafaa Ila Kwa wengine ni issue.

BTW ngoja tuone kama Black see fleet itapona hapo Sevastopol baada ya Ukraine kupata Storm shadow cruise missile.
Mambo mengi yanatokea ila tunayaacha yapite. Last month Shoigu alivyoita drills za ghafla kwa Pacific fleet yule Admiral alistaafu wiki ileile drills zikiwa zinaendelea. Haitakiwi iwe vile ni sawa na ligi inaendelea alafu kocha eti mkataba umeisha.

Warusi wana silaha zinatakiwa zifanye vizuri ila kwenye trials wanapindisha ukweli, storage wanaiba, contractors wanatafuta faida kubwa yani kila hatua kuna kitu kinapunguza effectiveness. Hata air warning radars zao kina Volonezh kuna taarifa nimesoma zina cheap components kama transistors hivyo radar hazipo effective inavyotakiwa. Ni kama wakandarasi wetu wa halmashauri wanavyonunua taa za solar zenye maandishi sawa kwenye makaratasi na label ila in reality quality ni ya chini, mnunuaji na mtengenezaji wanakubaliana waandike vitu sio wagawane cha juu
 
Germany kafunguka zaidi.
Maana yake kadri muda unavyoenda mwisho wa huu mwaka Urusi hatakuwa na uwezo wa kuipiga Ukraine maana atakuwa ma defenses nyingi na ujuzi, uzoefu
Nadhani dunia inashuhudia udhaifu wa Nchi za NATO na nguvu za Russia yaani NATO na EU nzima zinapeleka silaha isipokuwa tz hatujapeleka ungo kutoka sumbawanga[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kwa sasa wanaogopa ingia kizembe
Sio kwa sasa tu. Tangu siku ya kwanza battle of Hostomel walikuwa na Mi-8 transport nyingi, Mi-24 na Ka-52, kisha Mi-28 chache.

Wakati Mi-28 inatakiwa iirithi Mi-24 Hind ila sasa naona Hind ina performance nzuri ingawa zamani nilikuwa naidharau sana kisa tu nailinganisha na AH-64 Apache ambayo ni direct competitor wake.
Kitu ambacho nakuja kuona Mi-24 iko na armour nzuri, inabeba troops 8 na ni gunship hapohapo jambo zuri hasa kwa nchi zisizo na bajeti kubwa, hii heli hata NATO waliisifia kuleta idea mpya kabisa kwenye battle. Hapo nimekuja ona kwanini Mi-24 bado zinauzika wakati Mi-28 hazina soko kivile.

Ka-52 ni complex na nimeona iko very vulnerable kwa sababu ina components nyingi hasa za ile counter-rotating rotor, rahisi sana kujiuma ikipata hitilafu kidogo ya blades hata small caliber fire. Alafu kinachoiponza ni kukosa smart munitions, helicopter nzuri ila inatumia unguided rockets zaidi kuliko missiles. Matokeo yake lazima iwe karibu na adui inayeshambulia ishuke chini kupata target na isitembeee wakati inamshambulia, ni majuzi tu wameanza test new ATGM ambayo inasemekana ni ghali ila itaondoa ulazima wa Alligator kuingia sehemu hatarishi

Nina wasiwasi Mi-28 Night Hawk haiko vizuri, nitatafuta kujua
 
Labda Urusi alikuwa na plan ya assassination ya uongozi mzima au coup ndo maana hakufanya uharibifu,

Maana Zelensky anadai siku yalile tukio viongozi wote waliwekwa sehemu tulivu kwa mwezi mzima
Mwanzoni kabisa niliandika hisia ya mtaalamu mmoja aliyedai inawezekana Putin alitumia akili za FSB zaidi kuliko za jeshi. Ndio maana traitors, watoa targets na sympathizers walikuwa wengi ndani ya Ukraine wakielezea movements za majeshi, silaha zilipo, sites za AD, miundombinu muhimu. Baada ya Russia kuanza ua kiholela simphesizers wakaikataa, na Ukraine ikapiga operation kali kuondoa mamluki na sometimes walikiuka haki za binadamu.

FSB ndio iliwadanganya Warusi kwamba mambo yatakuwa kama Crimea twende na misururu. Wakati huko MI6 na CIA ilishawapanga Ukraine miezi miwili kabla wanabisha, baadae wakakubali mwishoni. Siku chache kabla tarehe ya kuvamia ilishajulikana na CIA. Hivyo ni sahihi Putin hakutaka kuiharibu Ukraine akijua kina Zelensky watatimua mbio
 
labda tunashindwa kuelewana kitu hapa...Wagner,NATO wote hawa ni Soldiers..!!!...wanaposhindana lazima awepo mshindi kati yao.....sasa ushindi unaletwa na nn?...hili ni swali la kwanza!...swali la pili ww unaongelea ubora wa askari wanaopigana au vp..??..labda kama hoja yako ni hizo mbili hapo juu...sasa njoo na ajenda ya kwamba Wagner hawawezi kupambana na NATO..kwa sababu kadha wa kadha..tuanzie hapa tafadhali...!!!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
leo T14 Armata yuko Live .... huenda ni kwa sababu ya hz ndege zilizodondoka leo...ila kuanzia kesho hatutamuona humu kama kawaida yake...atatuambia ratiba imemtait...kumbe hana cha kutuhubiria humu mambo yashakuwa alijojo kwa upande wa UKRN.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Chenga ya mwili alipigwa Putin, EGO pekee ndo inamsababisha Putin asisitishe hii vita.

Ila kashindwa, wanajeshi wake wengi hawaamini kabisa ila ndo hivyo wanafata amri.

Ile kwamba umevamia nchi afu Rais wa hiyo nchi yuko huru kusafiri kwenda nchi zingine mf leo yupo Italy kaondoka jana atarudi kesho, yaani siku 3 Zele yuko nje ya nchi yake na bado Urusi anapelekewa moto.

Binafsi naamini bila msimamo wa hiki kijamaa lazima Russia angekuwa amevamia nchi zingine.
Msimamo wake, uzalendo, hasira zimesababisha Ukraine iendelee kupigana
 
[emoji298]️During a meeting in the Vatican, Volodymyr Zelensky asked the pontiff to condemn Russian crimes in Ukraine

The President also called on Pope Francis to make every effort to bring home tens of thousands of Ukrainian children deported by Russia.

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
[emoji634]Italian Prime Minister Giorgia Meloni has expressed confidence that Ukraine will win the war against Russia after talks with President Volodymyr Zelensky.

“I am convinced that Ukraine will win, recover even stronger, more prosperous. The future of Ukraine is the future of peace and freedom, and it is the European future. And there are no other possible solutions,” Meloni said.

She noted that Rome will continue to work with allies to provide military support to Ukraine.

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…