Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kwenye hiyo article uli share, unaambiwa Ukraine bado wanahangaika kuvuka 'grey zone' kwahiyo hata layer ya kwanza ya defense hawajaweza kutoboa na Urusi wana layer za kutosha za aina hiyo, hiyo Surovikin line imesukwa kininja, 'dunia' haikuwahi kuona kitu cha namna hiyo kwa zaidi ya miaka 80.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Urusi alijiandaa vizuri sana kuzuia hii offensive.
Ukweli ni kwamba Ukraine asingeweza kutoboa hii mechi, kikubwa ashukuru ulimwengu wa magharibi umesaidia kuchelewesha failure....
Orban alisema kipindi kile Russia hawaeleweki wanataka nini...alisema Russia wanauwezo mkubwa wa kuadapt changamoto kuzifanyia kazi na kwenda mbele na wakiishafanya hivyo hawarudi nyuma...
Russia kajikuta anaadapt matumizi ya drones, electormagnetic jamming etc..kuliko ile traditional fighting style yake ya kutumia vifaru, msafara mkubwa etc...
Vita ni kama biashara tu....huwezi kujijua unaweza ama la..mpaka uingie ufanye mwenyewe despite ya kuwa na theories kibao..

Nawaonea huruma EU na NATO....kupitia hii vita (SMO)...Jeshi la Urusi limekua na real time combat experience ya live ammunitions against a forminable foe...Ukraine + NATO help + Ecomonic & Techlogical Sanctions...(Wamejifunza vitu vingi sana na mapungufu mengi )
Hao NATO hawajawahi pata forminable adversary kama hii..

KAZI wanayo
 
Hii Vita pia imeilemaza sana Urusi na jeshi lake, itachukua muda kwa jeshi la Urusi kurudia hali yake ya kabla ya Vita.

Japo bado wana man power ya kutosha ila pia wamepoteza sana vifaa vingi na askari wazoefu.
Hii napingana na wewe...Jeshi la Urusi limepata mazoezi na combat experience ambayo itawasaidia kubadirisha vitu vingi kwenye combat experience..
Experience is the best teacher...Now they know what real war means...kizazi chao cha vijana ambacho kilikuwa hakijakutaka na uhalisia wa vita..wamepata ukweli...huwezi linganisha na vijana wa West Europe...
Kuanzia vita vya Syria mpaka Ukraine.Urusi kapiga jalamba la kutosha..

VITA NI HATARI, SIO MAKARATASI NA MIHEMKO..
 
Hii Vita pia imeilemaza sana Urusi na jeshi lake, itachukua muda kwa jeshi la Urusi kurudia hali yake ya kabla ya Vita.

Japo bado wana man power ya kutosha ila pia wamepoteza sana vifaa vingi na askari wazoefu.
Manpower yao sio kubwa kivile. Population ya Russia iko kwenye decline wao na kuongeza idadi ya watu huwa ni ugomvi. Ulevi, magonjwa, ajari, lifestyle mbaya haviwezi waacha wakue kwa idadi. Watu wanaokufa kila siku Urusi ni wengi kuliko wanaozaliwa, hii ni tangu 1994.

Idadi yao ya watu 144 milioni wapo wengi ila wengi pia sio military material. Mfano, Putin alitumia miezi mingi kufanya mobilization kwa nguvu na sheria kali akapata wapiganaji kama 300,000 wakati Israel yenye watu wasiofika milioni 10 (inazidiwa mara 14 kwa idadi ya watu na Urusi) ilitumia chini ya mwezi kufanya mobilization ya wapiganaji 360,000 kujiandaa na all out war dhidi ya Waarabu. Na hawakuvutana na watu wala kukimbizana mtaani.

Usitegemee population ya Urusi kivile. Population ninayoiamini sana huwa ya Iran, Turkey na North Korea hizo kupigana zinaweza. Hata China na India namba zao zitawabeba.
 
