Mkuu Mzee Ngonyani heshima kwako.
Kuongezea maneno Yako uko sahihi 100 kwa 100.
Kwa miaka mingi ama Kwa miaka yote nimekua nikijua na pengine wengi wetu tumekua tukijua kua Teknolojia zote kubwa zinatoka nchi za Magharibi.
Na ninaamini kua vifaa vya kijeshi ndio vifaa vilivyoyengenezwa kwa Teknolojia ya Hali ya juu sana kuliko vifaa vingi,mfano Satellites za kijeshi ziko juu sana lkn zinaweza kuona picha na mienendo ya vifaa vya kijeshi vilivyopo ardhini na hata vinavyotembea.
Rada zinaweza kuona vitu vinavyokuja uelekeo wa ilipo rada kutokea mbali sana.
Mfano Satellites na lada zinaweza kuona ndege ikiruka kutoa nchi moja kwenda nchi nyingine,
Kuna Teknolojia kubwa sana kwenye vyombo vya kijeshi vipitavyo kwenye maji,baharini,ziwani au mitoni,lakini Kuna vyombo pia vya kuviona vyombo hivyo vya majini vikiwa mbali.
Kuna silaha zikirushwa au kupiga hazionekani kwenye rada mfano ndege za USA kama B2 na makombora kama ya hypersonic ya Urusi n.k.
Kuna vifaa vya mawasiliano vya hali ya juu sana, na pia kuna ndege za upelelezi ambazo zikipita TU juu ya anga lako zinapiga picha chochote watakachotaka kupiga,mfano kupiga picha sehemu mlizoficha silaha n.k.
Kuna vifaa vya ujasusi vilivyotengenzwa kwa Teknolojia ya Hali ya juu sana Kwa ajili ya kupelelezana kijeshi.
Nimeandika haya kwa ufipi sana ili kuonesha TU Kuna Teknolojia kubwa sana kwenye zana za kijeshi,lakini yapo makubwa zaidi ya haya.
Kwa Nini nimeanza kuandika juu ya Teknolojia?
Nimeandika hivyo ili kukuonesha nilivyokua naelewa zamani na jinsi Urusi ilivyonishangaza.
Kwa miaka yote nilikua naamini Magharibi yaani USA, UK, German,France, Italy, Norway, Denmark,Sweden, Holland, Spain, Portugal,Greece, Turkey,Japan ukiondoa wale waliokua upande wa USSR akina Poland,Romania, Bulgaria, na wenzako,niiiamini na ninajua hao west wa zamani ndio waliokua wana Teknolojia ya Hali ya juu sana,hivyo kupeleka kua na majeshi yenye uwezo mkubwa sana hapa duniani.
Kama nilivyokua najua na ninajua Hadi Leo kua west ndio nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani,hivyo kwa advantage hizo Tatu za Teknolojia,Majeshi ya Hali ya juu na uchumi mkubwa,Urusi alipoanzisha SMO hakika nilijua huo ndio utakua mwisho wa taifa liitwalo Russian Federation,kwa sababu USA na NATO waliionya Urusi isijaribu kuivamia Ukraine.
Ukweli ni kwamba hii ni ajabu ambayo Mimi bado nashangaa,
Kumbuka Hao west wala hawatanii,wala hawaionei huruma Urusi,wao ukifatilia kauli zao utaona walijipanga kuiharibu kabisa Urusi ikiwezekana isambaratike tena, ili kuwe na vi nchi vidogovidogo.
Kumbuka waliipiga vikwazo vya Kila aina na kuianzishia vita ili ichoke haraka ,ikiwezekana Urusi kutokee machafuko,Putin aangushwe,nchi ivunjike vipande.
Waliiandaa na kuijenga Ukraine kisilaha na kijeshi na mbinu za kivita kwa viwango vya juu kabisa vya NATO kwa ajili ya kuja kupigana na Urusi,walijengea miundombinu imara na Bora kabisa ya kijeshi kwa ajili ya kuja kupigana na Urusi.
