Urusi anasaidiwa na Iran,Korea Kaskazini kupigana na Ukraine
Ningekua Mimi ndio wewe wala nisinge ng'ang'ania kauli hii ya kua Urusi inasaidiwa na Iran na Korea kaskazini kwa sababu kauli hii inawaaibisha sana west.
Nadhani Pro west wenzako wanaona aibu wenyewe Kwa kauli Yako hii ambayo unaipenda sana lakini wanashindwa kukuziba midomo maana inaaibishano uwezo wa west dhidi ya Urusi.
Kwa sababu kauli Yako hii inaprove uwezo mkubwa wa Urusi na kuprove wrong uwezo wa west wote.
Kwa sababu kumbe na Kwa maana Yako na kwa kilio chako Cha muda mrefu ni sawa na kusema kua
I) Urusi peke yake ni sawa na nchi zote za west kijeshi.
ii)na kwa sababu west wamemshindwa Urusi basi ni Kwa sababu ya msaada wa Iran na Korea kaskazini.
Sasa sisi wachambuzi uchwara tunajiuliza huo ukubwa wa west kijeshi tuliokua tunaaminishwa uko wapi?
Kibaya zaidi hizo nchi Tatu TU yaani Urusi Iran na Korea kaskazini mlikua mnatuaminisha ni nchi masikini na third world countries.sasa Leo nchi masikini Tatu zimeweza kuzisimamisha nchi tajiri donor kantris 50.
Aisee kumbe tulipigwa pakubwa.
Namkubuka Putin alikua akisema huku anacheka kua,
"Katika vita vya propaganda hakuna nchi inaweza kuishinda USA na west."
Hivyo hiyo kauli Yako ya kua Russia inasaidiwa na Iran na Korea kaskazini inazidhalilisha mno nchi za First World,NATO,EU na west wote ambao humu hua tunaambiwa ni doner countries,Kuna watu humu hua hawaishi kusema hivi Urusi imewahi kutoa misaada Gani kwa Afrika?
Ooh Korea kaskazini ni nchi masikini sana raia wake wanatoroka nchi,ooh Iran ni third world country.
Sasa Leo hawa masikini watatu ndio wa kuwazidi akili matajiri wa Dunia?
Sasa Leo Mimi najiuliza hivi ilikuaje pale Urusi ilipokua kamili yaani USSR ambayo ndani yake kulikua Kuna akina Ukraine, Georgia, Lithuania, Beralus, Estonia,Moldova,Latvia, Azebaijan, Kyugistan, Tajikistan, Turkmenistan, Kazakhstan n.k?ambazo zote hizi ukiongeza na Russian federation ndio unapata USSR.
Sasa hapa ukiongeza na wazee wa Warsaw pact akina chekoslovakia,Hungary,Romania,Burgaria,Poland n.k unafikiri NATO walikua na Hali Gani?