Kabla ya offensive ya Ukraine kuanza, Western military pundits walitabiri kutakuwa na 'break through' kubwa sana kwa Ukraine hasa ukizingatia

performance mbaya ya jeshi la Urusi hapo awali.

Silaha za kimagharibi hasa vifaru na magari ya kivita kama Bradley zilizofikia 200+ yaliyopelekwa Ukraine (japo bado ni chache sana)

Idadi kubwa ya askari wa Ukraine waliopewa mafunzo na majeshi ya magharibi....

Ila inaonekana hawa wachambuzi wa kimagharibi waliidharau mno Urusi kupindukia ila ni kama vile Warusi walijifunza makosa ya awali na kujipanga vizuri tena.
 

Zelensky admits Donbass very hard to return, doubts NATO membership​

30.11.2023 15:38

kuna watu wengine akili hawana,nadhani zelensky ni mmoja wao.
wewe Urusi kiungwana kabisa kakuomba nchi Yako iwe nyutro,hasa kijeshi yaani isifungamane na upande wowote, lkn wewe unang'ang'ania NATO.huu ni umoja wa kijeshi.Ni Bora hata ungekua ni umoja wa kiuchumi tungesema pengine Urusi inakuonea wivu kua utakua na uchumi mkubwa ,lkn umoja wa kijeshi! Tena umaoja hasimu na Urusi!
ama Kwa hakika zelensky ni mjinga mmoja.

haya hapa chini ndio maneno ya zelensky ya kukata tamaa.angalia sasa

It will be difficult for Ukraine to return the Donbass because those living in the region do not want that to happen, Ukrainian President Volodymyr Zelensky said during a meeting with students in Mykolaiv (Nikolaev).

President Of Ukraine is licensed under Public Domain Mark 1.0.
After ten years of hostilities in the region and life in the Russian environment, the population of Donbass would not want to return to Kyiv's rule, the Ukrainian President said. He also admitted that Ukraine would "return its territories before it could return those people.”

Earlier, Ukrainian Foreign Minister Dmitry Kuleba said that Ukraine had no intention to give up on its territories for the sake of NATO membership. He also noted that he was disappointed with the tempo of arms supplies from Western countries.
 
Na taarifa mpya ni kwamba Marekani wameiomba Ukraine irudishe vifaru vyo vya Abraham virudi USA.🤣🤣🤣🤣kwa hofu eti vitadakwa na Urusi.
 
Haujajifunza bado?

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Maelezo ni marefu but there is no point, anyway wapeleke izo submarine na aircraft carrier kama azijachomwa moto. Kule sio middle east mzee
 
Kabla ya offensive ya Ukraine kuanza, Western military pundits walitabiri kutakuwa na 'break through' kubwa sana kwa Ukraine hasa ukizingatia

performance mbaya ya jeshi la Urusi hapo awali.
Hakuna mahali Urusi walikua na performance mbaya tangu vita hii ianze ambayo Urusi wenyewe wanaiita operation.
Kile wewe unakiita performance mbaya ni hiki hapa.
Kumbuka Urusi ndio walioanzisha vita au mashambukizi kwenda kwa Ukraine.
Kabla hata askari wa kwanza wa Urusi hajarusha hata risasi moja, Ukraine ilikua Ina jeshi imara kabisa,ambalo lilirithi silaha nyingi kutoka USSR,sio TU silaha Bali pia mbinu za kivita.
Pamoja na hayo pia Ukraine ilikua na viwanda vya silaha.
Ukraine pia ilifanikiwa kupata mafunzo ya Hali ya juu sana kutoka NATO tokea mwaka 2014,sio TU mafunzo kwa ajili ya kuja kupigana na nchi mfano kama Greece hapana,Bali mafunzo muhimu kabisa ya kuja kupigana na nchi kama Urusi.
Ukraine ilipewa mafunzo na nchi Bora kabisa kama USA UK, German,Canada,France n.k.hebu fikiria ni mafunzo Bora kiasi Gani.
Pia fahamu kua Ukraine ilijengewa miundombinu Bora kabisa ya kijeshi kutoka NATO kwa minajili ya kuja kukabiliana na adui wa aina ya Urusi.

