Nilicgoandika kama kinakuchekesha una matatizo, hakuna lolote la kuchekesha. Ngoja nikuulize, kama hutaki Mishustin awe famous ni ipi ranking ya powerful men in Russia?
Yani command ya Russia kiserikali watano wa juu ni kina nani. Sababu kwa Marekani unayoitaja namna ilivyo wa kwanza in command ni Rais Biden na wa pili ni Vice Kamala na wote hawa wanasikika vizuri sana na Kamala anafanya ziara na kumuwakilisha Biden mara kibao. Sasa hapo unasemaje hasikiki?
Russia haina Makamu, Waziri Mkuu Bwana Mishustin anaonekana wapi. Kwenye Victory Day Parade sherehe kubwa zaidi kitaifa haonekani, ziara kimataifa haonekani, kuunga mkono operation haonekani, media akifanya matangazo na hotuba hamna. Yani anafichwafichwa anatokea mara chache mno.
1. Dmitry Medvedev ni maarufu kumzidi, wakati Medvedev ndio aliondolewa kwenye nafasi ya PM na aliwahi kuwa Rais term moja. Sasa hivi yuko Security Council anasikika kuliko PM.
2. Dmitry Rogozin kaobdolewa ROSCOSMOS na alikuwa Deputy PM ila ni maarufu na anasikika kuliko PM sema kwa sasa anaumwa.
3. Dmitry Peskov ni msemaji wa Putin ila ni maarufu na anasikika kuliko PM.
4. Sergei Shoigu ni Defence Minister, maarufu sana na anasikika kuliko PM wake. Huyu ni untouchable.
5. Sergei Lavrov huyu hakuna haja ya kusema mengi.
6. Sergei Naryshkin mkuu wa ujasusi ni powerful, maarufu kiasi kutokana na unyeti wa kazi na ana umuhimu sana. Hata mkuu wa usalama naye anasikika kuliko Waziri Mkuu.
Hao wote ukitazama kwenye ranking Mishustin anawazidi kikatiba ila hasikiki kuliko wao. Hata kwenye vikao vya emergency, sijui kupata war briefing, kwenye maadhimisho ya kitaifa, ile baada ya Prigozhin kuasi kote uko humuoni akiwa front. Huwezi kutetea, point hamna.
View attachment 2688467
Mara zote za Putin kukaa kwenye meza ndefu na fupi kumkuta Mishustin ni nadra. Yani hata msemaji wa jeshi yule Igor Konashenkov anasikika na propaganda zake na hesabu za ajabu kuzidi Waziri Mkuu. Hata Maria anasikika mara chache chache