Kaka tafadhali tusiangukie haraka mno peopaganda wa upande mmoja jinsi wengi hapa wanavyofanya. Si rahisi kuona yote, maana ukweli ni mhanga wa kwanza wakati wa vita.
Nguvu ya jeshi la Kirusi ni tishio la silaha za nyuklia. Hakuna anayetaka vita ya nyuklia, (ingawa wote wanatishana) kwa sababu itaendeleea haraka kuharibu yale unayotaka kutetea, pamoja na maadui wote pia nchi yako mwenyewe.
Menginevyo hata mimi nilitegemea Urusi itashinda Ukraine haraka, sasa naendelea kushangaa udhaifu wa jeshi hili kubwa. Wiki nne! na bado linakwama mbele ya miji.
Umetaja mfano mmoja muhimu, uvamizi wa Crimea mnamo mwaka 2014. Ila sababu ya kufaulu bila upingamizi - sioni nhuvu ya kijeshi, zaidi nguvu ya kiuchumu. Maana nchi nyingi za Ulaya zinategemea mafuta, gesi na makaa kutoka Urusi. Pia makampuni ya Ulaya yalifanya biashara na Urusi. Hapa Waulaya walisita kujibu kwa ukali, ingawa mwaka ule Putin alianza kuvunja sheria ya kimataifa waziwazi.
Sasa kuna hasira kati ya wananchi wengi wa Ulaya wakiona wakimbizi pamoja na picha za uharibifu. Hapo wanasiasa wanasukumwa kuchukuia hatua, na pia makampuni makubwa yameamua kuachana na mali yaliyowekeza katika Urusi.
Hii ni tofauti mwaka huu kuliko 2014, Tuone wataendelea hadi wapi kubadilisha vyanzo yva nishati, maana bado Ujerumani inalipia Urusi $ milioni 200 kila siku kwa gesi ila wanatafuta njia mbadala sasa. Poland itafaulu mwisho wa mwaka kuachana na gesi ya Urudi, lakini bado wanategemea makaa mawe kutoka Donbass.