Walijenga makambi ya kijasusi ambayo yalikua yanaendeshwa na CIA zaidi ya kumi na mbili ndani ya Ukraine huku wakiwafundisha Majasusi wa Ukraine kuichunguza Urusi na kuihujumu,ndani ya hayo makambi kulikua Kuna Majasusi kutoka nchi kadhaa za NATO hususani MI6 wa UK.
Tazama umoja huo wa nchi zenye uwezo mkubwa namna hiyo,zimeunganisha nguvu kwa ajili ya kukabiliana na nchi moja TU ambayo Iko peke yake yaani Urusi.
Kwa kusoma TU alama za nyakati ni kwamba kama majeshi ya Ukraine yangefanikisha kazi waliyopewa bila kujua, ya kuidhoofisha Urusi angalau kwa 60% TU, naamini NATO wangeingia mazima kumsaidia Ukraine Kuipiga Urusi.
Ukitaka kuamini haya angalia idadi ya misaada ya silaha fedha na ushauri wanaompa Ukraine ndo utaona ni jinsi Gani walikua wanatafuta upenyo wa kuingiza majeshi Yao kamili.
Hakuna nchi duniani iliyowahi kupewa misaada ya silaha na fedha kwa ajili ya kupigana na nchi nyingine hapa duniani kama iliyopewa Ukraine,Lkn hebu angalia NATO waliingia kijeshi Yugoslavia,Iraq na hata Libya,je wnashindwa Nini kuingia mazima Urusi?
Mwaka Jana tuliona ndege za USA UK na Fra zikidungua makombora ya Iran yaliyoelekezwa Israel Hadi Zelensky akalalamika mbona hawadungui makombora ya Urusi kuelekea Ukraine?
Juzi hapa tumeona USA imepelekq ndege Kwenda kupiga Iran wakati Iran ikipogana na Israel,mbona hwafanyi hivyo Kwa Ukraine?
Wanachofanya ni kulipa Ukraine silaha na wao kupigana kwa "kificho."
Mkuu Mzee Ngonyani sio kwamba NATO hawako Ukraine,wapo sana na wanauliwa Kila siku wakiwa kwenye mahandaki , command center,wakiendesha vifaa ambavyo Ukraine hawawezi kuviendesha, lakini ki ukweli wanakutana na mkono wa Putin.
Mkuu hii ni vita, na kama ulivyosema nchi moja ikipigana na nchi nyingine, halafu hiyo nchi nyingine ikapata usaidizi na kutoka west,ujue hiyo nchi kutoboa ni miujiza,lakini Urusi imeni prove Wrong.
Kwa vita hii ya Ukraine,Urusi imewamudu west wote kwa pamoja.
Ukweli ni kwamba kama vita hii ingekua ni baina ya Ukraine na Urusi peke Yao, Leo hii Ukraine yote ingekua chini ya Urusi,lakini ni ukweli usiopingika Kwamba, west wote wamefanikiwa kumchelewesha Urusi kumaliza malengo yake haraka.
Lakini pia ni ukweli usiopingika kua, kwa uwezo Urusi ilionao imeweza kuzima kabisa matamanio ya west, kutaka kuidhoofisha au kuishinda Urusi.
Kwa kumalizia na kwa maoni yangu Mimi ni kwamba, Hadi kufikia Leo hii 03 August 2025 Urusi ndio mshindi wa vita hii, kwa sababu ameweza kuchukua sehemu kubwa ya ardhi ya Ukraine, na ameweza kulidhoofsha kabisa jeshi la Ukraine, na Ukraine haitajiunga na NATO asilani.
Leo hii vijana wa Ukraine wamekua wakitekwa na nchi Yao ili kwenda vitani,wakati huko Urusi,vijana wanaomba wenyewe kujiunga na jeshi.
Wakati huohuo Kuna wimbi la wanajeshi wa Ukraine wanajisalimisha Kila siku kwa majeshi ya Russia.
Urusi peke yake imeweza kuwamudu muungano wa nchi zote za Magharibi.