Wafahamu watu ambao ndo humpa ushauri wa kitaalam raisi wa Russia Vladimir Putin, waitwa Sloviki au kwa kiingereza Men of Force.
Hawa wakisema wamesema na neno lao huwa limeshiba ni sehemu kubwa yenye mchanganyiko wa deep state na serikali.
View attachment 2150801
Mazee.
Hao pichani ni baadhi ya mazee wanounda baraza kubwa la Usalama la Russia.
1. Nikolai Patrushev- mkurugenzi wa zamani wa idara ya usalama ya FSB
2. Sergey Ivanov nae amewahi kuwa bosi wa FSB na sasa ndo mnadhimu mkuu wa Kremlin ambayo ndo makao makuu ya nchi ya Russia.
3. Alexander Bortnikov ndie mkuu wa sasa wa FSB
4. Sergey Naryshkin ndie mkuu wa sasa wa idara ya ujasusi wa nje yaani SVR ambayo ndani yake imo idara ya ujasusi wa kijeshi ya GRU.
5. Victor Zolotov ni mkuu wa askari wa akiba yaani National Guard na amefanya kazi na Putin akiwa mlinzi wake.
Wanajeshi.
Sergey Shoygu si mwanajeshi bali ni mwanasiasa katika sare za kijeshi. Huko nyuma shoygu amewahi kuwa gavana na waziri na ni mmoja wa watu wa ndani kabisa wa bwana Putin au "Inner Circle".
Shoygu amesimamia operesheni za kijeshi nchini Syria, Crimea na sasa Ukraine.
Yeye pamoja na jenerali Gerasimov ndo sasa waongoza operesheni nchini Ukraine.
View attachment 2150807
Waziri wa ulinzi Sergey Shoigu (kulia) na Valery Gerasimov ambae ni mkuu wa majeshi. Picha na Reuters.
Wanasiasa
1. Vyacheslav Volodin ndie mwenyekiti wa bunge la Russia maarufu kama Duma na ndie aliesimamia uamuzi wa kuivamia Ukraine kwa kura nyingi za wabunge.
2. Anton Vaino ndie mkuu wa shughuli za Kremlin.
Wenye pesa au Oligarchs
Hawa ni mabilionea na vijisent vidogo ndo vilivyozuiwa kwenye mabenki huko Ulaya Magharibi. Hawa wana uhusiano na humsaidia Putin katika masuala ya biashara na kuiweka nchi iwe na ustahimivu katika masuala kama madeni ya nje na kuhakikisha uchumi imara.
Wafuatao hapo chini ni baadhi yao.
View attachment 2150825
Kwenda kulia kutoka juu kushoto: Oleg Deripaska, Roman Abramovich, Alexey Miller, Nikolai Tokarev, Andrey Kostin, Igor Sechin and Dmitri Lebedev. Picha na AP
Wa nje ya Russia au Proxies
Walowekwa kando wajifunze kazi.
Dmitry Medvedev
View attachment 2150834
Medvedev alibadilishana uraisi na uwaziri mkuu kati ya mwaka 2008 na 2012. Huyu yupo kimya akifanya shughuli zake Kremlin ila hujibu hoja za hapa na pale.
Pamoja na hayo makundi niloyataja hapo juu, bado raisi Putin ana mtandao mkubwa sana duniani pamoja na marafiki wa kuazima.