Sasa basi Urusi aljua fika uwezo wa jeshi la ukraine ,ambalo linadaiwa lilikua ni kubwa kuliko nchi yoyote pale ulaya nasema kubwa kwa maana ya idadi ya watu.

Urusi fika kabisa alijua kua Ukraine imejengwa imara kabisa kijeshi Tena kwa viwango vya NATO.

Achilia mbali kujengwa Bali pia Ukraine ilibahatika kupata ushauri makini kabisa kutoka kwa washauri wa kivita na kiitelijensia kutoka kwa makamanda bora na vifaa Bora kabisa kama satellite kutoka USA UK Canada German France Poland n.k

Lakini Urusi aliamua kuivamia Ukraine kwa Nia ya kuivunja nguvu Ukraine kijeshi.(demilitalization). Bila kuogopa wala kujali uwezo huo wa Ukraine niliouelezea hapo juu.

Sasa kile wewe unachokiita performance mbovu aliyoonesha Urusi sio performance mbovu Bali ni kuivunja nguvu kijeshi nchi kama Ukraine sio jambo dogo wala sio lelemama.
Hapo mwanzo jeshi la ukraine lilikua bado jipya kabisa na imara kabisa halijaguswa na likiwa limekamilika.
Kwa Hali hiyo ni lazima jeshi Urusi lilipata uponzani mkali sana.Halikuweza Kuua askari wa Ukraine bila wao kufa,isingewezekana kulipua vifaru vya Ukraine bila vya Urusi kulipuliwa,vivyo hivyo kwa zana nyingine.kwa hiyo mwanzo ilikua ni piga nikupige kwa saa,siku,wiki,mwezi na hatimae mwaka hatimae kidogokidogo jeshi la ukraine likaanza kupoteza nguvu zake na jeshi la Urusi likaanza kupata mafanikio.

Katika Hali kama hiyo Urusi alipata ugumu sana mwanzo sio kwa sababu Urusi alikuabdhaifu,no,Bali kwa sababu Ukraine ilikua bado Iko imara kabisa.
Urusi hapa anatakiwa apewe maua yake alianza kulivunjavunja jeshi la ukraine hatua kwa hatua.
Hali aliyopitia Urusi hakuna nchi isingeweza kuepuka kupitia kama ikiingia vitani na nchi kariba ya Ukraine.mafano,USA ilipoteza askari na vifaa Vietnam, Iraq, Afghanistan, somalia n.k
Kwa kifupi Urusi ime perform vizuri toka mwanzo hasi Leo,Hali aliyopitia ni suala la hatua kwa hatua.
Kumbuka west ndio waliokua wanaasisst kwa kumpa Ukraine apige wapi na Kuna Nini Cha kupiga.mfano Moscova.


Kuna mdau kasema huko juu kua Urusi haiwezi hata kupigana na Marekani wala china. aisee Kuan watu ni wabishi hatati.
Unajua hakuna kipimo kizuri kama matokeo.matokeo ya mtihani ndio yanatufanya tujue mtoto ana akili za darasani ama Hana.

Nasema matokeo kwa sababu Gani?
Je Kuna msaada ambao Marekani alikua hajautoa kwa ukraine ama kamaliza?
Sasa kama hajamaliza anasubiri Nini? Anapenda waukraine wafe kama nzige?
Ama anashirikiana na Urusi kuwahujumu Ukraine?

Kwa kifupi Marekani katoa misaada ya silaha Kwa Ukraine kwa kadri ya uwezo wake na haijasaidia kitu na waukraine wanaelekea kushindwa.sasa hapa kilichompeleka Marekani kusaidia ni Nini kama msaada wake hautoshi?
Kwa kifupi Hana uwezo wa kumshinda urusi kijeshi.

Matokeo mengine.
Mdau katuambia Urusi hawezi kupigana na Marekani na hata china,sasa nachoshangaa ni Marekani ipi hiyo inayoweza kumpiga Urusi?
Je ni hii hii iliyoacha silaha Afghanistan baada ya kushindwa na kikundi Cha wanamgambo Cha Talaban?ambao hawakusaidiwa na nchi yoyote duniani?
Ama kikundi Cha waasi Cha somalia?
Ama Marekani hii iliyoshindwa na Vietnam?

Pia mdau kasema Urusi Haina sijui manpower au population ni ndogo.hivi si tulikubaliana kua vita vya Sasa ni vita vya technolojia havihitaji sana idadi ya watu?

Ukweli ni kwamba performance ya Urusi katika vita hii Iko katika ubora huohuo hivyohivyo toka mwanzo Hadi Leo.
Kuivua nchi uwezo wake wa kijeshi ni jambo geni hapa duniani na sio jambo jepesi,hii ni vita vya kufa na kupona Kwa nchi inayotaka kuvuliwa Tena Kwa nchi inayoungwa mkona kwa misaada yote ya Hali na Mali na mataifa ya West na NATO.
Urusi ni kubwa zaidi ya tulivyokua tukiaminishwa inastahili heshima yake.

NATO nzima na west walikua bize kupambana na urusi walipeleka Kila aina ya silaha, intelligence fedha na vikwazo lakini wapi.

Sio wachambuzi wa kimagharibi waloiidharau Urusi,Bali waliofeli ni majasusi wa west na NATO uwezo wao ulifikia mwisho hawakuweza kujua uwezo wa Urusi kwa Kila kitu,kiuchumi,kijeshi na kisiasa za ndani na nje.
Hapa pia imeonesha kua,Urusi kijasusi Iko juu ya west.haya sio maneno yangu,Bali ni ushahidi wa matokeo ya tunayoyaona Leo.
 
M Mrusi hana hizo submarines? , unachofanya ni kuonesha mahaba yako Kwa Marekani, ila Kwa sasa Mrusi ameonesha Yuko vizuri. Marekani angeonesha uwezo wa kulinda anga la ukreni ningekusapot.unajivunia madege yenye uwezo wakuipiga Libya siria au ilaq nchi zenye mfumo duni wa ulinzi. Hizo ndege hata Kwa Irani haziendi zitadunguliwa tu. Hepbu nipe mfano ambapo Marekani alishinda vita. Tofauti na kutumika nyuklia kile japani
 
Misaada iliyopata Ukraine mingi ilikuwa ya kuweza kujilinda tu hii ya kufanya offensive inakuja kwa kusuasua tu na kwa uchache.

Hizo himmars alizopewa zipo 20 tu, Atacms zimekuja kwa kuchelewa sana, vifaru pia vimekuja vichache tena kwa kuchelewa sana (tena havijafika hata 300+), kumbuka pia hairuhusiwi kutumia hizo silaha kushambulia ndani ya Urusi.

Ukraine imejitahidi mno mpaka sasa kwanza kuzuia Kyiv isianguke mwaka 2022 na mpaka sasa kufanya Vita iendelee.
 
You nailed it!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Usikute Marekani wameshaanza kumchumbia huyu Meya ili kutafuta namna na kisingizio cha kumtosa Zelensky.

Namfananisha Zelensky na Osama Bin Laden. Baada ya kutumika hadi akatumika, then akatoswa. Akaamua kuwageuka mabosi zake.

Zelensky anaulizwa na mabosi zake wa NATO:

^Unaionaje SMO ya jamaa na counteroffensive yako? Vipi kuhusu kufanya naye mazungumzo ya amani ili kusitisha vita; muda si huu sasa?^

Zelensky: ^Not gonna happen. I just massacred my own people for nothing?^
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…